Pita hapa kama unataka kujua chochote kuhusu biashara Kampala

las Casas

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
575
711
Wakuu natarajia kuwa na safari ya Kampala mwanzoni mwa mwezi wa kumi na mbili . Lengo la safari hii ni kuangalia mazingira ya biashara kwa ujumla ikijumuisha gharama za vitu, usafiri, accommodation pamoja ushuru na taratibu za border. Ni muda mrefu sijaenda huko. Kama utakuwa unataka kujua lolote karibu.[HASHTAG]#Mrmitumba[/HASHTAG]
 
Safari hii ni ya kuangalia mazingira tu, niko Bukoba kwa hiyo kufanya safari nyingne itakuwa muda wowote. Kikubwa ni mtumba pamoja na nguo za special
 
Huko naskia ni balaa... Eti dar haikamati hata kidogo kwenye biashara..kuna mtu nilikua namshangaa anatoka dar kwenda kuchkua mzigo kampala...yeye ndo akanishangaa zaid..ipo cku ntaenda kujionea... Naskia hawana mabidhaa feki kama bongo..halafu fashion mpya znaanzia kule eti
 
Safari hii ni ya kuangalia mazingira tu, niko Bukoba kwa hiyo kufanya safari nyingne itakuwa muda wowote. Kikubwa ni mtumba pamoja na nguo za special
Unapeleka au unanunua huko kuleta Bukoba? Kama unafuata huko wala usisubiri, nenda tu bei ni nafuu sana. Miezi miwili imepita nilipata safari ya kuja Tz kuangalia familia yangu na kibiashara changu then nikaenda Kampala kununua nguo, tatizo kwa sasa kuna ushuru wa kukomoana kwa TRA. Unalipia Mtukula na TRA Kyaka zote nchi moja.
cc05e1556fb00b966297dc90747a2d06.jpg
. Pia hapo Bukoba kuna wafanyabiashara wengi sana wananunua nguo Kampala lakini wengi wanakuja kuuza kwa jumla soko la Mtukula
 
Asante mkuu

Sent from my TECNO P6 using JamiiForums mobile app
Ni mwenyeji sana huko hasa katika biashara hiyo kabla sijazamia mtoni. Nilikuwa nalala Bukoba mjini, then asubuhi naondoka na Bus la Friends, saa 7 mchana tuko Kampala na brocken english yangu, muda huo unafanya window shopping harafu asubuhi unaaza kununua au mchana huo. Ukiwahi kesho unaondoka na Friends ya saa sita mchana unalala tena Bukoba then asubuhi tu saa tano uko Geita. Nilikuwa nalala Samarini kama unapafahamu. Biashara ya nguo haina stress kama vipodozi ambavyo TFDA wamekuwa na bifu navyo.
 
Kingine hiyo biashara uchanganye nguo za kike na kiume, za kike ziwe nyingi kuliko za wanaume ambao si wavaaji kama wanawake pia wakopaji wazuri. Usisahau kununua chupi za kisasa hasa cotton, soma mazigira unayouzia kama kuna wadada wanapenda nguo za kimamtoni then waletee hizo. Ngoja nikipata muda takutumia business card za maduka ya nguo Kampala.
 
Vipi kuhusu ushuru mkuu maana mimi ni muda sana na Mara ya mwisho nakumbuka sikuwa na mzigo mkubwa so sikulipa

Sent from my TECNO P6 using JamiiForums mobile app
Ushuru hapo wakiamua kukukomoa unaweza omba mgawane mzigo ili wakuachie, wana roho mbaya kama nini washenzi wale. Kabla hujaanza tafuta mfanyakazi wa TRA hapo border ongea nae kiutu uzima (sijui umenielewa?) kama ni mtaji mdogo nunua mabegi madogo madogo hivyo nguo zikunje vizuri na kuziweka kwenye hizo begi, then kataa kuweka kwenye buti la basi isipokuwa ingia nazo ndani ya basi kwa mchongo na kondakta mkiwa Kampala usiku wa kuamkia safari. Utapita border ukila ndizi tu za kuchoma kwa raha zako lkn kama ni mzigo mkubwa fanya hiyo ya kumuona mtu wa TRA tofauti na hivyo hutarudi tena Kampala.
 
Dah Asante mkuu ila umenitisha aisee dah yaani nimeanza kuogopa, sijajua gharama za robota wanabana ngapi? Nataka nifanye juu chini nijue isije ikawa shida

Sent from my TECNO P6 using JamiiForums mobile app
 
Kingine hiyo biashara uchanganye nguo za kike na kiume, za kike ziwe nyingi kuliko za wanaume ambao si wavaaji kama wanawake pia wakopaji wazuri. Usisahau kununua chupi za kisasa hasa cotton, soma mazigira unayouzia kama kuna wadada wanapenda nguo za kimamtoni then waletee hizo. Ngoja nikipata muda takutumia business card za maduka ya nguo Kampala.
Mkuu Asante Sana umekuwa mtu muhimu sana hapa kwa members kijifunza kitu, itakuwa vizuri kama utatuwekea majina ya maduka ya jumla huko Kampala ili tukienda tusihangaike sana
 
Back
Top Bottom