CHADEMA hawawezi kumuelewa Paskali Mayalla. Ruzuku kwao ni baishara kuendesha maisha yao

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Akizungumza kwenye kongamano la kujadili Muswada wa Sheria ya Uchaguzi linaloendelea Jijini Dar es Salaam, Pascal Mayalla amesema;

“Ndugu zangu wa vyama vya siasa, wenzetu nchi za Ulaya utumishi wea chama ni wa kujitolea, chama sio ajira, vyama vya siasa tangu TANU havikuwa vinapewa ruzuku, vilikuwa 'funded' na wapenzi na wanachama, ifikie muda tuingie imani na Watanzania na umaskini wetu, kwanini tuendelee kuvipa vyama vya siasa ruzuku?”

“Jana Zitto nimemsikia anadai ruzuku, kama kweli ni kiongozi wa chama na unakipenda chama kwa moyo wako jitolee, uwe na shughuli nyingine ya kuendesha maisha yako utumishi wa chama uwe wa ziadi, sio fedha za Watanzania kwenda kugharamia vyama vya siasa," - Pascal Mayalla

IMG_9527.jpg
 
Ruzuku ikiondolewa wapinzani watapambana kweli waingie madarakani.
Kutakuwa na upinzani wa kweli hakuna mambo ya kwenda kunywa juice Ikulu na kisha picha picha kibao ukumbusho wa agano la kulambishana asali.

Hakutakuwa na utitiri wa vyama vya upinzani vinavyo hujumiana kwenye chaguzi na kuinufaisha CCM.

Wakiondoa ruzuku waruhusu vyama kupokea michango toka kwa diaspora n.k. Kusiwe na zengwe kama walilopigwa NGO kupokea ufadhili kipindi cha 2020. Vyama vitaungana kuunganisha nguvu.

Miradi ya vyama vya upinzani isipigwe vikwazo pia kodi iondolewe kwenye hiyo miradi.
Mgombea binafsi aruhusiwe.
 
Katika hili Zito hawezi kukubaliana na Mayalla kamwe. Zito alikuwa anajilia hela za matajiri wa kipemba kupitia mgongo wa maalim Seifu.

Sasa maalim Seifu hayupo, Zito anaanza kuhaha kutafuta sehemu ya kupatia pesa kienyeji kwa mgongo wa siasa zake uchwara.
 
Pamoja na kupora miradi na uwekezaji kadhaa wa Umma. Pamoja na kutumia magari na fedha za serikali kuendeshea siasa za chama chao, bado CCM kila mwezi inachukua mabilioni ya fedha toka hazina kama ruzuku na kufuja fedha hizo.
Ruzuku ikiondelewa itaokoa pesa nyingi za umma. Hizi pesa zinaweza kuelekezwa kwenye vitu muhimu kama BIMA kwa wote, elimu, afya, miundombinu, ruzuku kwenye pembejeo za kilimo, kukamilisha miradi ya kimkakati.
 
Akizungumza kwenye kongamano la kujadili Muswada wa Sheria ya Uchaguzi linaloendelea Jijini Dar es Salaam, Pascal Mayalla amesema;

“Ndugu zangu wa vyama vya siasa, wenzetu nchi za Ulaya utumishi wea chama ni wa kujitolea, chama sio ajira, vyama vya siasa tangu TANU havikuwa vinapewa ruzuku, vilikuwa 'funded' na wapenzi na wanachama, ifikie muda tuingie imani na Watanzania na umaskini wetu, kwanini tuendelee kuvipa vyama vya siasa ruzuku?”

“Jana Zitto nimemsikia anadai ruzuku, kama kweli ni kiongozi wa chama na unakipenda chama kwa moyo wako jitolee, uwe na shughuli nyingine ya kuendesha maisha yako utumishi wa chama uwe wa ziadi, sio fedha za Watanzania kwenda kugharamia vyama vya siasa," - Pascal Mayalla

View attachment 2861719
Mkuu Idugunde , asante kwa bandiko hili CHADEMA hawawezi kumuelewa Paskali Mayalla. Ruzuku kwao ni baishara kuendesha maisha yao

Hii hoja imejadiliwa pia hapa na Mkuu Sildenafil Citrate , Pascal Mayalla: Vyama vya siasa visipewe ruzuku, viongozi wake wajitolee

Wanasiasa, mtanielewa tuu in due time, kwasababu hili sikuanza nalo leo Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi

Paskali
 
Back
Top Bottom