Pole mama Anna Mkapa, wengi wamekusahau

Jana ilikua ni siku maalum kuwapongeza wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi tukufu waloifanya...tulikuwakilisha vyema Sana bro..maandamano ya amani yalianzia Mabaibo yakaishia Calabash!
Dan MNA roho kama za wajumbe lakini mbona hamjanitumia hata tasavali nipigie!?

Jr
 
Niache unafiki mwaka 1991 nikiwa mwanafunzi wa upadre nikaenda likizo pale Parokia Katoliki ya UPANGA. Paroko akaniambia kuna kesi ya ndoa ingia pia ukasikilize upate uzoefu. Kesi ilikua ya Baba Ben na huyu Mama. Mungu nashukuru bado ulinipa ujasiri wa kuweza kuoa pia. Ben alikua BINADAMU Mvumilivu sana.
Unamaanisha Bi mkubwa alikuwa anachepuka?
 
Kesi ilikua ya Baba Ben na huyu Mama. Mungu nashukuru bado ulinipa ujasiri wa kuweza kuoa pia. Ben alikua BINADAMU Mvumilivu sana.
Siku wakijua ben alikua kachero alietukuka sjui wataweka wap sura zao...wasichkulie watu poa.yule alikua kijana wa mwalimu.ohoooo....
 
Niache unafiki mwaka 1991 nikiwa mwanafunzi wa upadre nikaenda likizo pale Parokia Katoliki ya UPANGA. Paroko akaniambia kuna kesi ya ndoa ingia pia ukasikilize upate uzoefu. Kesi ilikua ya Baba Ben na huyu Mama. Mungu nashukuru bado ulinipa ujasiri wa kuweza kuoa pia. Ben alikua BINADAMU Mvumilivu sana.
Kanisa katoliki ambalo pia Mimi ni muumini,linapokuja swala la ndoa hailishiriki watu wengi ovyoovyo hata Kama kesi inahusu waumini wa kawaida.inapokuja kwa mh mkapa sidhani kama ulikaribishwa ambaye hata ngazi ya ushemasi ujaitimu na ungeweza kuukimbia.
Ngumu kuamini kwa katoliki labda kwa Gwajima &Co
 
Kanisa katoliki ambalo pia Mimi ni muumini,linapokuja swala la ndoa hailishiriki watu wengi ovyoovyo hata Kama kesi inahusu waumini wa kawaida.inapokuja kwa mh mkapa sidhani kama ulikaribishwa ambaye hata ngazi ya ushemasi ujaitimu na ungeweza kuukimbia.
Ngumu kuamini kwa katoliki labda kwa Gwajima &Co
Kuna watu wamemwanin..dah..we kapuku et ukasikilize kesi ya raisi
 
Pamoja na juhudi kubwa za mwanamke kutafuta usawa lakini bado jamii yetu inatawaliwa na mfumo dume.(sijui kama nitaeleweka na wengi)

Benjamin William Mkapa ...Ben ametwaliwa jana kutoka maidha haya...huu ni msiba mzito kwakuwa ndio rais wa tatu wa Tanzania tangu uhuru. Tunamkumbuka kwa mema na mabaya yake..hakuna mkamilifu...lakini mizania ya haki ndio itaamua ni aina gani ya kumbukumbu ametuachia.

Kwenye kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna mwanamke (japo pia wanawake wengi wamekuwa chanzo cha anguko la wanaume wengi)...mwanamke ni kama moto au kisu..inategemea unatumiaje...!!!!

Mafanikio ya Ben Mkapa RIP mpaka kufikia kuwa rais wa nchi hayawezi kukamilika bila ya kumtaja mkewe pekee wa ndoa takatifu ya kikristo mama Anna Mkapa na mwenyekiti mwanzilishi wa mfuko wa FURSA SAWA KWA WOTE...EOTF..

Ni mama huyu wa shoka .
Aliyempa mzee faraja kitandani
Aliyemshibisha mezani
Aliyemgh'arisha upenuni
Aliyempa tumaini jipya pale mzee alipochoka na kukata tamaa
Aliyemshika mkono pale mzee alipotaka kuanguka...

Kuna ya sirini kati yao..haya hayatuhusu..hata wewe una yako...hayo ni yako mwenyewe..kuna ya nuruni..tumeyaona ...tuyaenzi yale mazuri..na yale yasiyo mazuri yawe mwalimu wetu wa kutufunza kuwa watu wema na bora zaidi

Ben kalala...apumzike kwa amani..mwendo ameumaliza..kikomo chake cha kuwa kimefika tamati...msiba wake usitufanye tumsahau mwandani wake ,kipenzi na rafiki mama Anna Mkapa..naye anastahili pole nyingi kuliko marehemu
Anabaki mjane...wajane ni wengi kwakuwa wanaume tunakufa haraka kuliko wao...tuna maisha mafupi kwakuwa sisi tunatoa wao wanapokea

Mama atabaki peke yake..mkiwa na mwenye huzuni..yule rafiki na soulmate wake hatakuwapo tena kuonekana popote..sio chumbani sio sebuleni ..hata akitaka kusema wee Ben uko wapi hataweza tena.

Ni msiba mkubwa zaidi kwakwe kuliko mamia watakaoenda msibani kwa ajili ya show off za ukwasi, urembo umaridadi na umaarufu..ni msiba mkubwa kwakwe kuliko maelfu watakaotuma salam za rambirambi

Ni msiba mkubwa kwakwe kuliko makumi ya wanasiasa watakaoutumia kujipendekeza na kujipitisha huko na huko ili waonekane kwenye camera za waandishi wa habari

Mama yetu Mama Anna Mkapa nachukua nafasi hii kukupa pole nyingi sana...nakuombea kwa Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwandani wako....

TUKO PAMOJA MAMA JAPO HUTATUONA HAPO MSIBANI..View attachment 1516078

Jr
Very touching and shows your maturity in handling social and political affairs
 
Back
Top Bottom