Msiba huu wa Baba Mdogo uliotokea Jana ( Jumamosi ). Umeniumiza mno kwakuwa Marehemu alinipa Ishara zote za Kuniaga Jumatano iliyopita

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,034
Pole sana Wadogo zangu Wawili wa damu kabisa mlioko hapa Jamiiforums na mnaoijua pia hii ID yangu Kaka yenu GENTAMYCINE kwa huu Msiba mkubwa uliotukuka Jioni ya jana Jumamosi pale Hospitali ya Rabininsia.

Poleni pia Wanafamilia ( Ndugu ) na hasa hasa Majirani wa Bahari Beach na Tegeta kwa Msiba wa huyo Baba yangu Mdogo ambaye GENTAMYCINE nina Historia nae Njema kubwa sana ya Kimalezi, Maadili na Upendo Kwangu.

Pole pia Kwako Majizzo ( Mmiliki wa EFM Radio na TvE ) kwa huo / huu Msiba wa Jirani yako kabisa hapo Kwako Bahari Beach ambaye ni Baba yangu Mdogo na ni matumaini yangu makubwa kuwa kuanzia Usiku huu na hata Kesho tutajumuika sote Msibani.

GENTAMYCINE nilikuwa mbishi Kuamini kuwa Mtu akiwa anakaribia Kufariki huwa anajua na kuna Ishara fulani huzitoa na kama ukiwa ni Mfuatiliji na Mtu makini Kihisia na Kiupeo basi utajua tu kuwa muda wowote utapokea Taarifa za Msiba.

Siku ya Jumatatu ya Wiki hii kama kawaida nilienda Kumjulia hali Marehemu ( Baba Mdogo ) Kwake na tukasalimiana vizuri na kama kawaida yake akaniuliza Maswali ya hapa na pale na nikamjibu na kuendelea na mengine.

Sasa wakati wa Kumuaga ulipofika nikaenda Kufanya hivyo na katika Hali ya Kushangaza na ilinistua pale pale na Kuhisi kuwa Marehemu alikuwa Ananiaga GENTAMYCINE ila kwa aina ya Mafumbo.

Aliniuliza ( tena mara mbili ) kwa Sura ya Huzuni je, utakuja lini tena Kuniona ( na huwa hana kawaida ya Kuniuliza ) na nilipomjibu kuwa nitakuja tu Baba Mdogo aliinamisha chini Kichwa chake huku akiepuka Kuangaliana nami na kunipa Mkono na Kuagana nae.

Kuukweli hali ile ulinipa Maswali mengi sana na Hisia kuwa huenda Baba Mdogo alikuwa Ananiaga Kimafumbo na nikawa nategemea kabisa Taarifa si nzuri kwani Malaika nilionao hawajawahi Kunifunulia Kitu cha Kimatukio halafu kisije Kutoa na namshukuru sana na mno Mwenyezi Mungu kwa Zawadi na Karama hii kubwa aliyonipa.

Hatimaye jioni ya Saa 12 kuelekea Saa 1 Usiku wa Jana ( Jumamosi ) nimetoka kupokea Taarifa mbaya ya Kufiwa na huyu huyu Baba yangu Mdogo na Kuthibitisha kuwa kumbe ile Jumatatu kwenda Kwangu kule Kumsalimia na aliyokuwa ananihoji na kunifanyia ndiyo alikuwa Akiniaga rasmi.

Sina cha Kumlipa Marehemu Baba Mdogo kwa Kunilea vyema tokea Mdogo, Kunikuza katika kupenda Dini / Kusali, Kujiamini, kutokukata Tamaa Maishani, kunipigania Kitaaluma, Kuniongoza vyema Kimaadili na Kuujaza huu Ubongo wangu kwa Madini ya Fikra na Akili Kubwa.

Nenda KAPUMZIKE Baba yangu Mdogo, Asante kwa Maisha yako hapa duniani na Ubarikiwe kwa Kuwaacha Wanao wa Kiume Wawili, Wapwa zako Wawili na Mama yao ( Mama Mdogo ) waliokupambania Usiku na Mchana bila ya Kuchoka au kukuona ni Kero au Unawakera na WALIKUPENDA na KUKUJALI zaidi mpaka jana Ulivyoaga dunia rasmi.

Haya wale Mabrazameni wote wa Oysterbay ( hasa Mtaa aliokuwa akikaa zamani Marehemu ) wa Mkadini akina Nicky Ngonyani, Mpasa, Mtui, Bary, Kifanta, Martin Mwingira (alias. Mundii ), Familia ya Mzee Mbogo, na Wengine wa Morogoro Stores msikose huu Msiba wa huyu Mzee ambaye alikuwa ni Jirani yenu na Watoto zake Wawili hawa mmecheza nao mno tu Utotoni mwenu.

Na wale wa Jirani na alikokuwa akiishi Marehemu ( Baba Mdogo. ) Bahari Beach natumai kuanzia Usiku huu huu na hata Kesho hadi Siku ya Maziko yake tutakuwa pamoja Msibani japo msianze tu Kuulizia GENTAMYCINE ni nani na yuko wapi kwani hamtonijua.

Na najua hata Watu wa Kitengo ( Msaada Kontena ) Oysterbay mtakuja kwa wingi na kujazana Msibani kuanzia Kesho na hasa Siku ya Kuaga na Maziko hivyo mkija mje Msibani tu na siyo kuanza Kudadisi dadisi sawa?

Rest In Peace Baba Mdogo BAL.

Nichukue nafasi hii pia kwa dhati kabisa kutoa Salamu zangu za Pole / Rambirambi kwa Familia ya Marehemu Mzee Edward Ngoyai Lowassa kwa Kuondokewa na Mzee Wetu huyu.

Tuko pamoja katika huu Msiba mkubwa na mzito kwa Taifa / Nchi kwani pamoja na kwamba Marehemu Mzee Lowassa alipata Ajali nyingi za Kashfa za Ufisadi ila kwa upande wa Pili wa Shilingi alikuwa ni Mwanasiasa Mwerevu, Makini, Mpenda Maendeleo na Elimu na alichukia sana kuona Watu wakijisifia kuwa Masikini badala ya Kupambana ili Kuondokana na huo Umasikini ambao kwa sasa GENTAMYCINE nauona Umehama kutoka Mifukoni mwetu na sasa upo Ubongoni / Vichwani mwetu.

Rest In Peace pia Mzee Wetu ENL.
 
Poleni sana ...Ila sasa ni utandawazi vijana wakipewa hizi dalili wanasema ushirikina ,mara mambo y kizamani..

Watu wa zamani mtu anayekufa haswa mama mgonjwa wanajua mapema maana kuna dalili wanaangalia
 
Babu yangu mzaa baba 2days before Easter 2009 aliona mtu anapita nje nyumbani kwake (huko Lushoto) akamuomba huyo mtu anipigie simu ili aongee na mimi. Kwanza alimuuliza una namba ya FULANI? akajibiwa kuwa ndio ninayo, akamwambia mpigie niongee nae,

Kwenye mazungumzo yetu aliniuliza swali moja kwa msisitizo sana, UNAKUJA LINI? Nikamwambia babu nitakuja nipo Arusha field ila nitakuja, akauliza tena LINI? Nikawa nashindwa kutaja siku namwambia tu ntakuja. Aliuliza neno LINI zaidi ya mara 3 na sikuweza kumpa jibu exactly lini nitaenda. Ilikuwa siku ya Alhamisi (tuite Alhamisi Kuu), basi baada ya siku 2 tu, yaani ile siku ya Pasaka Jumapili alitoka nje kuota jua kama kawaoda yake ambapo waenda Kanisani walimpita wakisalimiana nae, baadae alimuaga mtu fulani aliyepita akamwambia by by, akaingia ndani akajilaza kitandani na kufariki akiwa na 83yrs old.. niliumia sana.

Nimekumbuka hiki kisa baada ya kusoma kisika chako.
 
Back
Top Bottom