Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,622
- 20,568
Pili pili hoho, hasa hoho za njano ni moja ya matunda yenye Vitamin C nyingi zaidi. Ina vitamin C nyingi kuliko machungwa na malimao.
Vitamin C ni muhimu sana katika kujenga mwili na kujenga kinga ya mwili. Ukosefu wa vitamini C uliua sana mabaharia wa zamani baada ya kuwa wamekosa matunda na mboga mboga katika safari zao.
Wakati wa Covid tulihamasishwa sana kutumia malimao ili tupate vitamin C. Kumbe tulitakiwa hasa kuhamasishana kula pili pili hoho.
Mtu mwenye mafua anaweza andikiwa kutumia vidonge vya vitamin C au malimao. Lakini hoho zina faida zaidi. Kuhusu vitamin C, mapera ndiyo funga kazi. Hakuna tunda lenye vitamin C nyingi kama mapera. Yangu ni hayo tu, dada Pipi nishushe.