Pikipiki ipi ni bora zaidi?

Pikipiki ipi ni bora zaidi?

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
676
Reaction score
1,025
Wakuu nataka ninunue pikipiki kwa ajili ya matumizi binafsi, yaani usafiri binafsi nk.

Nataka ninunue pikipiki ambayo itakuwa nzuri hasa katika mazingira ninayoishi ambapo kuna barabara nyingi za vumbi na vilima/miinuko kwa wingi.

Naomba ushauri kwa wataalamu na wenye uzoefu wa pikipiki ili nijue chaguo bora kati ya hizi:-
(a). Boxer
(b). TVS
(c). Honda
(d). Kinglion
(e). Sinoray, nk

Ahsanteni kwa ushauri, 😊
 
unaumri wa kundi gani,?
Uko mazingira yapi?
Unahitaji pikipiki kwa matumizi gani?
UKIPATIA UFUMBUZI WA MASWALI HAYO NJO PM.
 
Chukua Haojue express au plus hutojutia, ni imara sana, mafuta zinanusa, nguvu kubwa inachanganya haraka sana (nyepes kwenye mwendo) na mafundi wapo wengi na used yake inauzika kwa urahis tofaut na zingine ila changamoto zake ni
1.mzito sana kama itakuzimikia sehemu labda imeisha mafuta kuikokota kwake eeeh utaomba poo
2. Tair ya nyuma nyembamba kiasi kwenye michanga inateleza sana,
3.Wanadai inabinua mukikaa mshkaki sehemu za miinuko ila hii yangu hilo sijawahi liona.
 
Tazama ni piki piki gani (Brand) nyingi katika eneo unaloishi kisha nunua hiyo. Hapo hutapata shida ya mafundi, parts na kuiuza siku ukihitaji kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom