Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

Pinda: Rais amenipa maagizo mapya

Waziri hawezi kufanya dili ya mshiko bila katibu kumuhusisha katibu mkuu lakini katibu mkuu anaweza kupiga deal bila waziri
Kinadharia sawa lakini practically haiwezekani kuwatenganisha hasa ukizingatia wanafanyia kazi tanzania ingekuwa nchi za wenzetu sawa.
 
Hivi Jairo kapatia au kakosea aliposema kuwa Wabunge ni sawa na Ze komedi?? maana hata majibu ya Pinda na madai hayo ya Jairo kuwa ni Komedi kama vile yanaendana fulani hivi...nimeuliza tu
 
Tatizo Rais amelimbikiziwa madaraka mengi sana hadi imekuwa kero yaani kuteua Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na mengine yote hayo anafanya Rais pia kuwafukuza hadi asubiriwe Rais ndio atoe uamuzi huu ni upuuzi mtupu kama sio utumbo

Ni utumbo kweli, kwa statement ya Pinda Juzi sikutegemea Rais anaweza kuwa na maaelekezo mengine, spinning as usual anatafuata jinsi ya kumuokoa Ngeleja.
 
Yaleyale msingenishikilia angenitambua, Pinda ni msanii wa kimataifa anataka tumuone mchapakazi wakati hana lolote mbona rais akiwepo hatujaona ushauri wake.
pinda hana makosa. Angekuwa na mamlaka rasmi angekuwa tofauti na sasa. Wakati huu anatumia akili nyingi sana kuziba ishu jambo ambalo anaonekana hapendi. Mnakumbuka ishu ya albino?
 
yaani ni hivi kuna vitu ambavyo ni against sheria na kanuni na taratibu za kazzi lakini kwa sababu ya mazoea ndio inakuwa hivyo, yaani unaiba hadi unajikuta ule wizi unakuwa sehemu ya maisha ya kila siku sawa na ilivyokuwa kwa Takrima na upuuuzi mwingine, mimi naamini kuwa kilichotokea ni either Shelukindo alikosa mgawo au mtu wake wa karibu (pengine mmoja wa wana-kamati) alikosa mgawo au alipewa below mgao na akamtumia Shelukindo kuwalipua wenzie, hata hivyo hadi kuandikwa barua na Yoriyori sorry Jairo ina maana huu uchafu ulikuwa unatendeka siku nyingi na sehemu ya maisha ya kila siku ya bunge, wabunge, wizara na watendaji wake....anaebisha labda kakosa mgao.
 
Naweza ni kakubaliana na wewe kuhusu katibu kupiga dili bila waziri kujua, ila hili la kutoa rushwa ili bajeti ipite inamuhusu waziri moja kwa moja maana waziri huwasilisha mapendekezo yake na katibu huanza kuyashughulikia, na kwakuwa katibu siyo mwanasiasa wala hahusiki kushawishi wabunge wapitishe bajeti kwakujenga hoja bungeni ni dhahiri mwenye dhamani hii ni waziri kwani yeye ndiye mwanasiasa na anajua upepo umekaaji kwa wanasiasa wenzake kuhusiana na bajeti ya wizara yake.

sasa tukiambiwa NGELEJA hajui na sisi tukakubali kuwa ni kweli hajashirikishwa kwenye hii dili tutakuwa ni wehu ama hata zaidi ya wehu. hii ishu niagizo kutoka kwa mkuu wa nchi kuja kwa waziri na waziri kupeleka kwa katibu , nitatoasababu kwanini nimesema niagizo la rais. ni kwakuwa mkuu wa nchi hawezi kubali tena kuweza kuona baraza lake la mawaziri lina tetereka kwakuwa anafahamu hali halisi na hii ndiyo sababu kuu.
Unajua mimi nawashangaa sana watu wanaosema Ngeleja hahusiki wakati yeye ndiye waziri husika wa bajeti hiyo na cheo chake ni cha kisiasa na anataka bajeti yake ipitishwe na wanasiasa wabuge na tunajua toka mapema alivyokuwa anahangaika bajeti ipite tangu enzi za kamati ya January leo mtu atokee aseme hahusiki increadible. Yaani mnataka kutuambia Jairo aanze kugawa pesa ili bajeti ya Ngeleja ipite bila Ngeleja kujua kweli tutakuwa zaidi ya wehu.
 
Mpwa, kuna vitu katika uongozi vinaitwa Chain of Command, yaani nani ana uwezo wa kutoa taarifa, utendaji kwa mwingine, this simply imply kwamba,JK asipokuwepo kuna Makamu wa rais na huyo Pinda pengine (japo anaonekana kujikana) walitakiwa kufanya maamuzi na kumpa feedback aliyemteua as far as decision made ni crucial kwa manufaa ya taifa, Jk ni part ya Taifa so kama mtendaji aliyemteua analeta upupu halafu hamtaki kumuondoa hadi aliyemweka aje kumuondoa sidhani kama itakuwa na maana kuwa na makamu na PM ambao hawana maamuzi, kwa uweleewa wangu ni kwamba kuna mambo including hili lazima yanafanyika hata kama raisi hayupo. Mfano kama Jairo angekuwa anataka kutuua fasta fasta (mana hii ya sasa anataka kutuua slow slow) je hakuna hatua zozote ambazo zingechukuliwa just kwa sababu hakuna mtu wa kumuadhibu kwa kuwa aliyemweka hayupo?? Ujinga huuu, Naunga hoja mkono ya Jairo kuwaita wabunge na bunge zima kuwa ni sawa na kikundi cha Komedi na hawana ubavu wa kumfanya chochote.
pinda hana makosa. Angekuwa na mamlaka rasmi angekuwa tofauti na sasa. Wakati huu anatumia akili nyingi sana kuziba ishu jambo ambalo anaonekana hapendi. Mnakumbuka ishu ya albino?
 
Mbunge huyu kajitahidi kuumbua mambo jamani...serikali ya uwazi na ukweli sasa tunaiona...halafu hooo wanafichanaaa.sifieniii serikali kwa hilo
 
Naweza ni kakubaliana na wewe kuhusu katibu kupiga dili bila waziri kujua, ila hili la kutoa rushwa ili bajeti ipite inamuhusu waziri moja kwa moja maana waziri huwasilisha mapendekezo yake na katibu huanza kuyashughulikia, na kwakuwa katibu siyo mwanasiasa wala hahusiki kushawishi wabunge wapitishe bajeti kwakujenga hoja bungeni ni dhahiri mwenye dhamani hii ni waziri kwani yeye ndiye mwanasiasa na anajua upepo umekaaji kwa wanasiasa wenzake kuhusiana na bajeti ya wizara yake.

sasa tukiambiwa NGELEJA hajui na sisi tukakubali kuwa ni kweli hajashirikishwa kwenye hii dili tutakuwa ni wehu ama hata zaidi ya wehu. hii ishu niagizo kutoka kwa mkuu wa nchi kuja kwa waziri na waziri kupeleka kwa katibu , nitatoasababu kwanini nimesema niagizo la rais. ni kwakuwa mkuu wa nchi hawezi kubali tena kuweza kuona baraza lake la mawaziri lina tetereka kwakuwa anafahamu hali halisi na hii ndiyo sababu kuu.

Nakubaliana na wewe kabisa . Nilichojaribi kumueleza jamaa scenario ni tofauti inawezekanaje kutokea hivyo na nimeandika jinsi dili lolote waizri akitaka kufanya lazima amshirikishe PS hata kama PS hausiki lazima PS aandike kwa maelekezo ya Waziri au mamlaka ya juu

Sababu hata correspondent zote za wizara zinakuwa na adress ya katibu mkuu.

Na kwa kuwa pesa zinaagizwa zielekezwe Dodoma simple laymen forensic inanyesha kazi yake ilikuwa ni ya "kisiasa"

Je
  • Ni bwana Jairo( Mtedaji) ndio aliwashaurii Bwana Ngelejana bwana Malima kuwa hiyo ndio best way ya kupitisha bajeti na kina ngeleja akakubali?
  • Au ni bwana Ngeleja na malima ndio walimwagiza bwana Jairo awezeshe huo mpango haramu na Bwana jairo akatelekeleza. Pia bwana Jairo hawezi kuchomoka .atakuwa na kosa alitakiwa kuwa mshauri na kuwaambia Hii sio matumizi bora ya pesa za umma.
So nakubaliana na wanaosema Hirearchy nzima ya hiyo wizara ilitakiwa kukaa pmebeni kabla hata Pinda hajasema maamuzi yoyote.

Kinadharia sawa lakini practically haiwezekani kuwatenganisha hasa ukizingatia wanafanyia kazi tanzania ingekuwa nchi za wenzetu sawa.

Mkuu mimi sijawetenganishi. Hao Magamba wako ofisi moja nilichajirbu kumpa mwanga muuliza swali ni kuonyesha nini inaweza kuwa mchango wa kila mtu katika hili sakata. Kinachomuingiza Ngeleja mpaka sasa ni sababu hizo pesa inasemwa zipelekwe dodoma . na wote tunajua dodoma kuna ssue ya kisiasa sio kitendaji.

Nimeandika waizri hawezi kufanya dili bila PS na inawezekana ndio maana tunamtaja jairo katika hili .M ay be mawazo hayo ni ya Ngeleja na mwezake malima au watu wa sera na mipango wa Nishati. L akini hata kama sio mawazo yake alitakiwa kukataa sababu sio sahihi.

Tuko pamoja muu
 
wanataka kulifanya swala hili liwetamu zaidi unajua magamba huwa hawasomi alama za nyakati siku zote hufanya maamuzi too late na huwa inawagharimu sana kisiasa. Ngoja tusubiri hapa wananchelewesha tu maamuzi lakini hakuna namana ya kuokoa chochote na wakifanya vinginevyo lazima ile kwao.

Tangu lini Magamba wakawa na uwezo wa kusoma alama za nyakati? Kama wangeweza kuwa na uwezo huo akina 6 na mwakembe wangekwenda kwenye maandamano ya kitoto na kuongea utumbo pale Mbeya?
Kusoma alama za nyakati unatakiwa utulie na kutafakari na si kurukaruka angani kama popo.
 
Unajua mimi nawashangaa sana watu wanaosema Ngeleja hahusiki wakati yeye ndiye waziri husika wa bajeti hiyo na cheo chake ni cha kisiasa na anataka bajeti yake ipitishwe na wanasiasa wabuge na tunajua toka mapema alivyokuwa anahangaika bajeti ipite tangu enzi za kamati ya January leo mtu atokee aseme hahusiki increadible. Yaani mnataka kutuambia Jairo aanze kugawa pesa ili bajeti ya Ngeleja ipite bila Ngeleja kujua kweli tutakuwa zaidi ya wehu.

mkuu. watu wengi wapo kiushabiki zaidi badala kusimamia ukweli pale linapokuja swala nyeti kama hili, yaani kumsafisha Ngeleja na kumuhukumu Gairo ni sawa sawa na dereva kuacha gari lijiongoze lenyewe.
 
waziri mkuu, mizengo pinda ana siri nzito kuhusu hatima ya katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini david jairo baada ya jana kusema kuwa rais jakaya kikwete amempa maelekezo mapya kuhusu suala hilo.

Pinda alisema hayo, baada ya gazeti hili kumtaka aeleze hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya katibu mkuu huyo aliyetuhumiwa juzi bungeni kuwa aliziagiza zaidi ya taasisi 20 kuchanga sh50milioni kila moja kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

"suala hilo bado tunalifanyia kazi," alisema pinda alipotakiwa kueleza maagizo aliyopewa na rais baada ya kuwasiliana naye juzi na jana. "ndio niliwasiliana naye lakini, ametoa maelekezo mapya kuhusu suala hilo ambayo tunalazimika kuyafanyia kazi kwanza."

akizungumzia suala hilo la jairo bungeni juzi, pinda alisema: "kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.
Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa rais atakapotua south africa (afrika kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.

"tuhuma za rushwa katika wizara ya nishati na madini ziliibuliwa juzi na mbunge wa kilindi (ccm), beatrice shellukindo alipokuwa akichangia makadirio ya wizara ya nishati na madini bungeni juzi.

Shellukindo alisema, jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na geological survey of tanzania (gst) kwenye benki ya nmb, tawi la dodoma.

"tena inaagiza kwamba fedha hizo zikishatumwa kwenye akaunti hiyo, wizara ipewe taarifa kupitia ofisi ya dp kwa ajili ya utaratibu," alisema shellukindo akiinukuu barua hiyo.

jairo ni shosti wake mkuu kabisa. What do you expect?
 
najua jairo hawezi fukuzwa hivi hivi labda atafutiwe sehemu nyingine maana jairo na kiikwete ni watu waliokua pamoja wakati baba yake jairo akiwa katibu kule singida na jamaa ndo alikua anaingia pale sasa akawa anaishi kwao akina jairo hivyo kwa mahesabu ya kawaida ni kwamba walikua pamoja na nyumba moja sasa hapo unafikiri kuna kufuzana!!!! ha ha ha tumeliwa pia huo mchezo ni jambo la kawaida kwa serikali maana kuhonga ili bajeti ipite kwa jairo ni niksi tu aliamka vibaya
 
Tatizo nchi ikiwa haina checks and balance...powers zote kwa mtu mmoja!...bado tuko mballi na mfumo wa good governance.
 
Yaani hii kauli imekaa kama ya housegirl vile...........
"Baba amesafiri ameniachia maagizo ni ................."
 
Nakubaliana na wewe kabisa . Nilichojaribi kumueleza jamaa scenario tofauti inawezekanaje kutokea hivyo na nimeandika jinsi dili lolote waizri akitaka kufanya lazima amshirikishe PS hata kama PS hausiki lazima PS aandike kwa maelekezo ya Waziri au mamlaka .

Sababu hata correspondent zote za wizara zinakuwa na dress ya katibu mkuu.

Na kwa kuwa pesa zinaagizwa zielekezwe Dodoma simple laymen forensic inanyesha kazi yake ilikuwa ni ya "kisiasa"

Je
  • Ni bwana Jairo( Mtedaji) ndio aliwashaurii Bwana Ngelejana bwana Malima kuwa hiyo ndio best way ya kupitisha bajeti na kina ngeleja akakubali?
  • Au ni bwana Ngeleja na malima ndio walimwagiza bwana Jairo awezehe huo mpango haramu na Bwana jairo akatelekeleza. Pia bwan Jairo hawezi kuchomoka .atakuwa na kosa alitakiwa kuwa mshauri na kuwaambia Hii sio matumizi bra ya pesa za umma.
So nakubaliana na wanaosema Hirearchy nzima ya hiyo wizara ilitakiwa kukaa pmebeni kabla hata Pinda hajasema maamuzi yoyote.

kwenye hiyo Red hapo huwo ndiyo ulikuwa mpango mzima wanaobisha eidha ni wavivu wa kufikiria ama wanafanya mkusudi ilikunogesha mjadala, ila huwo ndiyo ukweli waziri na naibu wake pamoja na mkuu wa nchi wamo kwenye huwo mpango mzima.

HAKI NA UKWELI HAVIJAWAHI KUSHINDWA WANAO JARIBU KUBISHANA NA UKWELI HAWANA MUDA UKWELI UTAWADHALILISHA
 
Wanataka kulipotezea swala hili kiaina, tunasubiri tuone jinsi ambavyo watalichakachua ikiwa ni pamoja na kuwahusisha wabunge ili lionekane kuwa ni deal la wabunge. Wabunge wa upinzani hasa CHADEMA kuweni makini sana wasijekuwawekea fedha batili kwenye A/C zenu bila nyinyi wenyewe kujua kisha waseme Wabunge wa Chadema walipokea rushwa.
 
Back
Top Bottom