Piga kura yako sasa: Wangapi bado wana imani na straika wa timu yetu

Piga kura yako sasa: Wangapi bado wana imani na straika wa timu yetu?


  • Total voters
    121
Nina imani naye full...tuwe tu wavumilivu kama mashabiki wa Arsenal.
 
Halafu mbona yule beki wa pembeni namba tatu wetu Bashite, inasemekana usajili wake ulikuwa haujamilika ila anacheza tu, sijui ni kanuni ipi ya FIFA imetumika kumchezesha mchezaji asiye na vibali
 
pogba ajijui tu wametumia pesa nyingi sana kumuweka pale
Pogba is doing good. Yuko sawa TU. Amebadilisha game ya manUtd.

Ball collection hapo nyuma , possessing Mpira, Mpira haupotei hovyo hapo nyuma. Ameongeza ubora wa Herera,

Si mbinafsi....Tatizo tumezoea wabinafsi. Yeye anawafanya wengine wang'are pia. Anacheza almost uwanja wore ingawa ameegemea zaidi kushoto na nyuma. Alafu kiwango cha Mpira kinaathiriwa pia na watu unaocheza nao...Angecheza na wajuaji wote, ingekua tofauti...nae angekua busy kung'ara ila Sasa anajitahidi kusaidia wenzake timu kwa ujumla
 
Striker huyu bana mzuri sema mchoyo sana hataki kutoa assist kwa wenzake. Yeye anataka atoke katikati ya uwanja hadi golini bila kupiga pas kwa wenzake utafikir anacheza peke yake uwanjani... Next mechi akae banch tusiendelee kupoteza point tatu.

Mavugo bana tumekosa jana point 3
 
Naona mechi Ndio dkk ya 85 hivi na huyu streka wetu hana dalili ya kutupia kamba, mechi bado inasoma bao 0 - 0 wasiwasi wangu anarudi sana nyuma kukaba kwa sababu namba zote anataka kucheza yeye kuna Kila dalili ya OG goli la kujifunga dkk ya 90+ na mechi itakuwa imeishia hapo
 
Natamani timu ingeendeshwa kiuchumi zaidi hapo ingekaa poa maana timu za wenzetu dah zina vitega uchumi vya kutosha tu sisi hata kuitangaza timu yetu hatuwezi, na tunaoumia zaidi ni sisi mashabiki
 
Kama hadi sasa unashundwa kufanya analysis mwaka mzims na miezi kadhaa?? Basi kuna haja ya kubadili mitaala yetu ya elimu

Boss Kkimondoa, unaweza kuwa sawa au sio sawa, ila acha nikupe mifano miwili, Hope utanielewa.

Mfano wa Kwanza ni Mwanaume unapompa Mwanamke mimba, kuna Miezi 9 ya kusubiri uitwe Baba.

Mfano wa Pili, Mkulima anapopanda Mbegu, kuna muda wa kusubiri mpaka mavuno yaje.

Maana ya mifano yangu, kuna kipindi cha Kusubiri ili kujua hatima ya jambo husika.

Hope umenielewa.
 
Bavicha bado mnasafari ndefu sana, kura za mitandaoni ndo zilimfanya rais wa mioyo yenu akajua kuwa atapewa nchi, kumbuka wafuasi wa ccm wengi wao hawapo mitandaoni, endeleen kujidanganya na kura zenu za mitandaon,2020 tutawapiga kipigo cha PAKA SHUME
Mbona unatuhamisha kwenye mada hatuko kwenye vyama
 
Bench La Ufundi Lifumuliwe List Ipangwe Upya Wachezaji Hawajitumi Kapten Mwenyewe Kachoka Hoi
 
Bado mapema mno kumhukumu,nchi ilikuwa na matatizo mengi kuliko mnavyodhani, kusajili wachezaji wapya hadi wazoeane, kubadili mila potofu iliyokuwa imeingizwa kwa watanzania kumuona mwizi kama mjanja na mwaminifu kama adui na mjinga, inataka mda si ishu ya mwaka tu wabongo wenzangu
 
Hongera sana serikali ya Magufuli kwa kazi tukufu kwa watanzania



Mada hii inajadili uwezo wa straika wa timu yetu aliyesajiliwa kwa mbwembwe huku mashabiki wakihongwa kofia,kanga,t-shirt,chumvi na kila aina ya uchafu unaokiuka masharti ya usajili ili wamshangilie,sasa huyo Rais wako anaingiaje katika mada hii?Au unataka mleta mada aokotwe kwenye sandarusi kule Ruvu chini?

Straika huyu hana tofauti na Jama Mba wa Yanga au yule wa Simba aliyenaswa na hirizi kiunoni aliyokuwa anaitumia kumuwezesha "kunyumbulika" mithiri ya kambale uwanjani.Hana lolote zaidi ya kupambwa kwenye magazeti na runinga kuwa ni mshambulizi hatari kumbe hata goli lililoipa ushindi timu yake alilifunga kwa mkono!

Alipogundua kuwa uwezo wake wa "kuzifumania nyavu"ni mdogo,aliamua kuisimamisha ligi hadi 2020 ili asipate mikikimikiki ya mabeki mahiri walioapa kwenda naye " bampa 2 bampa",aliogopa "kulaliwa mbele" na wenzake akakimbilia kusimamisha ligi.
 
Sasa timu pinzani fanyeni hata mpango wa kuvunja jàpo kamguu kake ili akae benchi tutafute striker mwengine.
 
Back
Top Bottom