Arafat
JF-Expert Member
- Nov 17, 2009
- 2,581
- 758
si ajabu rais anataka waanze kufanya uchunguzi kama kawaida watasema wanaunda kamati. kweli kuna haja ya mambo yote yaongozwe na katiba ya nchi si mtu moja.
Inakuwaje kiongozi wa serikali bungeni hana mamlaka ya kuwawajibisha anaowasimamia bungeni? nini maana ya kuwa kiongozi? And anyways tunajua Vasco alikua safarini, lakini si makamu wake yupo? Grrrrrr...... aah wacha niseme.wakati mwingine mimi naona bora Lowasa.
Atakuwa kaambiwa atulize mambo ikiwezekana ajaribu kuchakachua akili za wabunge bajeti ipite.
kwa vyovyote atakuwa amemwambia kuwa hata yeye anahusika.
nchi hii hatuna head of state....
Mimi sishangilii sana Jairo kutimuliwa kazi, hata kidogo.
Imani yangu na nitazidi kuamini hivyo mpaka siku ya Mwisho ni kwamba jairo hakuamka kitandani kwake na kuingia ofisini aandike ile barua.
Kama lilikua wazo lake Binafsi lazima walikaa vikao na kushauriana na waziri husika au mkubwa mwingine.
Kama sio wazo lake ni lazoma alipewa maelekezo na aliye juu yake.
Inaposemekana rais ametoa maagizo mapya nakubaliana mia kwa mia na na hilo kwasababu Ni issue kubwa ambayo hamhusu Jairo peke yake au haimhusu yeye kabisa.
Hivi katibu mkuu ndio anafanya maamuzi ya wizara?
Ubaya wa kurundika maamuzi kwa Rais ndio haya matokeo ya maneno ya Pinda, pamoja na kwamba rasimu ya katiba mpya inaandaliwa lakini kuna umuhimu wa kuujulisha uma kupitia scandali hii kwamba haki haitapatikana kwa mfumo huu tulionao hivi sasa na tegemeo letu ni vyama vya upinzani kutuunganisha kwa maandamano ili ujumbe ufike ndani na nje ya inchi
Anaposema mapya ni dhahiri sasa ni tofauti na lile lake la kumfukuza mara moja, na anaenda mbali zaidi kusema wanalifanyia kazi ina maana linahitaji muda si kam alivyosema kuwa kama ni yeye alikuwa ni kutamka tu! Mara moja. Swali linalobaki gizani ni mapya yapi hayo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi?
Kama ingelikuwa ni kumchunguza ni lazima wangemsimamisha kazi mara moja ili uchunguzi uanze, hivyo nachelea kusema kuwa wana mchunguza! Kama ni kujuwa wahusika wote hili wachukuliwe hatua kwa pamoja nadhani pia hisinge zuia yeye kusimamishwa kazi na kuchukuliwa maelezo na katika maelezo yake ndipo uchunguzi wa mwanzo unge baini njia ya kutambuwa walio nyuma yake.
Hivyo basi ni dhahiri wanatafuta jinsi ya kuchakachuwa hili jambo! au wanataka kummaliza aondoke na ushahidi wote? sidhani au wanataka kumuamisha haraka hili kumuepusha na janga ya kuzee kichaa, maana nimemuona kama mzee vile akifukuzwa leo Penshen ya Katibu Mkuu ambayo ndugu yake na Swahiba wake alikuwa anamtafutia hataipata! kwahiyo nadhani wanataka awe katibu Mkuu Mstafuu kama kawaida ya CCM badala ya Mtuhumiwa! This is fine watakuwa wamemsaidia sana, ila wajuwe kila upuuza watakaofanya katika hili jambo litakuwa Milestone ya kuikaanga CCM, waamue ama kuisaidia Chama au Mpuuzi mmoja!
Labda wanataka kubadili baraza la mawaziri kwahiyo kampa kazi ya kuunda jipya akija walifanyie kazi na kulitangaza? Hili litakuwa wazo zuri sana, lakini watapata wapi watu maana Wabunge wa CCM ni wale wale. Myt: wote hovyo wote Posho na Rushwa, wazo zuri lakini siyo feasible; Pole sana Kikwete, haya ni madhara ya kuchakachuwa wagombea ubunge majimboni, itabidi CCM kama si sikio la kufa ijifunze kuanzia hapa maana najuwa ni kazi ngumu sana kupata watu safi wenyewe uwezo wa kuongoza wizara zote zilizopo kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM waliopo sasa, kazi ngumu sana labda waunganishe baadhi ya wizara.
Pinda tunasubiri, Muhimu waandishi wa habari warudi wamuulize tusubiri hadi lini?