Pole Pamella kwa kufiwa na BabaMkwe!,Pole Nakaya kwa kupoteza Baba, Pole EL kwa kufiwa na Mzazi mwenzio, Poleni wana Arumeru na PROEL
Wanabodi,
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb), amefiwa na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa mtoto wa kiume aliyemuoa binti wa Mhe. Lowassa.
Kwa vile humu jf tuna kikundi chetu kiitwacho PROEL, nawaombeni tumpe pole zetu Mhe. Lowassa!.
Nawaombeni msiulize majina na wale mnaowajua naombeni msiwataje kwa hii sio thread ya RIP bali pole tuu kwa Mhe. Lowassa kupatwa msiba!.
Pole Mzee wetu Lowassa.
Na kwa vile yeye sio member humu, pole zenu mwageni hapa nami nitamfikishia kwa vile nitahudhuria msiba huu mkubwa kwa familia ya Lowassa!
umesahau kukamilisha utambulisho wake....rais mtarajiwa wa jmt..!
Kazi uliyopewa na el ni kubwa pasco!!
huyu ndo yule mwenye majibu ya hovyo hovyo !?
Mheshimiwa Sumari alikuwa mgonjwa kabla ya kampeni za mwaka 2010 na ilijulikana wazi kabisa pasipo shaka yoyote asingemaliza kipindi chake cha miaka mitano.Nilitegemea Mheshimiwa Sumari angestaafu siasa ili apate muda wa kupambana na ugonjwa wake lakini kwa mshangao wa wengi aliingia ulingoni akahakikisha wanaCCM wenzake wenye afya nzuri hawapati nafasi ya kugombea.
Sehemu kubwa ya kampeni zake zilibebwa na Lowassa na makada wa CCM huku nguvu kubwa ya fedha ikichukua mkondo wake.Tangu achaguliwe hakupata nafasi ya kuwakisha wapiga kura wake kwakuwa hali yake iliendelea kuwa mbaya kama ilivyotarajiwa na wengi.Taifa litaingia hasara ya uchaguzi mwingine hali ambayo ingeweza kuepukika kama sheria na kanuni za uchaguzi zingekuwa zinaangalia afya ya mgombea kama wafanyiwavyo wafanyakazi wanao omba ajira sehemu mbali mbali.
Nawapa pole familia,ndugu jamaa na marafiki wa Mheshimiwa Sumari.
ah ha ha ha...King'asti umelegeza mbavu....Wifi kumbe hata kwa wanaume....BTW Pole kwa Msiba Mh. Lowassa