Ilipoishia….
Nilichokifanya nilimfanyia yule mzee ishara ya
kumnyamazisha kwa kutumia kidole changu
kukiweka mdomoni, kisha nikamchukua
mwanangu Adriani hivyo hivyo akiwa analia
nakumtupia uvunguni mwa kitanda na baada ya
hapo nikaelekea moja kwa moja mpaka mlangoni tena kwa kujiamini huku nimejifunika khanga
nakuufungua mlangu nusu.
“eenhe unasemaje..?”
Uso wangu kwa sasa ukawa umekutana moja kwa
moja na Mmama ambaye sura yake si ngeni kabisa
machoni mwangu huku akibubujikwa na machozi yalioambatana na kwikwi na nilipomuuliza tu kuwa
anasemaje. Pale pale alinisukuma nakuingia mpaka
chumbani kwangu kwa nguvu…
'
Sasa endelea….
“...Hivi jamani nikupe nini ili uridhike mwanaume
wewe..? eti Baba Jose..? Kwanini unanifanyia mimi
hivi..? kitu gani hujaridhika kutoka kwangu..? kitu
gani sikupi mie..?”
Nilishusha pumzi chini huku macho yangu
nikiyatoa kwa tahamaki nikiendelea kumshuhudia yule Mama akilalama. Kumbe yule mzee niliokuwa
nafanya nae mapenzi alikuwa ni mume wake wa
ndoa. Na kwa sasa alikuwa kama kishamfumania
akiwa na mimi. Aliendelea kumlalamikia sana
mume wake huku akimshika shingoni vilivyo.
“..Lakini mama Jose..?” “..lakini nini..? hivi kweli baba Jose ndio mchezo
wako huo unaofanyaga..? lini utakuwa mume
wangu..? kama ni watoto tunao wanne, badala
tupange ni jinsi gani tutawatunza na kuwasomesha
we ndio kwanza unahangaika nakutangatanga na
visichana vidogo.. embu inuka twende nyumbani huko..?”
Bado yule Mama alionekana kuwa na hasira
iliyoambatana na kwikwi kali kwani kila muda
alikuwa akihema kwa shida huku akiishiwa pumzi
kwa hasira ambayo alikuwa nayo ya kumfumania
mume wake. Akiwa bado anagombana na mume wake mara mwanangu Adrian akaanza kulia pale
chini yao.
“..tobaa..!!!, na tena kumbe binti mwenyewe ana
mtoto mchanga..? wewe baba Jose nini unafanya
jamani..? twende..!!, twende..!!, twende nyumbani
nimesema..? Nilisogea mpaka karibu yao kiuwoga woga huku
nanyata mithili ya simba anaponyemelea kitoweo
nakumchukuwa mwananagu Adrian nakuanza
kumbembeleza huku nikiwaacha yule Mama na
mumewe wakiendelea kuvutana. Waliendelea
kuzozana tena kwa sauti ya juu nakusababisha watu waanze kuchungulia madirishanai huku
wakipiga kelele za uchochezi. Baada ya muda
kama wa dakika tano nzima za ugomvi na
kuvutana huku na kule ndipo wakaondoka zao
wakiniacha nikiendelea kumbembeleza
mwanangu Adrian ambaye kwa muda huu ni kama alikuwa akizidisha kulia.
Baada ya muda kama wa dakika kumi ndipo
mwanangu Adrian akaanza kunyamaza
nakunifanya nijisikie faraja tele moyoni. Tabasamu
aliokuwa akiendelea kulitoa ni wazi kuwa alikuwa
mtoto msikivu anapobembelezwa. Niliinua mkono wangu wa kulia nakuanza kumpapasa maeneo ya
shingoni, mpaka usoni mwake. Alinishtua sana
kwani mwili wake ulionekana wamoto sana.
Kamasi za majimaji zilizokuwa zinamtiririka kupitia
puani mwake ni wazi zilionesha kuwa anaumwa.
Nilimvua nguo zake haraka haraka nakuanza kumuogesha. Nikiwa bado namuogesha mara tena
nikasikia kama mtu anabisha hodi. Mwanzo
nilionesha kusita lakini kadri nilivyokuwa
naendelea kumuogesha mwanangu Adrian ndivyo
na yule mtu alizidi kupiga hodi. Nilimtoa kwenye
beseni lake la kuogea nakumuweka kitandani nakuelekea mlangoni kujua ni nani alikuwa
anapiga hodi.
“Mama Adrian..? Mambo..? Samahani unahitajika na
meneja yupo mapokezi..?”
“..sawa Salma.., mwambie nakuja sasa hivi..?”
Alikuwa ni rafiki yangu wa humu ndani ambaye nayeye ni mfanyakazi na yupo mapokezi na kwa
muda huu alikuwa amekuja kuniiita kuwa
nahitajika na meneja. Ile hali yangu ya uwoga
ilianza kunitawala tena, mwili wangu wote
uliishiwa nguvu nakujihisi kama ile hali ya
kutetemeka imenianza tena kwani safari hii nilikuwa natetemeka sana maeneo ya mdomoni na
nywele kunisisimka. Nilichokifanya nilivaa nguo
zangu haraka haraka na kisha kumchukuwa
mwanangu Adrian nakuelekea mpaka mapokezi
ambapo ndipo alipokuwa meneja akiniita.
“..naam bosi wangu nasikia unaniita..?” “..ndio nakuita, hivi mama Adrian kwanini unataka
kutuchafulia jina hapa mtaani..?”
“..kwani vipi meneja..?”
“ina maana hujui kitu ulichofanya muda si mrefu..?”
“..anhh..!!, unajua meneja ni kwamba..”
Kabla sijaanza kumsimulia meneja. Alinikatiza kuendelea kuongea neno lolote. Sura yake ilikuwa
imembadilika na hakuwa kama meneja yule wa
awali niliomzoea kwani alionekana dhahiri
kuchukizwa na kile kitendo cha mimi kufumaniwa
na yule Mzee.
“..sitaweza kuvumilia ujinga unaoendelea kufanya kila siku humu ndani. Katafute gesti nyingine za
kufanya huo ujinga hapa kuanzia sasa hatukuitaji
na mambo yako ibilisi we..?”
“..Jaribu kunisikiliza na mimi basi meneja..?”
“..hapana..?, hapana nimesema siwezi kukusikiliza
tena wala kukuelewa kwa namna yeyote zaidi ya kukuona umeenda huko chumbani nakutoa kila
kilicho chako na ufunguo wangu nauhitaji ndani
ya dakika kumi, umenisikia na kunielewa..??”
Nilikuwa sina tena ujanja Tina mimi kwani pamoja
nakumpigia magoti meneja huku nikitoa machozi
ya hapa na pale lakini haikusaidia chochote wala kunielewa. Inaonekana kile kitendo cha mimi
kufumaniwa kilimuuma sana nakuona kuwa
amechafuliwa jina na atakosa wateja. Sikuwa na
jinsi zaidi ya kuelekea tena chumbani nakukusanya
kila kilichokuwa changu. Sikuwa na begi
lakuwekea nguo hivyo nilichukuwa nguo zangu na za mwanangu Adrian kisha nikaziweka kwenye
fuko kubwa la lambo, na vitu vidogo vidogo kama
chupa ya maziwa na vijipodozi niliviweka kwenye
ule mkoba wa kipindi kile nilioondoka nao kutoka
kwa mama yake na huyu mtoto. Nilirudi mpaka
pale eneo la mapokezi nilipomuacha Meneja. “..funguo wenu huu hapa..?”
“…Nenda huko hatukuhitaji tena hapa Malaya
uliokubuhu wee..?”
Niliumia sana moyoni kwa maneno aliokuwa
akinitolea yule meneja nakujiona kuwa sifai na sina
hata haja ya kuishi hapa duniani. “..Adrian..? najua wewe huna hatia lakini sina jinsi
inabidi nikuhifadhi nakukulea mpaka
utakapokuwa kwa hali yeyote ile. Kubali vitu vyote
utakavyokutana navyo ukiwa na mimi mpaka
utakapokuwa mkubwa..?”
“Nilijikuta naongea na mwanangu Adrian japo alikuwa haelewi ninachokiongea kwakuwa bado
mchanga sana lakini alitoa tabasamu nakunifanya
nimbusu paji la usoni mwake nakuelekea kituo cha
dala dala huku nisielewe ninapoelekea.
“..nitaishi tu, Mungu ndio ajuaye..!”
Nilijikuta naongea peke yangu huku mwanangu Adrian nikimuweka vizuri kwani alikuwa
ameshalala. Ilinichukuwa zaidi ya dakika karibu
kumi nzima nikiwa nimezubaa peke yangu kituo
cha daladala huku nikifikiria nitaelekea wapi na
huyu mtoto. Akili yangu ikawa si ya Tina yule wa
zamani bali ni ya Tina mlezi tena yule wa mlezi wa katoto kachanga ‘Adrian. Hatimaye nikaingia
kwenye daladala iendayo mwananyamala na bado
nilikuwa sijielewielewi.
“…Sitakuacha na wala sintokuwa msaliti kwako
mwanangu Adrian..!!”
Bado niliongea peke yangu nilipoingia kwenye daladala. Baadhi ya abiria karibu wote ndani ya
daladala walikuwa wakinishangaa sana na
nadhani nikutokana na kuonesha sura ya huzuni
na kuchanganyikiwa kwa mawazo juu ya
mwanangu Adrian. Safari ya kutokea Temeke na
kuelekea Mwananyamala ilianza. Njia nzima nilikuwa mtu wa mawazo tu haswa ni jinsi gani
nitaishi huko niendako. Kuna wakati nilifikiria hata
kwenda pale chuo kwa rafiki yangu Aisha japo
anipe ushauri wa huyu mtoto na maisha yangu
kwa ujumla lakini nikaogopa kwanza kuchekwa
na pili mara ya mwisho nilipata uchizi nikiwa pale chuo hivyo kama wataniona na mtoto mdogo
watanishangaaa sana na kunicheka kwa dharau.
“ahh..!! liwalo na liwe bwana…!!, konda nishushe
hapo magomeni hospitali..?”
Nilijikuta naghairi kufika Mwananyamala ambapo
ndio mwisho wa daladala hii na ndio malengo yangu kwa ujumla japo sikujua naenda kwa nani.
Hivyo akili na mwawazo yangu ya ghafla
yakabadilisha mwelekeo mzima wa safari yangu.
Na kwa sasa nikashuka pale magomeni hospitali
na mizigo yangu kisha nikaelekea upande wa pili
nakupanda daladala ziendazo Posta kwa lengo la kushukia pale chuo cha biashara CBE ambapo
ndipo nilipokuwa nasoma chuo na rafiki yangu
kipenzi Aisha. Saa ya kwenye daladala ilikuwa jibu
tosha kuwa inaelekea saa kumi na moja ya jioni.
Haikunichukuwa muda sana kwani mwendo wa
kutoka Magomeni hospitali mpaka chuo cha biashara CBE ni kama dakika saba hivyo nilishuka
huku nambembeleza mwanangu Adrian
mgongoni.
“..twende mwanangu.., hapa ndipo nilipokuwa
nasoma..??”
Tayari akili yangu ilikuwa ni sawa na ya mwanangu Adrian kwani kuna kipindi nilikuwa nikiongea
naye utadhani kuwa ananielewa nakunisikia kwa
ninachokiongea. Mshipa wangu wa aibu niliuweka
pembeni kwa muda nakuvaa sura ya mbuzi tena
yule beberu kabisa. Nilijitwisha fuko langu la lambo
kichwani huku kwenye kwapa nikiuweka mkoba wangu vilivyo na mgongoni nikimbeba mwanangu
Adrian tena akiwa amepitiwa na usingizi.
“..embuuu…!! embuu…!!, hivi tulikuwa tunakaa nae
bweni lipi tena..?? ok..!! ok, nimeshakumbuka
ghorofa G namba 13..”
Chuo chote cha biashara CBE kilikuwa kimya sana na najua tu ikiwa hali kama hii ni dhahiri kuwa
wanafunzi wote wanakuwa katika mitihani tena ile
ya kumaliza chuo. Pale getini hakukuwa na mlinzi
yeyote hivyo niliingia bila ya kuulizwa na mtu
yeyote. Nilipishana na baadhi ya wanafunzi
wachache sana tena wale masista duu na wengine mabrazameni bila ya kujali wala kujiogopa
nilipishana nao huku akili yangu yote nikulifikia
jengo G namba 13.
“..samahani Anti.. eti namba 13 kuna watu…”
Nilimuuliza mdada mmoja alioonesha sura yake ni
ngeni kabisa machoni mwangu kwanza hata alikuwa hanifahamu kwani hakuonesha mshtuko
wowote..
“..kwani wewe unamtaka nani..? Maana wanafunzi
karibu wote wanafanya mitihani kasoro wale wa
mwaka wa kwanza walioingia juzi juzi ndio wapo
wapo humu mabwenini..” “..sawa..!!, unamfahamu Aisha.., anakaa chumba
hicho hapo juu namba 13..?”
“..Aisha..? Aisha..??, mhhh..!! Namfahamu wewe ni
nani yake labda..?”
“..rafiki yake wakaribu na nimesoma naye hapa
hapa chuoni..” “””haloooo…!!! Eti rafiki yake wa karibu nimesoma
naye..??, unahadhi wewe yakutembea na Aisha..?
mwenye hipsi.., shepu shepu sio la mchina..
wakutembea na ‘Verosa’ sio daladala, bajaji wala
teksi..?
Alinitolea maneno ya umbea na yakuumiza sana roho tena kwa pozi huku mdomo akiyumbisha
kana kwamba sina hadhi yakuongea naye yeye
wala huyo Aisha.
“..subiri hapo hapo nikakuangalizie maana nahisi
utakuwa umekosea njia kwani Aisha nimjuaye
mimi hawezi kuwa na mtu kama wewe ambaye hujui hata kujipodoa wala kuoga, mwenye kunuka
makwapa na hilo toto sijui ndio kojo au lijimavi
limeshajinyea..?”
Aliondoka huku akiendelea kuongea maneno
yake machafu na kwenda kumuita Aisha. Niliumia
sana moyoni nakutamani hata kumrukia na kumpiga lakini niiliogopa kufanya vurugu yeyote
katika maeneo ya hapa chuoni. Kwani niliamini
nitakamatwa na tena ikijulikana nilikuwa nasoma
hapa ndio nitaharibu kila kitu.hivyo nikawa mpole
tena mjinga haswaa huku nimejibanza
nakumsubiri huyo alieenda kumuita Aisha. Ilinichukuwa dakika kama nne nzima peke yangu.
Harufu kali ya marashi ya ‘adorable’ ilioambatana
na sauti ya viatu ndio ilinifanya nianze kutoa
mchozi kwani ndio marashi niliokuwa nayapenda
kutumia na rafiki yangu kipenzi Aisha tulipokuwa
wote chuo kipindi kile. “..Aishaaaaa..?? Aisha rafiki yangu..?”
Nilishusha fuko langu chini nakumkimbilia aisha
huku nikitaka kumkumbatia lakini nilipofika karibu
yake tu akanikwepa nakunifyonza huku macho
akiyatoa vilivyo.
“..wee chizi vipi..?” “..jamani Aisha embu niangalie vizuri..?
umeshanikumbuka rafiki yangu kipenzi..?”
“..sauti siyo ngeni.., embu nikumbushe unatokea
wapi wewe..?”
Maskini Aisha alikuwa ameshanisahau kabisa japo
mimi nilishamtambua. Kuharibika kwangu sura na nyele zangu za kipindi kile vilitosha kunibadilisha
nakuwa Tina feki. Hata nilipomwambia Aisha kuwa
naitwa Christina ama Tina bado alikataa nakusema
kuwa Tina yule wazamani alishakuwaga chizi wa
mitaani na siwezi kuwa mimi. Nilitumia dakika
kama kumi nzima za kumulelewesha hadi akanitambua.
“..niwewe Tina..? hata bado siamini kipenzi changu
kwanini umekuwa hivyo jamani..??, shetani gani
aliokutembelea Tina ukabadilika kiasi kile..?? Ona
sasa mwenzako nimetoka kumalizia mtihani wa
mwisho.., si tungekuwa tumemaliza wote sasa hivi Tina..?”
Aisha aliongea na mimi kwa uchungu wa hali ya
juu huku akitaoa machozi kama vile mtoto mdogo.
Alinitoa mule chuoni ndani nakunipeleka mpaka
nje. Tukatafuta sehemu nzuri ya baa nakukaa kisha
nikaanza kumsimulia yote yalionikuta kipindi sipo naye. Aliona na kufananisha maisha yangu kama
vile sinema tena ile ya tamthiliya ambayo ya muda
mrefu sana. Nilimuelezea kuanzia tulipoanza naye
mpaka nilipomucha chuo nakuanza kufanya
umalaya wangu tena kwa kumficha mambo mengi.
Kuhusu kuathirika kwangu nilimficha lakini kuhusu huyu mtoto nilimdanganya kuwa ni mtoto
wangu ambaye nilizaa na mchungaji yupo Mwanza
kaniacha na kunitelekeza na mtoto.
“..pole sana rafiki yangu Tina, ndio maisha jinsi
yalivyo. Enhee kwa hiyo unaishi wapi kwa sasa..?”
“Aisha..? hapa unaponiona sina mbele wala nyuma na naishi peke yangu na huyu mtoto wangu tena
kwa kutangatanga..”
Tukiwa bado tunaongea mara mwanangu Adrian
akashtuka kutoka usingizini nakuanza kulia kwa
sauti ya juu. Nilimfunua vizuri nakuanza
kumbembeleza huku nikimtolea maziwa kwenye chupa..
“..mtoto wako mzuri sana Tina.., anaitwa nani..?”
“..anaitwa Adrian. Kwa hiyo sasa hivi Aisha
umeolewa au maana nakuona na pete ya uchumba
shosti..?”
Nilimbadilishia mada asiendelee kuniuliza juu ya huyu mtoto. Alikuwa amevalishwa pete lakini
hakuniweka wazi kuhusu bwana anayeishi naye
ila aliniambia tu ni mfanyabiashara tena
wakimataifa hivyo si mtu wakukaa sana nayeye
hivyo ni kama anaishi yeye na mfanyakazi tu.
Alinichukuwa pale nakuelekea mpaka eneo aliokuwa amepaki gari lake na safari ya kuelekea
kwake ikaanza kwani aliniahidi kuishi na mie
mpaka mtoto atakapokuwa mkubwa ama mimi
nitakapopata kazi yakueleweka nakujitegemea
mwenyewe.
“..Aisha..?, wewe ni rafiki wangu wa milele.., na sina rafiki kama wewe..?”
Niliongea kwa kusisimka huku uso wangu
ukitawaliwa kwa machozi ya furaha. Gari lake
lilikuwa zuri sana na lenye vioo vyeusi vya
kumfanya mtu wanje asiweze kuwaona.
Mwanangu Adrian nilikuwa nimeshamshusha mgongoni nakumlaza siti ya pembeni yangu. Muda
wote Aisha alikuwa akitabasamu nakucheka na
mimi karibu njia nzima na hata tulipofika kwenye
foleni alikuwa akinipigisha stori za chuo
nilivyoacha gumzo kwa kila anayenijua na hata
kitendo cha wazazi wangu kuja kunitafuta chuoni. Kifupi nilifarijika sana nakujiona mtu mwenye
bahati ya mara nyingine tena bahati ya mtende.
“..kumbe Aisha unaishi mbali hiivi…??, enhee..!! ni
wapi hivi shosti maana hiyo safari hatufiki tu..”
“..weee unafikiri mbali basi..?? ni hapo bunju tu..,
tukivuka aka kapori tu tumeshafika..” Gari ilitembea kama alivyoniahidi kuwa tukivuka tu
kapori tumeshafika. Giza nalo lilikuwa
limeshatanda. Nilihakikisha mwanagu Adriani
nimemfunika vizuri kwa ajili ya baridi ya mule ndani
ya gari. Tukiwa bado tupo eneo la kale kapori mara
Aisha akasimamisha gari kisha akaanza kufungua droo za mbele ya gari yake kana kwamba kuna
kitu amekisahau au anakitafuta amekikumbuka.
Ghafla akatoa bastola ndogo nakunielekezea
kichwani mwangu..
“..hapo hapo ulipo Tina..??, usitingishike wala
kuongea chochote na nitakufyatua usipotii amri hii..??”
Mapigo yangu ya moyo yakabadilika nakuanza
kutemeka huku kojo likichukuwa nafasi yake
kunitiririka. Nikawa siamini kwa kilichonitokea.
Nilibaki kimya kama alivyoniambia Aisha huku ile
bastola iking’ang’ana katika paji langu la uso vilivyo tayari kwa kufyatuka. Sikuweza kujipindua
zaidi ya kusikia tu Aisha akiongea na mtu kwenye
simu.
“..kazi yenu tayari haya sasa mko wapi mnipe
changu..?”
Aisha aliongea kwenye simu kwa sauti ya ukali na yakikatili kisha ndani ya dakika chache mlango wa
gari kwa upande wangu ukafunguliwa. Tochi
zilinimulika kisha nikashikwa na watu
nisiowafahamu halafu kwenye gari nikamshuhudia
Jerry kiingia kisha akambeba yule mtoto na
kuondoka zao na Aisha huku wakiniacha nimekumbatiwa na watu nisiowafahamu.
“..mnampeleka wapi mwanangu..??,
mrudisheni..??”
Nilitoa makelele ya nguvu lakini haikusaidia
chochote zaidi ya ile gari kutokomea huku wale
wavulana waliokuwa wamenishika kwa kunikumbatia wakianza kunivua nguo zangu na
zao tayari kwa kunibaka kwa zamu…
*********************** ***
kila siku stori inazidi kunoga je Tina atalipizaje
kisasi kwa Aisha..?
***
Inamaana Jerry alishampanga Aisha kuwa
kama Tina atatokea chuoni basi wamchukue mtoto
halafu watalipana pesa..?? nini hatma ya Tina..?
*******
hii ndio play gal (Revenge).., usithubutu
kuhadithiwa hata inayofuata kwani ni kali sana
zaidi ya hapa.
***
endelea kuwa nami kwa msisimko zaidi wa
hadithi hii yenye ukweli ndani yake ya play gal