Jaji Mutungi: Baraza Maalumu la Vyama vya siasa linakutana kujadili Lugha za kutumia kwenye Siasa kwa kufuata sheria!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Msajili wa Vyama vya Siasa amesema Baraza Maalumu la Vyama vya Siasa linalokutana kwa Siku 3 halina lengo la kunyoosheana vidole wala kutumbuana macho

Bali ni mkutano utakaojadili Lugha zinazopaswa kutumika kwenye Siasa kwa kufuata sheria

" Wala Hatuko hapa kujadili na kulumbana ni vyama vingapi vinawatumia Viongozi wa Dini, la hasha" amesisitiza mh Jaji Mutungi.

---
Hayo yamebainishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi,
leo Jumanne ya Agosti 1, 2023, katika ufunguzi wa mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Jaji Mutungi amesema wito wa mkutano huo maalum, haulengi matumbano na vyama vya siasa bali ni kuelimishana.

Kauli yake hiyo inatokana na kile alichoeleza kuwa, wapo wanaodhani wito wake kwa wadau wa siasa ulilenga kutupiana maneno na kuvituhumu vyama fulani vya siasa, ilhali si hivyo.

Kikao cha baraza hilo, kimeitishwa siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuratibu mkutano uliohusisha viongozi wa dini.

Mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Bulyaga Temeke jijini hapa, ulilenga kujadili mambpo yanayohusiana mkataba wa uwekezaji, uboreshaji na uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam, kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kupitia DP World.

Kutokana na kuhusishwa kwa viongozi wa dini, Jaji Mutungi aliiandikia Chadema kuisihi isitishe mkutano huo, huku akiwaita viongozi wake, lakini waligoma kufanya vyote.

Baada ya hayo, Jaji Mutungi aliwahi kuiambia Mwananchi Digital kwamba, kutotekelezwa kwa barua yake, kunaonyesha haja ya kutoa elimu kwa wadau wote wa siasa.

"Naomba niwaondoe hofu kwamba tumekuja hapa sio kurumbana kwamba kuna vyama vingapi vya siasa vinatumia viongozi wa dini, bali tumekuja hapa kuelimishana namna tunavyotakiwa kufanya siasa zetu," amesema.

Jaji Mutungi amesisitiza mkutano huo unalenga kufanya tafakuri ya lugha zinazopaswa kutumiwa katika siasa hasa kufuata sheria.

Msajili huyo kupitia baraza hilo, anatamani kuwepo taratibu zitakazofanya siasa zifanyike bila kulifikisha taifa kwenye mipasuko.

Source: Mwananchi
 
Katoro mafuriko ya Sisimizi....tuongee ki YUNANI au Kichina.....kama nongwa basi Latin
 
Mbona wakati Magufuli ananajisi uchaguzi wa nchi hakuitisha kikao kuongelea wizi ule?
 
Back
Top Bottom