Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

HTML:
Alichokosea Pinda ni kujifanya naye amekasirika kwa barua ile ya Jairo. Haya mambo hayajaanza leo serikalini na wala hayafanyiki hapo nishati tu. Hili ambao tumewahi kuwa watumishi kwenye taasisi za UMMA tunalijua na Pinda analijua zaidi.

Hili halina ubishi hata kidogo, na binafsi jambo halina tofauti sana na yale mengine kama Richmond, Epa n.k na ndiyo maana nasisitiza kwamba Serikali inawahonga wabunge ili bajeti zake zipite.
Ni waziri mkuu alitakiwa kuonyesha njia ya kuwajibika kwanza kabla ya hao wengine wa chini yake.
 
Mtu wa kuachia ngazi hapa ni JK. Kiburi walichonacho ngeleja na jairo ni kwa sababu JK anahusika moja kwa moja na ndio maana ameshindwa kutoa maamuzi sahihi na kwa muda muafaka. Ushaidi uko wazi sasa kigugumizi cha nini????????????????????? Tumechoka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hapo itabidi wah wawe macho maana nshaanza kuona usanii unatakakujitokeza na yeye mkuu wa kaya kwa nini anaondoka uku nyumbani kwake kumeungua..

Alichokosea Pinda ni kujifanya naye amekasirika kwa barua ile ya Jairo. Haya mambo hayajaanza leo serikalini na wala hayafanyiki hapo nishati tu. Hili ambao tumewahi kuwa watumishi kwenye taasisi za UMMA tunalijua na Pinda analijua zaidi.
Wakuu swali ninalojiuliza hivi Katibu Mkuu ndio anafanya maamuzi ya Wizara???? Kama Ngeleja anamruka Jairo kuwa hajui kuhusiana na hiyo barua basi Ngeleja atakuwa ni kilaza kiasi ambacho hajui Katibu Mkuu wa Wizara yake anafanya nini, maana kama ameweza kuandika barua kuagiza vitengo vyote vilivyo chini ya Wizara vitoe hizo Milioni 50 na Ngeleja hajui je ni mambo mangapi Jairo ameishayafanya ambayo Ngeleja hana habari nayo wakati yeye ndiye Waziri husika wa hiyo Wizara lakini kwa hili nasita sana kuamini kuwa eti Ngeleja hajui kuhusiana na hiyo barua kwa maana nyingine nasema Ngeleja ni INCOMPETENT.
 
tunaposema jk ndo chanzo cha matatizo nchii huwa tunaamnisha.......mtu ametarifiwa na akapewa ushahid kuwa swala hili halivumiliki na huyu mtu anapaswa kufukuzwa...yeye bado analemba kwa kutoa maagizo mapya...
maagizo mapya haya hapa:
Ngoja kwanza nicheze ndombolo ya solo.....!
 
Heheee!
yaani hapo tunauzwa make hizo ni blaa blaa tupu, huyo babake na Riz1 ni pete na dore na katibu Jairo so kumuwajibisha itakuwa vigumu
 
Kama akiachwa salama, basi kuna ukweli sanaa na usanii una wenyewe na wanaumudu kweli kweli.
 
Wakuu swali ninalojiuliza hivi Katibu Mkuu ndio anafanya maamuzi ya Wizara???? Kama Ngeleja anamruka Jairo kuwa hajui kuhusiana na hiyo barua basi Ngeleja atakuwa ni kilaza kiasi ambacho hajui Katibu Mkuu wa Wizara yake anafanya nini, maana kama ameweza kuandika barua kuagiza vitengo vyote vilivyo chini ya Wizara vitoe hizo Milioni 50 na Ngeleja hajui je ni mambo mangapi Jairo ameishayafanya ambayo Ngeleja hana habari nayo wakati yeye ndiye Waziri husika wa hiyo Wizara lakini kwa hili nasita sana kuamini kuwa eti Ngeleja hajui kuhusiana na hiyo barua kwa maana nyingine nasema Ngeleja ni INCOMPETENT.
Maamuzi yote yasiyo na SIASA ndani yake anafanya KM. Hili la kuchangisha rushwa ni la kisiasa. Linamlinda zaidi Ngeleja. Jairo hajui tu kuziandika barua kama hizi. Mgao wake ulimzubaisha tu.
 
jamani huyu mtu kumbukeni alikuwa ikulu anajua uuchafu mzima wa rais kikwete na kama mmesoma gazeti la leo alipoulizwa akadai haana jibu la kusema ana siri yake moyoni..ipi mi na wewe atujui tusubiri kikwete aje na kama msiposikia kaenda zambia kuhani 40 ya chiluiba sijui ..
kumbukeni hata tunachosema hiki lazima mh ngeleja anajua uchafu mzima na tunapoelekea kuna vituko zaidi yetu macho
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo baada ya jana kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo.

Pinda alisema hayo, baada ya gazeti hili kumtaka aeleze hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo aliyetuhumiwa juzi bungeni kuwa aliziagiza zaidi ya taasisi 20 kuchanga Sh50milioni kila moja kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

"Suala hilo bado tunalifanyia kazi," alisema Pinda alipotakiwa kueleza maagizo aliyopewa na Rais baada ya kuwasiliana naye juzi na jana. "Ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza."

Akizungumzia suala hilo la Jairo bungeni juzi, Pinda alisema: "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.
Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.

"Tuhuma za rushwa katika Wizara ya Nishati na Madini ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alipokuwa akichangia Makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni juzi.

Shellukindo alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma.

"Tena inaagiza kwamba fedha hizo zikishatumwa kwenye akaunti hiyo, wizara ipewe taarifa kupitia Ofisi ya DP kwa ajili ya utaratibu," alisema Shellukindo akiinukuu barua hiyo.


hayomaagizo yawe ya kumuwajibisha Geleja na Malima huwenda utaeleweka vinginevyo hatutaacha kukuchachafya kwasababu nyie ni wale wale hamna lolote lile, hii ishu hata rais anaijua. aliachabomu akakimbilia south africa ili atoe maagizo mepesi mepesi
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Raisi wenu anahusika kwenye hii scandal na ndio maana Jairo amewajibu waandishi wa habari kuwa kwa hivi sasa hana cha kuwajibu wasubiri kwanza maamuzi
 
................................

Hivi katibu mkuu ndio anafanya maamuzi ya wizara?

Yes kitendaji makatibu wakuu ndio accounting offficers.

Kifupi maamuzi na mtumizi yoyote matumizi ya wizara lazima yaidhinishwe na ofisi ya katibu mkuu . Kuna mambo ambayo waziri anaweza asijue kuhsu wizara lakini PS anatakiwa kuwa most informed personel kwenye wizara. n dality t daily basin na with details.

So kitendaji katibu mkuuu ndo anafanya maamuzi but kisasa ni waziri.

Waziri hawezi kufanya dili ya mshiko bila katibu kumuhusisha katibu mkuu lakini katibu mkuu anaweza kupiga deal bila waziri
 
Kuna ulazima wa kupigania katiba mpya haraka iwezekanavyo. Hii iliyopo inampa rais madaraka makubwa sana. Sasa bahati mbaya tulioipata ni hii ya kuwa na rais dhaifu kimaamuzi. Sidhani kama rais wetu hata kama anajua madhara yaliyosababishwa na kukosekana kwa umeme nchini. Maana kama angekuwa ana ufahamu wa kile kilichokuwa kikiendela bungeni wakati wa mjadala wa wizara ya nishati na madini, asingesafiri nje ya nchi kuhudhuria birthday ya mstaafu M. Hata Lowasa alipoishutumu serikali kwa kutokua na maamuzi alifahamu fika udhaifu wa kiongozi mkuu wa serikali, na kwamba alikuwa hana ubavu wa kumwajibisha kama sii yeye mwenyewe kujiuzulu kwa shinikizo la bunge na sii rais. Jk yeye alidandia gari ya bunge na kujifanya derever kuhusu sakata la richmond, lakini kiukweli dereva alikuwa ni Sita. Sasa hivi Hosea ndie chombo cha rais cha kuzuga katika deal zote za wizi mkubwa mkubwa. Takukuru ni taasisi mfu inayokula mifupa baada ya nyama kuliwa na wengine. Hakuna wizi mkubwa hata mmoja waliwahi kuugundua wao kama wao zaidi ya kusubiri wezi wakamatwe na watu wengine ndio nao wadandie issue.
.
 
Hizi statement mbili hizi, yaani ilipaswa huyu mtu achuliwe hatua sasa sijui hayo maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo wanalazimika kuyafanyia kazi ni yapi na kwanini hawayasemi kwani imeishakuwa ni siri?????
Wanamtafutia wizara nyingine ya kumpa.
 
Mimi sishangilii sana Jairo kutimuliwa kazi, hata kidogo.

Imani yangu na nitazidi kuamini hivyo mpaka siku ya Mwisho ni kwamba jairo hakuamka kitandani kwake na kuingia ofisini aandike ile barua.
Kama lilikua wazo lake Binafsi lazima walikaa vikao na kushauriana na waziri husika au mkubwa mwingine.

Kama sio wazo lake ni lazoma alipewa maelekezo na aliye juu yake.

Inaposemekana rais ametoa maagizo mapya nakubaliana mia kwa mia na na hilo kwasababu Ni issue kubwa ambayo hamhusu Jairo peke yake au haimhusu yeye kabisa.

Hivi katibu mkuu ndio anafanya maamuzi ya wizara?
Mahali wannaiacha hoi ni wapi bajeti ya fedha ipi walitumia? Ya Wizara 2011/2012 haijapitishwa, Tayari walikuwa nazo! Kwa vipi?
 
Nakubaliana na aliyesema kuwa Jairo hakukurupuka yeye binafsi. Wizara ya Madini ni sehemu ya Ulaji wa Wakubwa wote. Mimi nakwenda mbali zaidi. Hata Ngeleja, wakati mwingine ni kama hahusiki. Pale, yeye ni figurehead tu. Anatekeleza maagizo ya Mkubwa/wakubwa fulani. Nitajaribu kueleza kidogo. Wakati wananchi wameanza kuja juu kuhusu kushindwa kazi kwa Ngeleja na kumtaka ajiuzuru, yeye alitoa press release kuwataka wananchi wawapuuze watu wanaomtaka ajiuzuru kwakuwa wanajitafutia umaarufu wa kisiasa. Unajua hata mtoto mdogo haitaji kuambiwa kuwa Ngeleja ameshindwa kazi. Giza lililopo nchini likiambatana na porojo lukuki za namna tatizolinavyoshughulikiwa, huku ikiwa wazi kabisa tuko mbali na suluhu, ni wazi kuwa kunakushindwa kazi. Sasa anapotaka kutuaminisha wananchi kuwa yeye anaweza kazi na kuwa wanaeleza kushindwa kwake wanatafuta umaarufu. Kwa maoni yangu, huyu mtu ameambiwa wapuuze hao wanaokutaka ujiuzuru na uendelee kuleta pesa kwa namna yoyote uwezavyo. Washirika wake, au tuseme watekelezaji wa makusanyo ndio hao, akina Jairo. Mbinu ni pamoja na hizo ruzuku (tusiite rushwa) kutoka taasisi zinazosimamiwa kiutendaji na Wizara, pamoja na madudu yaliyoonekana kwenye bajeti ya wizara hiyo. Yaani lazima wachakachue hata kama ni kwa waziwazi. Ikiwa wazi sana, tutawaziba midomo wabunge wapenda posho kwa posho ya ziada (Nafikiri unawajua wabunge wapenda posho).

Kwahiyo, si ajabu kwa JK kujaribu kuchakachua maamuzi ambayo Pinda alijaribu kuyadokeza. Vinginevyo, wamtoe kafara huyo Jairo na Ngeleja. Lakini hilo ni dili la wengi.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya wajumbe vocal wa kamati ya Januari walihongwa na Wizara hiyohiyo. Ghafla, Januari alishangaa wajumbe waliokuwa wakali sana, wamelegea. Sina kumbukumbu kama kulitolewa adhabu kwa waliohonga na kuhongwa. Zaidi, nakumbuka kupata taarifa ya hongo nyingine, safari hii kwa wabunge. Wakati tukitarajia Rais atoe maagizo ya hatua kali, tunamsikia Waziri Mkuu akisema amepewa maagizo mapya. Nafikiri unaweza kupata majibu bila kukokotoa sana. JK haepuki lawamaa
 
Maamuzi yote yasiyo na SIASA ndani yake anafanya KM. Hili la kuchangisha rushwa ni la kisiasa. Linamlinda zaidi Ngeleja. Jairo hajui tu kuziandika barua kama hizi. Mgao wake ulimzubaisha tu.
Kama suala hili ni la kisiasa litamlindaje tena Ngeleja wakati cheo chake ni cha kisiasa.
Hapa hakuna cha Jairo Ngeleja wala Adam wote kundi moja.
 

Yes kitendaji makatibu wakuu ndio accounting offficers.

Kifupi maamuzi na mtumizi yoyote matumizi ya wizara lazima yaidhinishwe na ofisi ya katibu mkuu . Kuna mambo ambayo waziri anaweza asijue kuhsu wizara lakini PS anatakiwa kuwa most informed personel kwenye wizara. n dality t daily basin na with details.

So kitendaji katibu mkuuu ndo anafanya maamuzi but kisasa ni waziri.

Waziri hawezi kufanya dili ya mshiko bila katibu kumuhusisha katibu mkuu lakini katibu mkuu anaweza kupiga deal bila waziri

Naweza ni kakubaliana na wewe kuhusu katibu kupiga dili bila waziri kujua, ila hili la kutoa rushwa ili bajeti ipite inamuhusu waziri moja kwa moja maana waziri huwasilisha mapendekezo yake na katibu huanza kuyashughulikia, na kwakuwa katibu siyo mwanasiasa wala hahusiki kushawishi wabunge wapitishe bajeti kwakujenga hoja bungeni ni dhahiri mwenye dhamani hii ni waziri kwani yeye ndiye mwanasiasa na anajua upepo umekaaji kwa wanasiasa wenzake kuhusiana na bajeti ya wizara yake.

sasa tukiambiwa NGELEJA hajui na sisi tukakubali kuwa ni kweli hajashirikishwa kwenye hii dili tutakuwa ni wehu ama hata zaidi ya wehu. hii ishu niagizo kutoka kwa mkuu wa nchi kuja kwa waziri na waziri kupeleka kwa katibu , nitatoasababu kwanini nimesema niagizo la rais. ni kwakuwa mkuu wa nchi hawezi kubali tena kuweza kuona baraza lake la mawaziri lina tetereka kwakuwa anafahamu hali halisi na hii ndiyo sababu kuu.
 
Mimi sishangilii sana Jairo kutimuliwa kazi, hata kidogo.Imani yangu na nitazidi kuamini hivyo mpaka siku ya Mwisho ni kwamba jairo hakuamka kitandani kwake na kuingia ofisini aandike ile barua.Kama lilikua wazo lake Binafsi lazima walikaa vikao na kushauriana na waziri husika au mkubwa mwingine.Kama sio wazo lake ni lazoma alipewa maelekezo na aliye juu yake. Inaposemekana rais ametoa maagizo mapya nakubaliana mia kwa mia na na hilo kwasababu Ni issue kubwa ambayo hamhusu Jairo peke yake au haimhusu yeye kabisa. Hivi katibu mkuu ndio anafanya maamuzi ya wizara?
Ahsante umelijua wazo langu.
 
Back
Top Bottom