mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
- Thread starter
- #21
Usikalili, wale kwa Sasa ni marafiki sio maadui, kumbuka Hana adui wala rafiki wa kudumu sera nzuri sana hii.
Lakini Iran imeshamshtukia marekani tayari!! Imesema vikwazo sawa nifungulieni lakini bado nitafanya biashara na Urusi!!!!! Hapo pia Marekani nduki!!!
Ila yule Rais Maduro wa Venezuela yeye bado hajaweka hadharani msimamo wake!!
Nitashangaa sana kama Maduro atawakubalia Marekani!! Huo utakuwa ni ujuha wa hali na usaliti wa hali ya juu dhidi ya Urusi!! Kumbuka bila Urusi Maduro angekuwa ameshaondolewa tayari, kama ilivyo kwa Rais Saad wa Syria!!
Hebu tangalie kwa pamoja: Venezuela ilikuwa na akaunti yake Marekani ambapo walikuwa wanaweka pesa zao za mauzo ya mafuta huko. Marekani ikaamua kutokumtambua Maduro kama Rais halali wa Venezuela, badala yake
Nchi takriban 14 duniani zimepeleka msaada wa silaha za kivita Ukraine, hata Marekani wenyewe wamepeleka matani kwa matani kabla ya vita na sasa vita inaendelea mbona huyo babako Putin hakurespond? Germany pekee wamepeleka Ant-tank 500 na Missles karibu 1000 zaidi, mindege ya kivita kibao Ukraine wamepewa unafkiri iyo vita iliyoko Ukraine ni ya kitoto?
Kwanini hujiulizi kama Russia anatisha kiasi hicho angechukua leo siku ya 14 Kiev bado yuko pembeni pembeni uko anajamba jamba, jana jenerali wao kapigwa chuma.,
Putini amepanik sasa ukimgusa anatishia nuclear mana mbinu zake zimegonga mwamba, alidhani siku 2 zitamtosha kuichukua Kiev
View attachment 2144264
Sijui una umri gani na sijui wakati wa vita ya ghuba ambapo mataifa karibuni yote ya magharibi (ukiondoa Ufaransa) yaliishambulia Iraq ya Sadam Hussein kwa kupitia kuwait. Kama unafahamu niambie walichukua siku ngapi miezi mingapi kumshinda Sadam Hussein? Kumbuka walikuwa nchi nyingi zenye nguvu zote huku zikiwa hazijawekewa vikwazo vyovyote lakini zilichukua miezi mingi sana kumwangusha kabisa Sadam Hussein. Sasa kama muungano wa NATO (isipokuwa Ufaransa) walichukuwa miezi lukuki kuishinda kabisa serkali ya Sadam Hussein na bado wakachukua miaka kadhaa wafuasi wa Sadam wakiwa bado wanawasumbua, unadhani ingewezekana kiuhalisia Urusi kushinda kwa siku mbili huku akiwa na vikwazo kila kona!!! Mwilize google marekani alifiwa na askari wangapi huko Iraq na alipoteza ndege ngapi? kisha njoo hapa utoe majibu!!