Poland imeshtuka kuingizwa mtegoni na Marekani Vita ya Urusi na Ukraine

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,651
18,021
Kulikuwa na suala la kupata ndege za kivita ili kupeleka Ukraine zikasaidie kupambana na Urusi. Nchi zote zikaingia baridi, halafu Marekani ikasema inafanya majadiliano na Poland ili ikubali kupeleka ndege zake Ukraine. Poland hakutaka kumkatisha tamaa Marekani, ila ikamwambia kuwa haiwezi kuzipeleka moja kwa moja Ukraine kutokea Poland isije ijikuta kwenye midomo ya Putin.

Ila Poland ikasema nitazipeleka hizo ndege na kuzikabidhi kwa Marekani kwenye kambi ya Marekani iliyoko Ujerumani TENA BILA GHARAMA! Halafu Marekani kama ina ubavu huo ndio izipeleke hizo ndege huko Ukraine!

Marekani kuona hivyo ikaruka kimanga!! Tuambizane ukweli, hakuna mwenye ubavu wa kujitumbukiza kwenye midomo ya Putin. Ikasema SIWEZI KUFANYA HIVYO!!

Sasa najiuliza, wakati Marekani inaiambia Poland (mwanachama wa NATO) kuwa ipeleke ndege zake Ukraine haikuwa inajua kuwa itaziingia nchi za NATO kwenye vita na Urusi? Ila kwa sasa Marekani ilipoambiwa yenyewe ndiyo izipeleke ndo inajua kuwa itaziingiza NATO vitani na Urusi??

Mchezo uko hivi: Putin aliipigia simu Poland kuitonya kuwa usijaribu kuleta ndege zako Ukraine, iambie Marekani kama ina ubavu izilete yenyewe!! Ona hapa!

A plan under which the US would transfer Polish-owned planes to Ukraine risks dragging NATO directly into a military conflict between Kiev and Moscow, the Pentagon said, as it seemingly rejected a deal earlier proposed by Warsaw.

On Tuesday, Poland announced that it was ready to deploy “immediately and free of charge” its fleet of MiG-29 jets to a NATO base in Germany and hand them over to the US military.

Marekani kwa suala hili imepata aibu sana!! Ni sawa na baba mtu aliposikia kuna sauti ya hatua za mtu akitembea kuzunguka nyumba yake usiku halafu akamtuma mtoto atoke nje kwenda kuangalia ni kitu gani. Mtoto akamjibu baba kuwa hawezi maana anaogopa, ila ataenda kufungua mlango ili baba mwenyewe atoke nje!!

Baba kuambiwa hivyo akasema, "mwanangu kutoka nje usiku ni hatari sana kwa maisha yetu wote hapa nyumbani". Sasa mtoto atabaki akijiuliza hii hatari ameijua saa ngapi? Wakati ananiambia mimi nitoke hakuwa anajua hatari hiyo?

Kumtegemea baba wa hivyo yatakukuta yaliyomkuta Rais Zelensky wa Ukraine, alivimbishwa kichwa kwa kuahidiwa kujiunga na NATO na kupewa vimsaada vya kijeshi ambavyo mpaka sasa vimeshasambaratishwa!
 
Marekani imeikatalia Poland kupeleka msaada wa ndegevita (MiG29 fighter jets) Ukraine kupitia base ya kijeshi ya Marekani iliyopo Ujerumani. Marekani imekataa ofa hiyo ya Poland kwa kuogopa Putin atashambulia nchi za NATO zitazohusika.

Kila mmoja aogopa kumfunga kengele Paka. Ingawa walijisemesha kuwa ati watapeleka msaada wa ndegevita

========

SmartSelect_20220309-092650_Chrome.jpg


Kumbukizi: Juzi kati Marekani ilipojisemesha kuwa nchi za NATO zinaruhusiwa kupeka ndegevita Ukraine

SmartSelect_20220309-095736_Chrome.jpg
 
Poland ninawapa big up.Halafu cha kushangaza US wamekataa Ombi la Poland la kupeleka ndege US ya Ujerumani. US anajidai mjanja. Kuna wajanja zaidi yake.
Zelensky kichwa maji, ameisambaratisha nchi yake kwa kutafuta sifa za kijinga.

Hata ikitokea Warusi wamerudi nyuma uharibifu uliyofanyika ni mkubwa mno.

Serikali yake itakuwa na jukumu la kujenga tena miundombinu iliyoharibika.

'Nchi imejidumaza'.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Zelensky kichwa maji, ameisambaratisha nchi yake kwa kutafuta sifa za kijinga.

Hata ikitokea Warusi wamerudi nyuma uharibifu uliyofanyika ni mkubwa mno...
Ulitaka aongoze nchi kwa kufuata maelekezo kutoka Moscow, kichwa maji ni Putin anayeharibu uchumi wa nchi yake huku akigharimu maisha ya Askari wake. Zelensky kavamiwa ulitaka asitetee nchi yake?!
 
Marekani imeikatalia Poland kupeleka msaada wa ndegevita (MiG29 fighter jets) Ukraine kupitia base ya kijeshi ya Marekani iliyopo Ujerumani. Marekani imekataa ofa hiyo ya Poland kwa kuogopa Putin atashambulia nchi za NATO zitazohusika...

Haya yalikuwa ni maneno ya Marekani kutaka kumwingiza choo cha kike Poland! Hapa Marekani anasema nchi za NATO zinaruhusiwa kupeleka ndege zake Ukraine.

Lakini Poland alivyoshtukia mtego huo akamwambia Marekani sawa, mimi nikuletee hizo ndege halafu wewe uzipeleke huko Ukraine!! Marekani kuona hivyo akala nduki!!!! Ila ni AIBU!! Hakuna tena nchi ya NATO itakayoiamini Marekani kivile!!

Utasukumiaje mzigo kwa mwenzako ambao wewe hauna u8bavu wa kuubeba?? Tusidanganyane, Putin anatisha!! Fikiria anapigana vita huku kafungwa mikono na miguu ya kiuchumi karibuni nyote!!!! Hakuna nchi inayoweza kuhimili hali hiyo!!!
 
Ukitaka aongoze nchi kwa kufuata maelekezo kutoka Moscow, kichwa maji ni Putin anayeharibu uchumi wa nchi yake huku akigharimu maisha ya Askari wake. Zelensky kavamiwa ulitaka asitetee nchi yake?!
Kuirudisha Ukraine ilivyokuwa awali itahitaji miaka 30-50 wakati Russia alijarushwa hata jiwe. Mwisho wa siku Russia atapiga hiyo nchi nzima na wataenda Moscow kupiga goti.
 
Kulikuwa na suala la kupata ndege za kivita ili kupeleka Ukraine zikasaidie kupambana na Marekani. Nchi zote zikaingia baridi, halafu Marekani ikasema inafanya majadilioano na Poland ili ikubali kupeleka ndege zake Ukraine....
Nchi takriban 14 duniani zimepeleka msaada wa silaha za kivita Ukraine, hata Marekani wenyewe wamepeleka matani kwa matani kabla ya vita na sasa vita inaendelea mbona huyo babako Putin hakurespond? Germany pekee wamepeleka Ant-tank 500 na Missles karibu 1000 zaidi, mindege ya kivita kibao Ukraine wamepewa unafkiri iyo vita iliyoko Ukraine ni ya kitoto?

Kwanini hujiulizi kama Russia anatisha kiasi hicho angechukua leo siku ya 14 Kiev bado yuko pembeni pembeni uko anajamba jamba, jana jenerali wao kapigwa chuma.

Putini amepanik sasa ukimgusa anatishia nuclear maana mbinu zake zimegonga mwamba, alidhani siku 2 zitamtosha kuichukua Kiev

PHOTO-2022-03-09-00-43-41.jpg
 
57 Reactions
Reply
Back
Top Bottom