Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

kwa kweli ukiona manyoya ujue kaliwa na dalili ya mvua ni mawingu, wingu hilooo limeshakuja kwa mtindo wa maagizo mapya, kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firaun
 
Enz zile nipo UDSM...Maandamano yamekolea,malalamiko dhidi ya Bodi ya Mikopo kutangaza uwepo wa 40% kila mwanafunz ajilipie....nikaandka bango kuubwaaa "TATIZO SIO BODI YA MIKOPO...NI HII SERIKALI YA KISHIKAJI YA KIKWETE"....."ELIMU YA JUU NI LAZMA!SAFARI ZA NJE NI ANASA NA UFISADI" Mkandala na Mwenzake Msola wakankomalia eti mi "muhuni"mpaka nikarudi mtaani...Lakn leo usanii wa JK Unaonekana!Jaman uyu jamaa tumfanyaje?kawa sugu(simanish Mr.II)
 
UK Premier kakatiza ziara baada ya skandali ya News of the World,Huku kwetu mteule wa Rais katuhumiwa kuchanga fedha kwa matumizi yanayoelekea kuwa rushwa wakti huo huo nchi bado ingali katika giza totoro bila ya ufumbuzi wa kuaminika,Rais yuko SA anatembelea kisiwa cha Robben...napata taabu kujua vipaumbele vya Mkuu wetu...
 
Hivi tutaendelea kusikia ma upuuzi kama haya mpaka lini hivi hatuwezi kuchukua madaraka kwa nguvu ya umma na kuwaweka viongozi wanaostahili?
 
Kama wameshindwa kumfukuzu Jairo tunaomba basi Pinda mwenyewe ajiuzulu kwani amedanganya umma kwa mara nyingine tena!
 
Suluhisho pekee katika maisha tuliyonayo na kukabiliana na majibu mepesi kwa matatizo mazito ni kudai KATIBA MPYA ndani ya miaka 2 hii tulionayo na siyo kusubiri 2014, maamuzi mengi anayafanya mtu mmoja, na nina imani hoja hii ikurudi bungeni itapitishwa tu na wabunge wa CCm hata kama hatua kadhaa hazijachukuliwa.

Nchi hii watu wengi kama sio wote hatuna Uzalendo wa kweli kutoka moyoni, Unafiki ndio mwingi, bila watu kumwomba Mungu na kudai haki zao hatutoki hapa tulipo, ninaongea haya kwa uchungu mkubwa kwani viongozi hawapo serious na Nchi na pia Watanzania wengi hawapo serious na Nchi.
 
Hivi kama Pinda amepewa maagizo mapya, je yale ya zamani ni yapi? Au ndio yaliyotekelezwa na Jairo?
 
Nakumbuka siku ile JK alipoitisha kikao cha mawaziri wote na makatibu wa wizara, aliwaasa kwamba wafanye kazi kwa kushirikiana, na wote wawe kitu kimoja na wala isitokee maziri kafanya jamba bila naibu wake kulifahamu na katibu wake pia! Wote wapeane taarifa kwenye wizara wasije wakawa na misimamo inayokinzana! Kikao Hichi kilirushwa na TBC1, sasa kwani nini Ngeleja na Malima wanataka kujitoa kwenye hili! wote wamebariki uamuzi wa kuandika barua hiyo kwa lengo la kutoa rushwa! Mimi Namshangaa sana bwana Hosea wa Takukuru kwa nini hadi sasa hajaanza uchunguzi hadi sasa au kuwafikisha mahakamani kwa sababu ushaidi upo! Hata Pinda wenyewe kasema hakuna wa kulikataa hili jambo!
 
Hivi Sharobalo akisafiri na nchi haina Rais? Tumekwisha, anasafiri na nchi ya Wadanganyika mfukoni mwake.
 
naamini pinda anafedheeka sana moyoni na kuona Rais ni lege lege.maana kwa kauli yake ya juzi ni kwa huyu jairo angekuwa hana kazi lakini kwa kuwa syndicate nzima inamhusisha rais basi lazima afanye manuva ili a spin issue nzima.......na inavyoonekan hapa ni kuwa huyu jamaa(jairo) anaweza kusave
Yaleyale msingenishikilia angenitambua, Pinda ni msanii wa kimataifa anataka tumuone mchapakazi wakati hana lolote mbona rais akiwepo hatujaona ushauri wake.
 
Labda Rais atafanya maamuzi magumu sasa hivi kulingana na maneno ya Lowasa ili aonyeshe Serikali yake ipo makini.
 
Mpwa hujaelewa analifanyia kazi maanake jinsi gani tuhuma hizi atakavyo zipotezea
Mpwa kwa suala hili jinsi kila mwananchi alivyolitolea macho sidhani kama jamaa anaweza kupotezewa tuhuma hivi hivi kijuujuu tu
 


Hizi statement mbili hizi, yaani ilipaswa huyu mtu achuliwe hatua sasa sijui hayo maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo wanalazimika kuyafanyia kazi ni yapi na kwanini hawayasemi kwani imeishakuwa ni siri?????

Hapa naona wanatafuta namna nzuri ya Kulindana, Si unamjua Dagama anavyowapenda penda washkaji zake.
 
Jairo atakuwa ameongea na Rais na kumpa ukweli wote. Mimi naamini Jairo ameyakuta haya yakifanyika hapo wizarani kwa miaka mingi tu. Hauwezi kukurupuka na kuandika usichokijua. Mimi namshangaa Pinda anayejidai kuyaona haya kama mapya na ya ajabu serikalini!
 
Back
Top Bottom