Bourgeoisie
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 656
- 162
Nafikiri ni Kukubali yaishe!!Badala ya kusubiri jibu la Tendwa ambalo ni multiple choice yenye option moja bora tujiulize what is Chadema's next step.
Nafikiri ni Kukubali yaishe!!Badala ya kusubiri jibu la Tendwa ambalo ni multiple choice yenye option moja bora tujiulize what is Chadema's next step.
Ni tabia ya uoga...na kuto kuelewa.....Inabidi kusupport upande fulani ili uwe member hapa? Na sisi tusiofungamana na upande wowote inakuwaje?
Kwa walio Jijini Dar es salaam, Msajili wa vyama vya siasa Ndg, J. Tendwa alitegemewa kuzungumza na vyombo vya Habari leo kutoa maamuzi juu ya Pingamizi la CHADEMA dhidi ya JK wa CCM, je maamuzi yashatoka, tunaomba mwenye updates atujuze
Yaani wewe post ya kwanza unaanza na kuomba updates kuna mtu humu ulimtuma be serious mpigie simu Tendwa atakuwa nazo
Ringmaster
Join Date Mon Sep 2010
Posts 1
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power 0
Either you are with us (indigenous) or with them mafisadi.
walisema NEC ndiyo inatoa pingamizi lakini Tendwa ndiye anapaswa kushauri kutokana na maelezo ya wahusika na pia atatoa copy ya ushauri wake kwa vyama husika
Cha msingi, Tendwa hana maamuzi. Akikubali pingamizi tu ni kwamba kazi hana kwa hiyo tusitegemee jipya sana. Pia Kungekua na TUME huru, Msajili huru hapo sawa. Kami ni msajili wa vyama, kwa nini ateuliwe na chama kimoja tu ili hali kuna vyama vingi? CCM wangejua hii sheria ingekua hivi basi, wangeisubirisha hii sheria waliipitisha fasta sana.
Source: JIACHIE
sina taarifa yoyote ya kutoa kuhusiana na pingamizi la chadema dhidi ya mgombea urais wa ccm-tendwa
Monday, September 6, 2010
Msajili wa vyama vya siasa nchini,John Tendwa amesema leo hana taarifa yoyote ya kutoa kuhusiana na pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa aliahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi bila kuhusisha Bunge kitu ambacho kinaenda kinyume na sheria ya Fedha za Uchaguzi.
Bw. John Tendwa alikuwa ameahidi kutoa taarifa baada ya siku tano, hata hivyo leo waandishi wa habari walipokwenda ofisini kwake kwa ajili kutaka kujua hatma ya suala hilo, alisema kuwa leo ana mkutano mwingine, na kuhusu pingamizi la CHADEMA tayari ameshavijibu vyama na pia taarifa ipo Tume ya Uchaguzi ya Taifa . Hivyo akashauri Waandishi hao waende kwa vyama husika na kuwauliza, aidha akaongeza kuwa vyama hivyo pia bado vitalazimika kuwa na muda wa kutosha kupitia kwa kina majibu hayo.