Pole mama Anna Mkapa, wengi wamekusahau

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
162,031
2,000
Pamoja na juhudi kubwa za mwanamke kutafuta usawa lakini bado jamii yetu inatawaliwa na mfumo dume.(sijui kama nitaeleweka na wengi)

Benjamin William Mkapa ...Ben ametwaliwa jana kutoka maidha haya...huu ni msiba mzito kwakuwa ndio rais wa tatu wa Tanzania tangu uhuru. Tunamkumbuka kwa mema na mabaya yake..hakuna mkamilifu...lakini mizania ya haki ndio itaamua ni aina gani ya kumbukumbu ametuachia.

Kwenye kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna mwanamke (japo pia wanawake wengi wamekuwa chanzo cha anguko la wanaume wengi)...mwanamke ni kama moto au kisu..inategemea unatumiaje...!!!!

Mafanikio ya Ben Mkapa RIP mpaka kufikia kuwa rais wa nchi hayawezi kukamilika bila ya kumtaja mkewe pekee wa ndoa takatifu ya kikristo mama Anna Mkapa na mwenyekiti mwanzilishi wa mfuko wa FURSA SAWA KWA WOTE...EOTF..

Ni mama huyu wa shoka .
Aliyempa mzee faraja kitandani
Aliyemshibisha mezani
Aliyemgh'arisha upenuni
Aliyempa tumaini jipya pale mzee alipochoka na kukata tamaa
Aliyemshika mkono pale mzee alipotaka kuanguka...

Kuna ya sirini kati yao..haya hayatuhusu..hata wewe una yako...hayo ni yako mwenyewe..kuna ya nuruni..tumeyaona ...tuyaenzi yale mazuri..na yale yasiyo mazuri yawe mwalimu wetu wa kutufunza kuwa watu wema na bora zaidi

Ben kalala...apumzike kwa amani..mwendo ameumaliza..kikomo chake cha kuwa kimefika tamati...msiba wake usitufanye tumsahau mwandani wake ,kipenzi na rafiki mama Anna Mkapa..naye anastahili pole nyingi kuliko marehemu
Anabaki mjane...wajane ni wengi kwakuwa wanaume tunakufa haraka kuliko wao...tuna maisha mafupi kwakuwa sisi tunatoa wao wanapokea

Mama atabaki peke yake..mkiwa na mwenye huzuni..yule rafiki na soulmate wake hatakuwapo tena kuonekana popote..sio chumbani sio sebuleni ..hata akitaka kusema wee Ben uko wapi hataweza tena.

Ni msiba mkubwa zaidi kwakwe kuliko mamia watakaoenda msibani kwa ajili ya show off za ukwasi, urembo umaridadi na umaarufu..ni msiba mkubwa kwakwe kuliko maelfu watakaotuma salam za rambirambi

Ni msiba mkubwa kwakwe kuliko makumi ya wanasiasa watakaoutumia kujipendekeza na kujipitisha huko na huko ili waonekane kwenye camera za waandishi wa habari

Mama yetu Mama Anna Mkapa nachukua nafasi hii kukupa pole nyingi sana...nakuombea kwa Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwandani wako....

TUKO PAMOJA MAMA JAPO HUTATUONA HAPO MSIBANI..
IMG-20200724-WA0039.jpg

Jr
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,619
2,000
Binadam tuna kawaida ya kusifia mtu akishatwaliwa, sio kwamba amesahaulika la hasha, muda wake haujawadia.

Mbona wakuu wameonekana wakimpa pole na kumfariji?

Huu ni wakati wa Mzee Ben kama ilivyo ada yetu mtu anapofariki.

Kuna uzi umeanzishwa na mwamba, rais wetu Nyani Ngabu ukinukuu maelezo ya Jenerali, huyo kaamua kutema ya moyoni kama yalivyo bila kuweka chujio.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
162,031
2,000
Binadam tuna kawaida ya kusifia mtu akishatwaliwa, sio kwamba amesahaulika la hasha, muda wake haujawadia.

Mbona wakuu wameonekana wakimpa pole na kumfariji?

Huu ni wakati wa Mzee Ben kama ilivyo ada yetu mtu anapofariki.

Kuna uzi umeanzishwa na mwamba, rais wetu Nyani Ngabu ukinukuu maelezo ya Jenerali, huyo kaamua kutema ya moyoni kama yalivyo bila kuweka chujio.
On serious note....Ben alinifanya nizidi kukichukia chama na kuzichukia siasa

Jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom