Pole January Makamba

Pole January Makamba

"Wazee Mliozaliwa Nchi hii kabla ya Uhuru MSAHAU URAISI"
Makamba

Ila kajamaa kana Amri aisee!
 
Nimegundua nchi hii kila mtu anaweza kuwa rais. Huyu january makamba anasifa gani ya kuwa rais wa nchi hii???? Watanzania tuwe makini na hawa watu ambao hawana chembe yoyote ya uongozi zaidi ya kutumia sifa za baba zao amabo hata wenyewe hawakuwa na sifa za kiuongozi. Kwanza hiyo tuhuma ya shule yake hajaijibu. Tujiulize kama ingekuwa nchi za wenzetu huyu kijana angeweza kuthubutu na yeye kujiita kiongozi??????? Tuache utani jamani. Sehemu alipokuwa mwanza, kuna watu ambao wanaweza kuwa viongozi wazuri kuliko yeye kila kukicha anakimbilia mwanza. Huko mwanza kwenu????? Si ungeenda tanga!!!! Mnawatumia wasukuma kuwa viongozi kwa mgongo wao wakati na wao wakiamua hata leo kupiga kura kwa mtindo wa kenya, hakuna utakachoambulia.
 
Ndugu wana jf na wa Tanzania kwa ujumla ,leo katika sikukuu hizi za Noel na Mwaka mpya na taka niwapashe yaliyo jili katika jijij la Mwanza .Jana nili bahatika kukutana na January Makamba katika hotel ya Victoria Palace,alitukusanya tulikuwa Wachungaji na Wainjilisti 152 kutoka kakitika madhebu mbalimbali ya kikristo katika mikoa ya Mwanza,Geita,Shinyanga,Mara,na Kagera.Kikao kilianza saa mbili na dakika hamsini na tisa usiku na kumalizika saa tano na dakika ishilini na tatu usiku.Katika kikao hicho January alikuwa amevalia suti yake nyeusi na shati nyeupe ikiambatana na tai nyekundu, kweli kijana ulipendeza kwa vazi hilo cha kunisiki tisha ni pale ulipo anza kujifananisha na nabii Yeremia,nilikusikiliza ukisoma kitabu cha Yeremia moja na kwamba kwa maneno yaliyomo katika kitabu hicho yanakushawishi kutangaza nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 vivyo unatuomba sisi watumishi wa Bwana tukuunge mkono na tuwashawishi waumini wetu pia.Ndugu January nikweli unashauku ya kuwa Raisi wa Tanzania lakini naomba nikuulize kupitia waraka huu maswali yafuatayo

1. Watanzania wameshuudia chama chako kupitia wabunge wake mkimzushia mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani kwamba alifanya siasa za udini kwa kukutana na watumishi wa Bwana kule Arusha ,sasa hiki ulicho kifanya jana ni Kuharalisha udini au ulikuwa unabadili dini?.

2.Mfuasi wako uliye mtuma kuandaa kikao hicho,Bwana Mustafa kada wa chama cha mabinduzi nikati ya watuhumiwa ,wa mipago hovu ya kuandaa vijana waliyo kwenda na nia ya kudhuru kule Kigoma hivi majuzi sasa nikuulize unapata wapi mamlaka ya kimahadili ya kuandaliwa kikao na mtuhumiwa wa utesi tena kikao na watumishi wa Bwana uoni kwamba unamsanifu Mungu?.

3.Ulitupatia posho ya shillingi elfu hamsini kwa kila mmoja wetu,ulitupatia chakula na vinywaji ,ulitukodishia hoteli, ulitukudishia gari aina ya costa no T926 BDP mali ya bwana Mukeshi ambayo ndiyo ili beba mabaunsa wa Matata kwenda Kigoma hivi majuzi,gharama zote ni takribani millioni ishilini tunashukuru lakini tujiulize,hizo pesa za kutuonga ulipata wapi?,kwanini unataka kununua Uraisi?,Je kwa pesa hiyo unge chonga madawati mangapi kwa ajili ya watoto wanao kaa chini uko Bumbuli? na je unafikili kutuonga sisi utakuwa umewaonga na waumini wetu?.

4.Wewe ni mshilika wa Bwana Rowasa,ambaye pia anakiu ya Uraisi kama wewe lakini pia wewe pia ni mshilika wa Ngeleja ambaye pia kiu ya Uraisi sasa niku ulize tumpigie debe nani kati yenu? ,au mnatafuta kura za sambusa yaani wawili tujitoe mmoja apite?.

5.Umelifanyia nini taifa mpaka uone unaweza kuwania Uraisi,wakati suala la tozo za simu ambalo ni mzigo wa dhambi kwa wananchi,limekushinda ukiwa kama naibu waziri wa wizara usika au una maslahi na makampuni ya mawasiliano,kama sivyo uoni ukiwa Raisi utaleta na kodi ya kusikiliza redio.

6.Unalisemeaje suala la operationi tokomeza ujangili ambayo imetesa na kuuwa wasiyo na atia wakati watuhumiwa wa ujangili akiwemo kinana katibu mkuu wa chama chako bado wana kula bata?.

7'Tuambie nini kimekushawishi kuwa na nia ya kuwa Raisi?.

8.Tuambie nikiongozi ghani wa upinzani unaona anaweza kuwa Raisi kama wewe utopata fursa ya kuwania uraisi?.

9.Kunatetesi kuwa wewe na baba yako mlishiliki kumuondoa Sherukindo kwenye nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Bumbulina kukupitisha wewe bila kupingwa kwenye CCM,Sherukindo aliye kuwa mwenyekiti wa kamati yakudumu ya Bunge ya nishati na madini ambaye alisimama kidete juu ya kashfa ya Rich mond iliyo muondoa Rowasa kwenye kiti cha uwaziri mkuu,ambaye ni swahiba mkubwa kabisa wa Mzee Makamba baba yako aliye kuwa katibu mkuu wa CCM?[Comflictof interest] leo ukifanikiwa kuwa raisi si utatengeneza mamlaka ya kifamilia?.

10.Nikumbushe ile divishion four ya formu six kule kigoma uli isafisha lini?.Au na wewe ni muhumini wa division five

11.Niambie leo unawambia nini wa endesha boda boda wa Mwanza au unaomba day waka?.

Mwisho jipime


huko kukosea kwako tu hizo spellings za maneno ya kawaida kabisa na za baadhi ya majina inaonyesha jinsi gani ulivyokuwa na wasiwasi na usiyejiamini. LAZIMA KUNA KITU katika kutojiamini huko, mi sisemi sababu najua wote humu ndani wana akili timamu. we kama vipi ipeleke kule makao makuu nafikiri inaweza kuwa ajenda pia kwani kama GONGO iliweza sioni kwa nini hii ishindwe!!!! km vp we kajipane tu.
 
Tatizo lenu pro cdm kila anaepingana nanyi ni ccm,
Mimi sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote Tz, sijawahi kupiga kura hata mara moja,
Kwa sababu Mara zote nakuwa sipo home,
Mimi nashabikia mtu sio chama,vyama vyoye vina sera nzuri lakini watekelezaji hawapo,jifunzeni si kila anaekuwa kinyume nanyinyi ni ccm,wengine,CUF,UDP,TLP, na wengine kama sisi hatuna vyama ila ni wa Tanganyika tu

Tatizo lako wewe ni kuiogopa Chadema. Wewe nini kimekuthibitishia kuwa aliyeandika "Ujangili+ubakaji+usambazaji na utumiaji sembe+ufisadi+uuaji=CCM" ni pro chadema? Kwani mfuasi wa vyama vingine CUF,UDP,TLP au mtanzania asiye na chama hawezi kuandika hivi? Hi ni vitu vinavyofanyika kwa ccm, kila mtanzania anaguswa na "Ujangili+ubakaji+usambazaji na utumiaji sembe+ufisadi+uuaji, vinavyofanya na ccm. Kama huna chama chochote wewe umeajiriwa kuitetea ccm? Acha Unafikia na uzandiki!! Kama huna chama si ukae kimya! Watanzania wanaumizwa na hivi vitu wewe unakuja na bra! bra! Ni heri ungekataa kwamba hivi havifanywi na ccm, ungeonekena wa maana kidogo!
 
Hivi hili suala la kila anayetaka urais wa Nchi hii lazima akae na viongozi wa Dini ya kikristo mbona linazidi kushika kasi.....ndio udini umehalalishwa rasmi au.....na kwanini watafutwe viongozi wa kikristo tu.
 
Makamba ni jembe, CCM mzima hakuna kijana kama Makamba..
Huyu mtu ni maarufa kuliko CCM...

Kama ni kweli jermbe, bai acche kutoa rushwa kwa viongozi wa dini! Kinachozungumziwa hapa ni kuanza kampeni za urais kabla ya muda wake na kwa njia rushwa ili kushawishi watu!
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa

Ata mm nashangaa wachungaji wengine bana vioja
 
Mawaziri na manaibu mawaziri wengi wa jk wanahujumu mamilioni wizarani kwao kwa lengo la kulainisha watu ili wapitishwe kuweza kugombea urais, january ni mmoja ya wanasiasa wanaokula 10% kutoka kwa makampuni ya mawasiliano ya ndani na nje kwa ajili ya maandalizi ya kugombea urais!
 
Du January Makamba na wewe umeingia kwenye huu uchafu?
Hivi ku-campaign 'kibongobongo' nako ni uchafu? Lakini navuta subra za Selemani anauonaje muktadha wa uzi huu.

From neutral point of view, mi naona watz kwenye haya mambo ya siasa lazima tutaendelea sana kukatwa kidizaini flani sana...maana ugombeaji wa uongozi bado uko kwa kifichoficho na inashangaza jambo hili kama ni la kheri kwanini liwe la kificho na mizengwe mingi. Mathalan kwanini wagombeaji wasijiainishe na kutanabahisha nia zao za uongozi na wafadhali wao wakafahamika na hata 'waonesha-nia' kuomba ridhaa ya kuwekewa michango zaidi ili wafanikishe nafasi wanazotaka kupata? yangu macho.
 
Hii ni hatar

hivi huyu dogo mbona anahangaika hivi?ni nani alimdanganya kuwa anafaa urais?hatutazami sura jamani tunatazama uwezo!huyu aendelee kwenda bills kucheza disco asijizeeshe wakati umri bado,tunataka "watu wazima" kama Slaa pale bwana.Si mnamuona kijana wenu kutwa kucha ni safari za Ulaya kupiga picha santiago bernebeu na kushangaa magorofa sasa mnataka mumweke mwengine mdogo zaidi yelewii,hatutaki!tunataka mbabu wetu arudishe discipline ikulu!eti Yeremia kwii kwi kwiii!jamani kama kuna baba paroko humu naomba kuuliza, nabii Yeremia alinyoa "para"?kwii kwii!
 
Tatizo lako wewe ni kuiogopa Chadema. Wewe nini kimekuthibitishia kuwa aliyeandika "Ujangili+ubakaji+usambazaji na utumiaji sembe+ufisadi+uuaji=CCM" ni pro chadema? Kwani mfuasi wa vyama vingine CUF,UDP,TLP au mtanzania asiye na chama hawezi kuandika hivi? Hi ni vitu vinavyofanyika kwa ccm, kila mtanzania anaguswa na "Ujangili+ubakaji+usambazaji na utumiaji sembe+ufisadi+uuaji, vinavyofanya na ccm. Kama huna chama chochote wewe umeajiriwa kuitetea ccm? Acha Unafikia na uzandiki!! Kama huna chama si ukae kimya! Watanzania wanaumizwa na hivi vitu wewe unakuja na bra! bra! Ni heri ungekataa kwamba hivi havifanywi na ccm, ungeonekena wa maana kidogo!

Tazama avatar yake alieandika hayo,na pia huyo member namjua sana kwa michango yake hapa jukwaani,Yule ni cdm pure,
 
Huu sasa ni unafiki, wewe ulikua nae hapo kwa masaa hayo kadhaa uliyoyasema, iweje ushindwe kumuuliza wakati mpo nae unasubiri aondoke ndo uandike huu upuuzi humu, hebu kua bhana achana na habari za kinafiki wewe.

We ushalamba hiyo posho kaa kimya, kamuongezee waifu wako mtaji wa vitumbua walau mlisongeshe, ebo.
 
1. Edward Lowassa
2. Bernad Membe
3. January Makamba
4. Asha-Rose Migiro
5. Samwel Sita
6. Fredrick Sumaye
7.
8.
9.

Patachimbika...
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa

ndo ujue vitu vingine ni kujudhalilisha...

jitu limepoke posho ,limekula,limeitikia mwaliko na mbaya zaidi limeshindwa kumuuliza haya maswali unakuja kutujazia thread za kipuuzi humu....

eti pesa anapata wapi??? kumbuka ni mbunge huyo na naibu waziri at the same t,na kila chei kina mshahara wake ujue...na wabunge ni moja kati ya mafisad wakubwa maana wanalipwa hela nyingi kuliko watumish wengine wa siasa,sasa atashindwa kuwalisha nyie wajaza tumbo..

ushatumika mkuu
 
Tatizo lenu pro cdm kila anaepingana nanyi ni ccm,
Mimi sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote Tz, sijawahi kupiga kura hata mara moja,
Kwa sababu Mara zote nakuwa sipo home,
Mimi nashabikia mtu sio chama,vyama vyoye vina sera nzuri lakini watekelezaji hawapo,jifunzeni si kila anaekuwa kinyume nanyinyi ni ccm,wengine,CUF,UDP,TLP, na wengine kama sisi hatuna vyama ila ni wa Tanganyika tu

So Kumshabikia ZITTO ndio U-Tanganyika?

Labda ni kutonye kuwa huo ni U-Kigoma au U-Dini.

Ushahuri wa bure ni kuwa jipambanunueni tu kwa vyma vyenu, Kama wewe sio CCM na pia ipi wazi sio chadema je Unashabikia chama gani? Usiniambie unashabikia Mtu.

Cuf nini wewe?
 
Nafikiri tungetafari lengo la mleta mada kwani kama hasingeliwasilisha hili tusingeweza kufahamu upuuzi alioufanya/anaoufanya J.Makamba.
Mleta mada ndio mpuuzi na ww unauhalalisha upuuzi wake sijui nakuekewe kama nilivyo muelewa yeye? Mleta mada angemuliza Januari haya aliyo yaleta hapa halafu angetuletea hayo maswala alio muuliza Januari na majibu ya Januari sio kuja kumuuliza Januari kupitia hapa jf.
 
JF imepungukiwa watu wenye uwezo wa kujadili hoja. Wamebaki mazombi tu wanaotumia hisia kuzungumza!

Mleta mada upo sahihi sana, ila kutokana na upuuzi wa wachache unaonekana hujaweka cha maana.

Kupanda costa moja watu 152 sio hoja, inaweza kwenda na kurudi.

Ni ujinga kumwambia mleta mada kwanini asingeuliza pale pale. Sababu kualikwa kwako hakumaanisha ukakubali kila kitakachofanywa! Pili inaonekana kikao hakikuwa cha maswali na majibu.. Ni presentation tu. Tatu, sio kila swali unaweza kuuliza moja kwa moja kwenye hadhara, bila kuangalia pros and cons.. Inawezekana mleta mada amefikiria swali lake akaone sasa ndo wakati wa kuuliza, na kwakuwa hawapo tena kwenye mkutano, basi kwenye mitandao ya kijamii ndo mahala pake (ref. Mwigulu, Nape na wengine wapo humu), kwa kuwa Makamba ni muumini mzuri sana.

Zaidi ya hapo, si kila anayehudhuria mkutano ana lengo la kupiga makofi, wengine wapo kazini kujua mambo mbalimbali na kuuhabarisha uma kama hivi.

Alichofanya Makamba ni rushwa ya waziwazi..

HAIKUBALIKI!!
 
Back
Top Bottom