Elections 2010 Pingamizi la CHADEMA latupwa

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Kwa walio Jijini Dar es salaam, Msajili wa vyama vya siasa Ndg, J. Tendwa alitegemewa kuzungumza na vyombo vya Habari leo kutoa maamuzi juu ya Pingamizi la CHADEMA dhidi ya JK wa CCM, je maamuzi yashatoka, tunaomba mwenye updates atujuze
 
Nadhani unataka update ya sababu ya pingamizi kutupwa kwa sababu unajua fika kuwa hilo pingamizi litatupwa; kama sio limeshatupwa. Do you still live with that wishful thought kwamba mgombea urais kupitia CCM ata....
 
Amesema atapeleka uamuzi wake kwa Tume ya Uchaguzi.
Wadakuzi wanapaswa kupiga kambi NEC maana nimjuavyo Tendwa akishavurunda hawezi kuwa news source hata kidogo.
Ila nitamshangaa akiusoma uamuzi huo hadharani maana atakuwa amekiuka sheria
 
Naona saa sita ishafika. Hakuna mwenye update ya yanayoendelea kwa msajili kuhusu pingamizi la CHADEMA...
 

Wadau, leo ndiyo leo, ile hukumu inayosubiriwa ndiyo inatoka. Ingawa wengi hawana imani kwamba Msajili huyo ataamua kitu cha kuwaudhi waajiri wake -- lakini ni bora tukajua hukumu inakaaje.

Wenye kufuatilia please, tuwekeeni hapa.
 
Pale hakuna jipya, pingamizi litatupwa na ambaye hakuridhika ataambiwa aende mahakamani!! Nilipopata habari kuwa Chadema wamewailisha pingamizi kwa JK, nilijiuliza mara mbili, je ni hapa hapa Tanzania au mwamuzi atatoka nje ya Tanzania. There is no fair politics in Tanzania, given the fact that the appointees of crucial authoritative positions are held by the persons appointed by the president of the rulling party!! Hapo itakuwa tofauti kama pengine ingekuwa ni nchi za wenzetu. Poor chadema!! Yaani hata kama makosa yangekuwa yanang'aa kama almasi lakini hayataonekana!! But the vice versa is the case!
 
Amelitupilia mbali pingamizi hilo kutokana na............,
Subiri kidogo ntarudi kumalizia
 
Nadhani unataka update ya sababu ya pingamizi kutupwa kwa sababu unajua fika kuwa hilo pingamizi litatupwa; kama sio limeshatupwa. Do you still live with that wishful thought kwamba mgombea urais kupitia CCM ata....
hata likitupwa lazima atoe sababu za kufanya hivyo, ndicho tunachosubiri.
 
Sipati picha pingamizi lisipotupwa.
Maana kila mtu ametabiri kuwa litatupwa.
 
Ni akili ndogo sana ya kufikiria,unaweza kutoa hukumu ya kifo kwa baba yako?hata kama ni mimi siwezi kumhukumu JK kwa njia hiyo,nitasukuma hili shauri kwa wengine kama mahakamani au bungeni mwaka ujao,au nisingizie mapungufu ya sheria yenyewe,ili mradi ipite mbali na mimi,hiki ni kitanzi cha Hon Tendwa na inabidi atii aliyemweka hapo.
 
Hakuna mwenye akili timamu narudia tena timamu anayeishi Tanzania anategemea pingamizi litapita, asiye tu na akili timamu ndiye anategemea lipite.

Baada ya kusema hivyo, Chadema inachotaka ni kuonyesha uwezo wa Msajili na NEC kama huwa inafanya maamuzi sahihi bila kuingiliwa na mwajiri wake, kingine Chadema inachotaka ni kupata majibu ya kwanini pingamizi lao limetupwa ili liyatumie hayo majibu kufungua kesi mahakamani na kupeleka kesi kwa wananchi. Nakumbuka hata Mnyika aliliweka hili wazi siku ya kupeleka pingamizi.
 
Hivi huyu msajili alishirikshwa katika kuiandaa sheria ile ya matumizi ya kampeni?
 
Ni akili ndogo sana ya kufikiria,unaweza kutoa hukumu ya kifo kwa baba yako?hata kama ni mimi siwezi kumhukumu JK kwa njia hiyo,nitasukuma hili shauri kwa wengine kama mahakamani au bungeni mwaka ujao,au nisingizie mapungufu ya sheria yenyewe,ili mradi ipite mbali na mimi,hiki ni kitanzi cha Hon Tendwa na inabidi atii aliyemweka hapo.

Hatutegemei haki itendeke. Hata Chadema wenyewe sidhani wanategemea pingamizi kupita. La hasha. Nia ya Chadema ni kuwavua nguo kina Tendwa na Judge Makame. Hawa ni makada wa CCM. Tangu lini nyani akaamua kesi ya ngedere?
 
Bado tu? Watuambie fedha za kulipa wafanyakazi zilipitishwa na kikao kipi cha Bunge, hilo tu!
 
Masikini Tendwa na Makame.

Wako kati ya Nyundo na fuawe. Sijui watakwenda wapi..........

Hapa CHADEMA wamewapata kwelikweli.........
 
Bado tu? Watuambie fedha za kulipa wafanyakazi zilipitishwa na kikao kipi cha Bunge, hilo tu!

Hakuna mahali palipoandikwa jinsi wafanyakazi watakavyolipwa,hakuna hansard yoyote bungeni inayotamka mishahara ya wafanyakazi,kwa hiyo hakuna ushahidi wowote endapo mishahara haitaongezwa,changa la macho kama la mahakama ya kadhi,kwahiyo ahakuna sababu yoyote ya kutetea rushwa ya mishahara ya wafanyakazi,wataalam na wasomi wote wanasema hiyo ni test capability ya Hon Tendwa.Namuonea huruma sana,kwasababu ni mtu wa watu na ni mchapa kazi mzuri sana kutoa uamuzi kwake utakuwa ni kumtundika kitanzi shingoni. asilaani hawezi hata kidogo kumpiga chini tajiri yake.
 
Back
Top Bottom