Pita hapa kama unataka kujua chochote kuhusu biashara Kampala

Mkuu hiyo isikupe tabu, tafuta parking ya basi la Friends ama Taqwa ya Kampala. makondakta watakupa details zote,mie niko mbali kidogo kwa hizi siku brother
Wadau ebu fungukeni basi kama kutoa mzigo Kampala mfano nguo na viatu kama inalipa mimi nifanye mambo wakuu
 
Habari mkuu, nilipata taaria kuwa huko uganda kuna biashara sana ya SAMAKI hasa wale wa IRINGA waliopasuliwa katikati na kukaushwa kwa moshi. Kama utakuwa na taarifa zaidi naomba kujuzwa mkuu
 
Ni mwenyeji sana huko hasa katika biashara hiyo kabla sijazamia mtoni. Nilikuwa nalala Bukoba mjini, then asubuhi naondoka na Bus la Friends, saa 7 mchana tuko Kampala na brocken english yangu, muda huo unafanya window shopping harafu asubuhi unaaza kununua au mchana huo. Ukiwahi kesho unaondoka na Friends ya saa sita mchana unalala tena Bukoba then asubuhi tu saa tano uko Geita. Nilikuwa nalala Samarini kama unapafahamu. Biashara ya nguo haina stress kama vipodozi ambavyo TFDA wamekuwa na bifu navyo.
Mkuu, kwa mm ambae ni mhitimu wa chuo na muhanga wa ajira inanipasa niwe na mtaji wa sh ngapi niweze kuanza biashara hiyo kwani biashara ipo damuni.
 
Kwa anayefahamu dealers wa pikipiki za mtumba aina ya Honda Uganda anijuze tafadhali nasikia huko bei ziko powa kuliko kwa wahindi wa kariakoo
 
Hii thread ina madini sana. Siku zote nilikuwa natamani kwenda Kampala kuchungulia fursa, lakini thread hii imenipa nguvu zaidi. Next month lazima nifike Kampala.
 
Samaki mkuu, nataka kufanya kitu cha utofauti kidogo

Ntafungukaje zaidi ya hapo wakati hata mm nataka wadau wanielekeze maa a nilisikia juu juu tu
Samaki kaka sikushauri hata kidogo maana Waganda wanapata samaki wengi kupitia ufugaji (samaki aina ya sato au tilapia Uganda unapata kwa bei cheap harafu samaki wa ukweli. Nasema haya kwa kujiamini maana naona wanavyouzwa kwa wingi na bei ya chini hata ukiwa kwenye hotel kubwa Kampala, samaki mzima na aliyetulia utampata kwa sh, 5000/= akiwa tayari ameandaliwa.
 
Back
Top Bottom