Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Pinda afuta amri ya Waziri Magufuli

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Kama ilivyotarajiwa, Serikali imesalimu amri! Sheria imepindwa, na sasa wenye malori ruksa kuendelea kuharibu barabara.

Juzi niliyasema hapa Jukwaani kuwa nitashangaa kama Pinda ataunga mkono msimamo wa Magufuli.

Huu ndiyo wakati mzuri kwa mtu kama Magufuli kujiuzulu maana kila anapojaribu kuafuata sheria, anapigwa nyundo ya utosi.
 
Hii ni mara ya pili sasa Magufuli anabwagwa na Serikali yake!
 
Bado kuna watu hawataamini kuwa hii serikali ni DHAIFU eti!!!!! Maskini TZ yangu.
 
Kama ilivyotarajiwa, Serikali imesalimu amri! Sheria imepindwa, na sasa wenye malori ruksa kuendelea kuharibu barabara. Juzi niliyasema hapa Jukwaani kuwa nitashangaa kama Pinda ataunga mkono msimamo wa Magufuli. Huu ndiyo wakati mzuri kwa mtu kama Magufuli kujiuzulu maana kila anapojaribu kuafuata sheria, anapigwa nyundo ya utosi.
Salaam kiongozi.Kujiuzulu atakwambia SIYO SERA YA CHAMA CHAO hivyo mwache tuendelee kumchukia kwani naye kazidi misifa.Hakuna ishu ya kufata sheria hapa wengi wao wameingia madarakani kwa wizi ,rushwa na hila hivyo usitegemee jipyaHata aliyemteua alishamwambia apunguze ubabe.,.Pinda endelea kupinda ili mtumishi wako aadhirike zaidi.
 
lazima awe mdogo kwa kauli ya waziri mkuu, ............
ni kweli huyu (magufuri) anakuwa na idea/ wazo ambalo linaweza kuwa na faida sana lakini ndio hivyo....... nyundo ya utosi. ( kpnd: alipokuwa wizara ya mifugo alitoa wazo la kusajiri mifugo yote hapa tz, lakini hakufanikiwa).

pia napata wasiwasi kwamba, pengine anagusa Maslahi ya wakubwa ili apate Prommo kwa kuwa anajua anachokifanya.
 
Ni wazi kuwa Magufuli ni mkurupukaji tu na kauli zake za kidhalilishaji, safari hii amekutana na watu wasio na njaa kama yeye, alidhani hawa ni sawa na wale aliowaambia wapige mbizi?
 
Uamuzi wa waziri Magufuli ulikuwa ni wa kujitafutia sifa za kijinga kwa gharama za kuhujumu uchumi wa nchi.

Kwa taarifa yenu weigh bridges za Tanroads zina variations za ajabu. Unakuta transporter anapima mzigo mzani wa Kibaha anapata readings X, akipima mzigo huo huo Chalinze bila kuongeza hata kilo moja anapata readings Y, akipima mzani wa Msata anapata readings Z!

Hili ninalisema kwa uhakika kwakuwa nimepata ku deal nao hao watu wa weigh briges (Tanroads). Kwahiyo transporters kutolipia hiyo variation ya 5% ilikuwa ni sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom