Poleni sana vijana wangu wa TMAA

Hili halitaishia kwa watumishi waliokuwa TMAA pekee, litaenda pakubwa sana. Taasisi zinazolipa CEO na DG zaidi ya 12M zipo za kutosha.

Ila mzee mkubwa anafanya kazi kwa mihemko sana, hii ni hatari sana!!!
Mimi namkubali. Alichofanya ni sahihi
 
Wapigwe chini tu maana walimu na wauguzi kule vijijini hawana mishahara mikubwa lakini ni majembe kweli wanapiga kazi mno tena hawatoshi lakini hawaachi kazi huo ndio uzalendo wakweli ikikuuma acha kuna na biashara nyingi za kufanya mtu unalipwa mamilioni ya hela kwa mwezi unashindwaje kuishi wakati wenzio wa laki tatu na wanasomesha hadi ndugu zao shame
 
wewe unafanyia kazi serikali hiyo hiyo unalipwa kama ofisa wa serikali ya Ulaya wakati mwenzio analipwa kama anafanyia kazi serikali fulani ya Afrika.

Ndo maana hatukomai kuwa wajasiriamali. Ukipata ubosi ndo kila kitu. Au ukipata kazi TMAA au TRA umemaliza
 
Zinakusanya zilizozalishwa na wazalishaji
yaani maana yake kama tunaangalia kwa namna sawa,haitakiwi hawa walipwe mbuzi,wengine ng'ombe.

maana humo humo kuna watu wanafanya kazi nzito sana na wanalipwa mbuzi,yaani mambo ni shaghala baghala.
 
Umeongea point ya msingi sana kila kazi ina umuhimu wake huyo anaekusanya mamilioni asingeweza kukusanya bila kupita kwa mwalimu
...mkuu hii dhana sio sahihi..hakuna mtu asiye na umuhimu kwenye sekta ya kazi au Aliye muhimu kuliko wote..watumishi wote ni sawa uki-analyse critically...mfano mdogo huyo aliyeko kwenye mzunguko mkubwa wa pesa akiumwa anamhitaji daktari maana pesa anazosimamia haziwezi kumtibu..pia anahitaji ulinzi wa polisi na jeshi ili aishi kwa usalama&amani..kifupi tunategemeana kama viungo vya mwili hakuna anayemzidi wenzake kwa umuhimu
 
Na huo ndio uzembe mwingine uliofanyika kwa nini taasisi za serikali zisiingizwe ktk scale za serikali(TGS) toka awali?
Kuna sehemu kama taifa tuliyumba na kuachia watu mianya madhara ndio tunayaona sasa.
 
..mkuu upo right kwenye baadhi ya maelezo but sio kweli kuwa usa watu wenye akili tu ndio wanaingia NASA...usa kuna best students wengi wanaenda kwenye fani ya upolisi, ufundi magari, usafi wa mazingira,etc na wanalipwa vizuri kuliko huko NASA..kule kazi ni passion kwanza kuliko salary.
Hapana mkuu,NASA ni moja ya tasisi ambayo staff wake wanalipwa vizuri,wizara/taasisi zinazolipa vizuri USA zinafahamika wala sio kitu cha kuficha,hata katika jeshi,jeshi la anga la marekani wanafahamika kwa kuwa na malipo mazuri.hata training academy zao zipo classic sana tofauti na wengine,hiyo ipo wazi hata ukienda youtube utakuwa documentary kibao na videos zipo.Point yangu ni kwamba,tuangalie namna ya kulipa watu wetu mishahara kuendana na uhalisia wa maisha ili kusiwe na haya malalamiko,ila sio kupunguzia watu mishahara kwa nguvu
 
Huyu mnyampara uwezo wake wa kufikiri uko < average afadhari angewastishia ongezeko la mishahara hao anaoona wana mishahara mikubwa wakati huo huo akiwapatia nyingez wale anaoona wana mishahara ya mbuzi kama member mmoja alivyisema hapo juu
 
Me naona ni wivu na umasikini tu kwa sababu sijaona mkiongelea kupunguza mishahara mikubwa na kuwaongezea wenye midogo
Lakini sijaelewa unavyosema mishahara iwe sawa unataka mkurugenzi wa TRA alipwe sawa na Askari wa level ya chini kabisa au mwalimu mweye certificate?
Ni kitu ambacho hakipo

Swala la kujiongezea mishahara ni kwamba kwa mfano mkurugenzi kapewa Taasisi ina wafanyakazi 1000 labda kawakuta na mishahara yao kama ilivyo lakini makusanyo ya Taasisi kwa mwezi labda ni bil10 na imekuwa hivyo kwa miaka mingi tu Sasa uongozi wa mkurugenzi huyu mpya ukawa wa tofauti kidogo
Makusanyo yakapanda mpaka kufikia bil20 kwa mwezi maana yake ufanyaji kazi lazima utakuwa umeongezeka kidogo miongoni mwa wafanyakazi
Wakaona tukiongeza watu 100 kwenye ajira majukumu yatakuwa sawa kwa sababu kazi zimekuwa nyingi kidogo
Sasa kwa sababu hiyo watu wakijiongeza mishahara kuna tatizo gani hapo?
Makusanyo yakiongezeka tena wajiongezee tena, yakiongezeka tena wajiongezee tena hawa wengine ambao sio wakusanyaji wabaki tu stagnant wakati wenzao wanapaa?
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom