FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,819
Fundo lililozua utata baina yangu na somo yangu takriban miaka 40 iliyopita.
Ilikuwa katika matayarisho ya harusi yangu, shoga'ke kipenzi bibi yangu nae nilimwita bibi, alikuwa ananisiriba manjano mwilini, kunitayarisha bi harusi, huku ananifunda hili na lile.
Akanambia, basi mumeo "anapomaliza" atakuwa hoi, na wewe umpe "pole", tena pole isitokee mdomoni, itokee puani". Nikauliza, pole ya nini?
Jibu halikuja moja kwa moja bali lilianzisha mjadala mrefu baina yangu na somo yangu. Ingekuwa sijamzoea tusingekuwa na mjadala lakini kwa kuwa alikuwa ni mtu wa karibu sana na nikimuita bibi kwa kuamini kabisa naye pia ni bibi yangu, tulikuwa na utani wa ubibi na mjukuu uliopelekea kutohofia kuongea nae chochote, naona hilo ndilo likawa kigezo cha yeye kuwa somo yangu.
Toka siku hiyo na mjadala huo, somo yangu mpaka anakwenda mbele ya haki, kila tukikutana husema, pole, tukawa tumejenga msamiati wa siri ya utata wa malumbano kwa pole ya kutokea puani.
Kabla sijatoa majibu ya malumbano na utata na majibu niliyopewa nawauliza wanajamvi, mwanamke hutoa pole ya nini na mwanamme hupewa pole ya nini baada ya.
Funda nikufunde mwana.