Nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
315
888
kwanza namshukuru Mungu Mtoaji wa vyote, endapo atanibariki uongozi wa juu wa Taifa letu la Tanzania nitafanya haya yafuatayo;

1. KUHUSU KATIBA
Nitaruhusu katiba inayopendekezwa na wananchi wengi kwa kupigiwa kura

2. KUHUSU MUUNGANO
Hakutakuwa na serikali mbili kwenye nchi moja, hii ina maanisha kwamba Zanzibar itatambulika kama mkoa kama ilivyo mikoa mingine ndani ya nchi ya Tanzania. Hapa nitawapa uhuru wa Zanzibar kujipigia kura kuendelea kuwa ndani ya Tanzania au wawe nchi huru wenye madeni mengi kutoka Tanzania. Haiwezekani wazanzibar wanapata favor kubwa katika muungano huku watanganyika hawapati hizo favor kama kuwa Viongozi katika eneo la Zanzibar.

3. KUHUSU VYAMA VYA SIASA
Nitaweka masharti magumu ( uwe na zaidi ya wanachama 1 million) ili vyema vyingi wasindikizaji vipungue, na Tanzania kubaki na vyama visivyozidi 3 kwa ajili ya upinzani wenye tija kwenye nchi yetu. Lengo ni kufanya vyama imara kama Democrats na Republican kule USA.

4. KUHUSU BUNGE
Hakutakuwa na kitonga cha kitu kinaitwa VITI MAALUM kwa wanawake ndani ya bunge, kumbuka katika dunia ya leo hata wanaume pia wanaitaji kupewa kipaumbele.
-Ili kuwa mbunge wa JMT, Mtanzania yeyote ataruhisiwa kugombea ubunge akiwa na elimu angalau degree moja na kuendelea.
_ Nitapunguza wingi wa majimbo ambayo wabunge wake wengi wanaonekana tu katika kipindi cha kusaini posho. Hii inamaanisha majimbo 3 au 4 katika mkoa mmoja yanaweza kuwakilishwa na mbunge mmoja. Kwa namna hiyo mle bungeni kutakuwa na wabunge wasomi na wazelendo wasiozidi 150 kutoka wabunge wa sasa ambao ni zaidi ya 300. Hapa kuna pesa nyingi tu nitaziokoa na kuelekea kwenye shughuli za vijana nchini hasa kwenye kuwezesha upatikanaji wa Matrekta kwa wingi na kilimo cha umwagiliaji.

5. KUHUSU WAKUU WA WILAYA
Hiki cheo nitakifuta mara moja na majukumu yao yatatekelezwa na wakurugenzi wa Halmashauri. Sioni umuhimu wa nchi maskini kama hii Tanzania kujibebesha majukumu ya mishahara kulipia makada wa chama kwa kitu kinachoitwa mkuu wa wilaya.

6. KUHUSU ELIMU
Kutoka elimu ya Nursery hadi chuo kikuu, lugha ya kufundishia itakuwa kiingereza, huku kiswahili kikifundishwa kama somo na kikitumika katika shughuli zote mtaani hadi serikalini. Haiwezekani viongozi wanaodai kiswahili kiwe lugha ya kufundishia, watoto wao wanawapeleka katika shule za International za English medium. Lazima vijana wa kitanzania watengenezewe mazingira mepesi ya kushindana katika soko la dunia kwa kuimidu lugha vyema lugha ya kiingereza.
- Pesa ya mishahara itakayookolewa kutoka kulipa mishahara ya wakuu wa mikoa itaenda kuboresha maaslahi ya watumishi wadogo wa umma hasa WALIMU NA MANESI

7. KUHUSU KILIMO
Nita tia nguvu kwenye mapinduzi ya kilimo (Agrarian revolution) hapa nitahakikisha mifumo ya umwagiliaji na matrekta vinakuwepo vya kutosha huko maporini kwenye mashamba. Sitafunga mipaka kwa ajili ya mazao ya kutoka mashambani, bali nitaongeza kodi maradufu kwa mazao yanaenda nje sana kwenye nchi zinazotuzunguka hapa Africa mashariki.

8. KUHUSU MICHEZO
Nikiamini katika sekta hii inachukua vijana wengi, nitaweka mazingira ya vijana wengi kupenda michezo.
  • Nita jenga VIWANJA 2 vikubwa vya michezo, 1. Kiwanja cha mpira wa miguu kitakachoitwa PELE SERENGETI STADIUM kitachojengwa Mara ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kuendeleza utalii wa Serengeti mbuga maarufu Tanzania na cha 2, kitajengwa Dodoma makao makuu kwa ajili ya kufanya michezo yote ya Olympic. Kwa kuongeza viwanja hivyo vikubwa viwili vya michezo, napenda uhakika wa kuandaa mashindano kama ya AFCON. Haiwezekani nchi ndogo kama Guinea zinaweza kuandaa mashindano haya halafu sisi kama Taifa tukishindwa kufanya kitu kama hicho.
  • Nitawezesha kuanzishwa kwa TANZANIA LEAGUE B, Ligi kuu itakayohusisha wachezaji wazawa tu ili kuinua uchumi wa vijana wengi wa kitanzania na kuinua timu yetu ya Taifa. Ligi yetu imekuwa hivyo lazima kuongeza mashindano mengi kwa ajili ya kuinua vijana kupitia michezo.

9. KUHUSU FILAMU NA MUZIKI
Hii sekta inachukua vijana wengi wasio na ajira hivyo nitawekeza nguvu na akili sana hapa.
  • kuhusu filamu, kwa sababu now days filamu zimeamia kwenye SCIENCE FICTION nitatoa vifaa vya kisasa na wataalam kutoka Hollywood na Uchina ili movie nzuri ziwe zinazalishwa za kutosha kutokea hapa hapa Tanzania.
  • Nita iruhusu JWTZ, JKT kutumia na kutoa dhana za kivita kwa ajili ya kutengeneza movie za kivita kwa uhalisia sio tuna vifaa na kambi nzuri za kijeshi vita hamna hata kuigiza movie za ki science tushindwe.
  • Kuhusu muziki na sehemu za ku shoot, nitaruhusu vibali kitolewa hata maeneo ya utalii au ikulu ilimradi kupata mziki mzuri na filamu nzuri kulingana mazingira yetu huku tukikuza utalii wetu kupitia kazi hizo za wasanii wetu.

10. KUHUSU MWENGE
Mbio za mwenge ni jambo linalokula pesa nyingi za serikali, sitafuta mbio hizi kwa sababu mwenge ni nuru katika taifa. Ili kupunguza upotevu wa pesa kutokana na mbio za mwenge nitaruhusu mwenge kukimbizwa katika mkoa mmoja nchi nzima ambao ni Kirimanjaro, mwenge ukishakimbizwa mkoani humo mara moja baada ya miaka 2 utapandishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro ili kuleta Nuru Tanzania na Africa kwa ujumla.

11. KUHUSU KUDHIBITI RUSHWA NA UFISADI
Hapa sitakuwa na masihara kwa sababu umasikini ndani ya nchi hii ni kuendelea kukubatia viongozi na mifumo iliyojaa rushwa. Fisadi itabidi kuundiwa sheria kali ya kuwafukuza kazi bila kubadilishiwa kituo cha kazi.

12. KUHUSU KUINUA UCHUMI NA BIASHARA
Tanzania sioni sababu ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa sababu kama nchi bado hatujafikia kitu kinaitwa FULL EMPLOYMENT ambapo rasilimali zote zinatumika kwenye uzalishaji. Kama ndivyo basi kunaitajika kuelekeza pato la taifa kwenye miradi muhimu ya uzalishaji bunifu na uuzaji wa bidhaa kimataifa hii itasaidia kukuza biashara ya vijana wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

13. KUHUSU MIKATABA MIBOVU
_Katika serikali yangu nitajitahidi kudhibiti mikataba mibovu ambayo seeikali inaweza kuingia ambayo inaweza kuuza utu wa Mtanzania. Mikataba ya ubinafisishaji mali lazima useme wazi manufaa kwa wananchi ni yapi kwa muda gani.
_ Kwa mikataba mibovu ambayo serikali za awamu ya nyuma ziliwahi kuingia najua zinalindwa kimataifa, sitatumia nguvu nyingi kuziridisha kwa wananchi bali nitawaomba tukutane kwenye meza ya mazungumzo tuone ni kwa namna gani wanaweza wakaboresha maisha ya wananchi. Wakigoma nadhani naweza kuwaondelea ulinzi wa kipolisi ili wananchi wadeal nao wenyewe kwa sababu wanaoibiwa na mikataba hiyo mibovu ni hao hao wananchi. Haiwezekani GGM Wanavuna Dhahabu nyingi kule Geita halafu Geita yenyewe ni maskini.

14. KUHUSU RAIS KUABUDIWA
Katika serikali nitapiga marufuku neno Baba wa Taifa kuitwa Mwl Nyerere nadhani kama Taifa hapa napo tulikosea sana, anaiestahili kuitwa baba wa taifa hili ni MUNGU pekee. Yaani sifa za kimungu tunampa mwanadamu wa kawaida kisa tu eti ni rais tena alieasisi udhaifu mkubwa serikalini. Kwa hiyo maneno na nyimbo za mapambio ya kusifiana kama ANAUPIGA MWINGI, wala mama wa taifa havitakuwepo kwenye awamu yangu ya uongozi.



Hayo ni kwa uchache nitakayofanya katika kipindi changu cha uongozi katika nchi hii. Kwa sasa nina 32 yrs na bado sijaingia chama chochote, Elimu degree ya kwanza. Mungu ibaliki Tanzania, Mungu wabaliki watanzania.
 
13. KUHUSU AFYA
Nitajitaidi Kupunguza gharama za BIMA ili kila familia hasa za vijijini zipate matibabu ya hospital kwa bei nafuu. Hilo naona litawezekana sana kutokana na kudhibiti pesa nyingi ambayo inaenda kwenye shughuli za serikali kama safari zenye misafara mirefu zisizo na maana yoyote.
 
Ni mapema sana kuijadili Katiba. Hii mijadala ya mpira,kila kona ya Jiji itakapobalika kuwa mijadala ya Katiba,huo ndio utakuwa wakati wa kuijadili Katiba.
Free and fair election haihitaji Katiba ibadilishwe. Inahitaji tu watu kukutana and to talk sharp,to talk earnestly,to 'hard talk'.
My suggestion ni kwamba Katiba inaweza kujadiliwa bàada ya 2025.
 
Andiko zuri sana. Yaani wewe ni mimi kabisa; umenakiri sera zangu. Kipindi nikiwa rais hata mimi napita humu humu.
Safi sana mkuu tuwaandikie hao wakuu wa nchi wajue wananchi wa Tanzania tunataka nini kutoka kwa viongozi wetu
 
Rais Bora kabisa kuwahi kutokea!

Ila hutaweza kuyafikia hayo Kama hutauvaa ukatili Mara mia wa JPM!
Amini nakuambia!
Kuondoa Taifa kutoka mikono ya Mabwanyenye kuipeleka kwenye manufaa ya raia wote si Jambo la kisport sport!

Kila ha kheri ktk ndoto zako!
 
14. Kazi ya Upolisi/uanajeshi ni Lazima uwe na Elimu kuanzia Certificate,

Umri wa kujiunga na Polisi na Jeshi uwe kuanzia miaka 20 na kustaafu uwe miaka 50,

na Wakuu wote wa Majeshi na Polisi umri wao wa Kustaafu uwe Miaka 50 mwisho na baad ya hapo wasipewe cheo kingne chochote yani Chochte wakitaka wakajiajiri.
 
Unazani wale walioingia madarakani hawakuwa na mipango mizuri kama hii? Unapoingia madarakani jua kuna watu wamekuweka and you will start serving their interest
 
Ni mapema sana kuijadili Katiba. Hii mijadala ya mpira,kila kona ya Jiji itakapobalika kuwa mijadala ya Katiba,huo ndio utakuwa wakati wa kuijadili Katiba.
Free and fair election haihitaji Katiba ibadilishwe. Inahitaji tu watu kukutana and to talk sharp,to talk earnestly,to 'hard talk'.
My suggestion ni kwamba Katiba inaweza kujadiliwa bàada ya 2025.
Sasa unapataje free and fair election kama hujabadiri katiba? Muongozo wa tume ya uchaguzi ipo kwenye katiba
 
Back
Top Bottom