Poleni na Kifo cha CCM, ila mimi sijalia

Poleni na Kifo cha CCM, ila mimi sijalia

Mashamba Makubwa Nalima

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2024
Posts
7,658
Reaction score
3,746
Poleni na kifo ila mimi sijalia.

Nalia na ndugu wa Ali kibao, nalia na ndugu wa Mdude, nalia na wamama hospitali wanapambania afya zao na za watoto wao, nalia na watanzania wanapambana usiku na mchana ila wanakutana na kodi za ajabu kwenye kila kitu.

Nalia na waTanzania walio na wanaouawa.

Nalia na waTanzania walitekwa enzi hizo hakuna CCTV kila mahala na cameras, kwahiyo iliishia kuwa "TLP wanatafuta umaarufu", "CUF wanatafuta umaarufu", "CHADEMA wanatafuata umaarufu", "wanajiteka hao" . Ubaya nilikuwa naamini sana vyombo vya dola pamoja na waandishi pamoja na vituo vyao, nikiamini ni kweli hakuna utekaji. Nalia na nyie, mnisamehe.

Nalia na wachimba madini wadogo mnaotapeliwa kila siku na wasiojulikana, msiwaze kuna kuna Docuseries inafanyiwa kazi tutaiachia waTanzania waone kwa macho yao wanachofanyiwa wenzao na watu waliopewa mamlaka ya kusimamia ulinzi wao.

Nalia na vitu vingi chini ya huu ukoloni, ila uzuri mahakama itaanza kufanya kazi huru. Haki itatendeka hapa hapa.
 
Nalia na mchimba madini wa Mtwara aliyeuliwa kitatili na polisi. Hawakuridhiki tu na kumuua walienda kwao wakapora na mali kadhaa za mama yake.

Jasho lako ulitakiwa kulifurahia. Nalia na wewe
 
Nalia na familia ya Shyrose, nakumbuka Spika Tulia ulikuwa unachukulia poa ishu ya utekaji, sijui ulidhani watauawa watu wanaoipenda nchi yao pekee na kubaki wanyonge mnawashika akili kwa story za AMANI ambayo nyie mmekuwa wakwaza kuipoteza hapa nchini.

Leo vijana wadogo wanauliwa kila siku na huyu binti kauliwa mkoani kwako. Vipi ni maigizo?, alijiteka?

Poleni familia ya Shyrose, najua inaumiza kiasi gani
 
proxy-image44.jpeg
 
Back
Top Bottom