Poleni sana vijana wangu wa TMAA

mkuu kote huko njaa tupu ndio mana juzi kati kipindi cha uchaguzi wote walikimbilia kwenye ubunge si unaona DED gaita kalitapika lile V8
Mkuu niamini ,wateule wa JIWE wanapiga pesa hatari,kwenda Bungeni ili wawe na uhakika wa Kupata fedha za uhakika na mikopo mikubwa! Huku wanapiga za MADILI.
 
hii nchi ya jabu sana.

yaani kuna taasisi top officials wanalipwa 5mil net.
kuna taasisi nyingine za serikali hiyo hiyo watu wanalipwa 15ml net.

sasa mkuu,badala ya kuangalia namna ya kupandisha na hao wengine,anafikiri namna ya kiwashusha waliopo juu,anyway wanaolipwa mishahara mbuzi ni ujinga wao wenyewe.

Sent from my ONEPLUS A3003 using JamiiForums mobile app
Kitu anachokosea ni kudhani kuwa kwa kufanya hvy anawafurahisha wapiga kura, wkt in real sense anapunguza mzunguko wa fedha na ambapo effect hiyo itawagusa hao anaodhani anawafurahisha.
 
Kitu anachokosea ni kudhani kuwa kwa kufanya hvy anawafurahisha wapiga kura, wkt in real sense anapunguza mzunguko wa fedha na ambapo effect hiyo itawagusa hao anaodhani anawafurahisha.
hapana,sifikirii kama ndio tageti yake.
 
Mkuu hela haitoshi hata siku moja, hicho sio kigezo watu wana ambition za hatari.
Issue sio kutosha bali kuna wengine wanalazimika kuchukua rushwa kwa sababu ya shida za kijinga kabisa kama kulipa ada, kuhudumia matibabu n.k! Hivyo, unapotoa malipo ya kueleweka, unapunguza risk ya rushwa kwa wengine ingawaje wengine bado wataendelea kuchukua tu kwa sababu ni hulka yao, na kama ambavyo watu wanasema, kila mmoja anahongeka, na unachotakiwa kufanya ni kutafuta tu bei yake.
 
Zoezi liende koote kwenye taasisi za hivyo. Nchi inanyooka sasa,haiwezekani woote mna degree sawa lakini mwezio anakuacha kima cha mtu mzima kwenye mshahara.
Umeongea point Kwa nini mwenye degree 2 TMAA apate mil 10, huku kwingine mil 1.5?. Hii ni kawaida kwenye mashirika ya Umma MTU hajasoma anamzidi mshahara mwenye elimu. Ndio maana morali ya kazi inakufa na majungu ndio mtaji WA kupatia vyeo.
 
Mkuu haya mawazo ya kimaskini ukweli utabaki hatuwezi kufanana kamwe..kumbuka kuna taasisi zinazalisha TRA,PTA NK hivyo watu wanafanya kazi kubwa kuingizia mapato serikali na kuna zingine zinatumia tu pesa za serikali bila kuzalisha hivyo hawawezi kulingana malipo.

Messi na Ronaldo wanalipwa hela nyingi kuliko Samatta lakini ndo wanafanya kazi kubwa kila msimu na wanaziingizia timu zao vipato vikubwa hivyo hawawezi kulipwa sawa na mtu kama John Bocco.
Zoezi liende koote kwenye taasisi za hivyo. Nchi inanyooka sasa,haiwezekani woote mna degree sawa lakini mwezio anakuacha kima cha mtu mzima kwenye mshahara.
 
Ndio maana watumishi wengi biashara zao zinakufa mapema na wenye hela ndefu wanawekeza mwenye majengo sababu risk ni ndogo
Eeh real estate ndio biashara isio na stress kabisa, wakiingia wapangaji wewe ni kuvuna tu. Umekaa zako mahali watu wanakutengenezea hela tu.
 
1. Je, taasisi husika inazalisha?! Taasisi zinazozalisha pesa kama TPA, TANAPA kwa kawaida wanalipwa vizuri kwa sababu wao ndo cha mapato serikalini.

2. Je, taasisi husika ina vishawishi?! Taasisi zenye vishawishi huwa wanalipwa vizuri ili kuwapunguzia kudaanganyika hata kwa virushwa mbuzi! Hapa ndo wanaingia TRA na TMAA. TRA always wanacheza na pesa. TMAA hawa wanafanya ukaguzi wa madini yanayozalishwa na kampuni mbalimbali.

3. Wingi wa waajiriwa: Ukishakuwa kwenye taasisi ambayo watumishi wengi ni wengi, sahau kupata mshahara wa maana! Hili ndilo linawakumba kada kama za Waalimu na nyingine kama hizo. Leo hii ukisema mwalimu apate angalau 1M basi huenda kodi zote za TRA zikaishia kulipa mishahara kwa walimu!!

Lakini yote kwa yote, busara ni kuboresha mishahara ya wote hata kama isipokuwa sawa lakini sio kushusha ya wale wengine ili eti wafanane fanane.
Asante kwa kumjibu kantalambaz
 
Kuna watu wanadharau sana boss, kisa ana mshahara wa mawinguni...utasikia anakwambia "wewe mimi mshahara wangu wa mwezi mmoja nawalipa mishahara nyie 10"emoji57]
sasa akikwambia hivyo wewe inakuuma nini boss wangu? Ongeza juhudi na maarifa ili umzidi kipato
 
1. Je, taasisi husika inazalisha?! Taasisi zinazozalisha pesa kama TPA, TANAPA kwa kawaida wanalipwa vizuri kwa sababu wao ndo cha mapato serikalini.

2. Je, taasisi husika ina vishawishi?! Taasisi zenye vishawishi huwa wanalipwa vizuri ili kuwapunguzia kudaanganyika hata kwa virushwa mbuzi! Hapa ndo wanaingia TRA na TMAA. TRA always wanacheza na pesa. TMAA hawa wanafanya ukaguzi wa madini yanayozalishwa na kampuni mbalimbali.

3. Wingi wa waajiriwa: Ukishakuwa kwenye taasisi ambayo watumishi wengi ni wengi, sahau kupata mshahara wa maana! Hili ndilo linawakumba kada kama za Waalimu na nyingine kama hizo. Leo hii ukisema mwalimu apate angalau 1M basi huenda kodi zote za TRA zikaishia kulipa mishahara kwa walimu!!

Lakini yote kwa yote, busara ni kuboresha mishahara ya wote hata kama isipokuwa sawa lakini sio kushusha ya wale wengine ili eti wafanane fanane.
Kuna watu hawaingizi kipato serikalini ila shughuli yao sio ndogo mfano 92 kJ makomando ngerengere hapo.
Kuna haja ya kuwa na salary debate chini Tanzania
 
Back
Top Bottom