Pole sana Dada

Pole sana Dada

Kwa anayejitambua hakuna shida.

Shida ni kwa wanaume wanaopenda kuwadanganya wasichana kuwa watawaoa.

Mpaka na wengine kujitambulisha kwako at last binti anaachwa solemba ndiyo tatizo kubwa Dada zetu nowdays.

Wabinti wengi wanaona vijana wengi kuwa si wa kweli ktk mahusiano bali kuchezeana tu
Mbona hata wadada nao sio wakweli. Wanashindwa kujiamini. Mara nyingi unakuta binti ana wachumba zaidi ya wawili. Likisanuka wote wanamtema. Utasemaje wanaume ni waongo.
 
Sometimes sio sisi wanaume ndo tunamakosa....maana tunapanga kweli kumuoa mwanamke na unakuta ni kweli tunapenda kutoka moyoni, sasa sijui ni pepo gani linalowakumba wadada zetu ambapo mwisho wa siku wanaonekana katika hali ya kutoeleweka, hapo ndo mwanaume anafikia hali ya kumpotezea iwe ni kwa muda au moja kwa moja.
Ni kweli mkuu. Hawatulii. Wanakuwa na waume wengi kama kubahatisha na mwishowe bahati Nasibu inawaponza.
 
Maisha sio kuolewa tu.....

(Ukizingatia walioolewa wenyewe wanajuta kwa tabia za ajabu walizonazo wanaume.... (baadhi))
Ni kweli kuna walioolewa na mambo yao si mazuri. Hata hivyo kuna waliofanikiwa. Ni kwanini ujitabirie kundi la walioshindwa na iwe sababu ya kutoolewa?
 
Tuache kuwananga wanawake wakati tatizo 75% ni sisi wanaume
Kwa asilimia kubwa wanawake wanaachwa kwa kupenda makuu. Kama vile maisha ya juu. Wengi wanakubali wanaume kwa lengo la kupata chochote na wanakuwa hawana mapenzi ya kweli. Baadae wanaanza kulia wanaume hawaaminiki!
 
Ni kweli mkuu. Hawatulii. Wanakuwa na waume wengi kama kubahatisha na mwishowe bahati Nasibu inawaponza.
Na ndo maana baadae wanakuja kufikisha umri hadi miaka 40 anakuja kujishtukia kuwa kajipotezea muda kwa kumkimbia anayefaa na kuwakimbilia wachezeaji t .
 
Poleni Sana madada wa zama hizi wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea. Mliochezea fursa.

1. Ulivyokuwa una miaka18 mpaka 22 walikuja waposaji ukasema bado unasoma. Au Wazazi wako walikwambia huwezi kuolewa bado unasoma na hujapata msingi wa maisha. Ulisahau kama ambavyo walivyosahau kuwa maisha anapanga Allah na rizki haina mahusiano na elimu. Mkasahau kuwa unaweza ukaolewa na masomo yakaendelea.

Pole Sana Dada yetu.

2. Kweli ukaendelea na masomo lakini ulivyofika form four au six ulifeli mtihani. Au ulifaulu lakini sio kwa kiwango ambacho ulitarajia ukalazimika urudie mtihani au usomee kitu ambacho hukukitaka. Au ukafika chuo kabisa lakini ukafeli. Au ukafanikiwa kumaliza chuo. Kwakuwa ni binti unapendeza na ndoa ilikataliwa walikuja wachumba wasio rasmi (maboy friend). Na ulikuwabalia maskini. Wakachill sana mkachat sana na mkatoka out. Kumbe walikuwa wanakupoteza muda tu.

Poleni Sana Dada yatu.

3. Ukafika chuo kikuu ukaanzisha mahusiano na kijana mkawa na ndoto za ndoa. Na wakaja watu wengine kuposa. Ukajibu una mtu wako. Tena kwa mbwembwe ukasema una mpenda sana (mahaba niue). Ukabaki kila siku unabadilisha profile yako kutilia mkazo kuwa umezama kimahaba. Ukasahau kuwa uchumba ni mwanamume kuja nyumbani na akakubaliwa. Kumbe alikutamani tu moyoni ulikuwa haumo ndio maana hakuona haja ya kuleta posa.

Poleni Sana Dada yetu.

4. Uliwakataliwa wengi wenye sifa nzuri za kukuoa kwasababu yake. Una maliza chuo ukiwa na miaka 27 au 28. Wale wote waliokuja kutaka kukuoa washaoa. Matokeo yake unapoteze Imani na wanaume wote. Hali ya kuwa kosa ni lako.

Pole sana Dada yetu.

5. Walikuja wenye kukuposa ukasema hawana hadhi kama yako. Unataka msomi mwenzio. Au awe na mali. Ukasahau kuwa mwanaume mwenye mafanikio huwa nyuma yake kuna mwanamke makini sana. Na hukutaka umakini huo ukitaka uzikute tu hizo mali.

Pole Sana Dada yetu.

6. Upo kazini mwaka wa tatu hajaja mchumba. Una miaka 30. wote Wanaokuja wanataka wakati matamanio yao ya kimwili tu. Na ukikumbuka ulitoa mimba kadhaa wakati unasoma kwa kuwa hukutaka mimba hiyo. Itakuharibia malengo yako ya kielemu.

Pole sana Dada yetu.

7. Walikuja watu wakitaka kukuoa ndoa ya uke wenza ukasema hutaki kusikia upuuzi huo. Ni bora usiolewe lakini kuolewa matala ni nuksi Kwako. Unataka mume wa peke yako. Kuolewa Matala ni mambo ya kizamani ukasahau kuwa hata bibi yako mzaa babu yako alikuwa ni mke wa nne kama si watano wa babu yako.

Jambo ambalo ulishindwa kulifahamu Dada yetu, ni kuwa huu ulimwengu waoaji ni wachache sana katika. Wengi ni mafukara sana, wengi ni wazinzi sana sio waoaji, wako mashoga sio waoaji, Wapo walioathirika sio waoaji, Wapo ambao ni wagonjwa wasio weza kuhimimili ndoa.............. Na walolewaji mko wengi Sana.

Maskini Dada yetu ulishindwa kufahamu kuwa ulimwengu wa Leo Waume ni kushare kama sio kw njia ya Halali basi itakuwa kwa njia ya haramu.

Pole sana Dada yetu.

8. Sasa Leo umri umeenda huna kazi hata pesa ya kukunua mahitaji ya kike huna. Wachumba uliokuwa unawaona wa nini Leo unajiuliza utawapata vipi. Masomo Umemaliza kazi hakuna. Ndoa za wake wengi ulizozikataa Leo unazitamani lakini hakuna hata anaekuuliza hali.

Umeamua ujiachie mitandaoni labda kutapatikana mchumba. Kila ajae anataka akuchezee tu.

Kazi unayo nzuri lakini hakuna mume wa ndoto zako wote wajao wanaitaka mali yako tu. Sasa unaamua unitafutie mtoto wa Zinaa kwa hoja kuwa una mali zako. Maskini Dada pole sana. Maamuzi ya mtu alipoteza muelekeo wa maisha.

Umebaki umejiinamia hujui Unafanyaje pole sana Dada yetu. Ulisahau kuwa ujana ni maji ya moto. Lakini ujana wa mwanamke ni maji ya moto yaliyomo kwenye chumba cha barafu. Au mlisahau usichana ni biashara ya nyanya.

Wale wote ambao uliona washamba kwakubali ndoa mapema wamo ndani ya Ndoa zao. Wanaitwa mama mwenye watoto wanaofahamika baba zao. Maisha yanawaendea. Na wako vizuri tu kimaisha.

Pole sana dada yetu
1479408462627.jpg
 
Kwa lugha nyepesi tuseme wanawake wanaume wote ngoma droo hakuna aliezidi mwenzie,

Wenye nia nzuri hawakutani na wenye nia nzuri wenzao, hii formula sijui ikoje.
Hapa dada ndo umeongea point. Big up!
 
Pole sana dada, hata vimini havikupendezi kwasasa!, maana goti limekomaa utachekwa na vijana huko nje
 
Mbona hata wadada nao sio wakweli. Wanashindwa kujiamini. Mara nyingi unakuta binti ana wachumba zaidi ya wawili. Likisanuka wote wanamtema. Utasemaje wanaume ni waongo.
Ni kweli hapo unakula ametegesha atakaye kuwa mkweli basi ndiyo atafanikiwa kuoa.

Na huyo wa hivyo ukirudi nyuma utakuta alishaumizwa na mwanaume kisaikolojia na hapo haamini MTU tena kama anachosema ni kweli.
 
Pole sana dada wema sepetu í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…
 
daaah sio wote wasio olewa walichezea baati au walilinga ujanani, wengine wanaupenda usingo ndo maisha walio jiamulia, afu sio ndoa zote nzuri kuna wengine wanajuta hata kuolewa usikariri
Hiyo ni kauli tumezoea kuiskia siku zote toka kwa wakosaji.
 
Hahahahhaha duh sio kwa mashairi hayaa chaa...
 
Wanaume tuna bahati sana na mambo ya ndoa. Hata uwe na miaka 50 utaona mtoto wa kike anatafuta mume wa miaka 50. Lakini huoni mwanaume anatafuta mchumba wa miaka 50.
Labda mariyoo ndio huwa hawaangalii umri wa mwanamke wao wanahitaji mwenye pesa tu.
 
Back
Top Bottom