PICHA: Ziara ya Kinana Mtwara yafana

Mimi nafikiri wapewe muda kwani naona Safu yao ni makini sana kwani Mwenyekiti ni Lt Col (Rtd) Kikwete na Katibu wake ni Col (Rtd) Abdul rahman Kinana. sasa tungojeee kwata lake.


Kila la kheir
 
Kuamka ndio kushabikia CDM? Haya hao wa arusha na moshi wameamka kwenye nini?

wameamka kimaendelea jiulize mtwara imeunganishwa lini na dar kwa lami na Arusha/Moshi zimeunganishwa lini utapata jawabu
 
Nakubariana kabisa na Things fall apart,mie nilikuwepo kwenye mkutanoo
1.Amepanda Wazili Engeneer Chizza kuhusu Korosho kazomewa maana alikuwa haeleweki na wananchi wakaomba wamwulize maswali hakujibu.Kinana aliruhusu watu waulize maswali ,yalipoulizwa akasema hawezi kujibu maswali magumu kwa majibu mepesi
2.Alipanda Waziri Ghasia alizomewa sana mpaka Nape akapanda na kumsaidia mawili matatu.
3.Alipopanda Waziri Mwandry ndiyo akaharibu kabisa anazungumza habari ya Madawati wakati watu hawajauza hata Korosho?,we uliona wapi Serikali inamkopa Mkulima Korosho kilo 50 imlipe kwa awamu?.

Mkutano ulipokwisha nilimsikia Mama Mmoja mwenye sare za CCM akisema namnukuu "WAALWAHIII CCM INAKUFA KABISA MTWARA" mwisho wa kumnukuu.
Wananchiwengi baada ya kuisha Mkutano walikaa kwenye vikundi vidogo vidogo na kujadiriana mawilimatatu ,wengi wao walikuwa wanalalamika sana kwa CCM kuwaona watu wa Mtwara kama wasio na AKILI na kuamua kuja kuanzia Mkutano wao huku kama NGOME yao,basi kuanzia sasa wajue chama cha CCM Mtwara hakina nafasi tena.
 
Mimi nafikiri wapewe muda kwani naona Safu yao ni makini sana kwani Mwenyekiti ni Lt Col (Rtd) Kikwete na Katibu wake ni Col (Rtd) Abdul rahman Kinana. sasa tungojeee kwata lake.


Kila la kheir


Kwani hii Nchi iko vitani?
 
basi bwana nikiwa mtaa wa coco bichi (mtwara) nikiwa kwenye pikipiki (bodaboda) nikamuuliza kijana alienipakiza kwa nini hujaenda kwenye kuwapokea viongozi wa ccm kama wenzio maana vijana wengi wenye pikipiki wamekodiwa kwenye maandamano ya kuwapokea kina kinana, kijana akajibu huku akimaanisha koko bichi na maeneo ya karibu wanatujua hatuwataki na na kama huamini lile shina lao na hapa koko bichi tumelivunja tumeweka bedera ya chadema na ni kweli lile eneo sasa ni chadema ccm haina wafuasi pale. na kweli leo vijana wamevuna mafuta ya bure kutoka ccm!!!

Sio huko Koko Beach pekee,Nakupa taarifa tu Mtwara Mjini pote CCM haifiki kata Railway kufanya kitu chochote ,mpaka Diwani wa CCM hashaambiwa kuwa hana kazi pale tena.HATUMTAKI .Kuna kijana wetu tunae kwa tikiti ya CHADEMA tunamuandaa pale.Kwa taarifa tu hii Kata ndiyo iliyobeba karibu kila kitu kwa maendelea ya Mtwara ,Viwanda,Bandari ,Gas plant,Huko Bandarini ndiyo kuna Maabara kubwa ya Mafuta,kwa hili CCM wajipange sanaa.M bunge Mulji analijua hili na hakanyagi Railways,nenda kamuulize kama ashawahi fika.
 
NImetoka ss hivi katika mkutano wa CCM nimegundua CCM bila nape hali itakua ngumu'swala la korosho na gesi ni gumu kwa serikali ya chama changu cha CCM,wananchi wa kusini tunauliza kwanini gesi ipelekwe KINYEREZI,GHASIA kajiuma umauma mpaka Nape kaja kumuokoa.kazomea mpaka amepaniki,wanakusini wanataka kujua kwanini huo mtambo uliojengwa KINYEREZI USIJENGWE MTWARA

Safi sana,na bado
 
Kama kawaida ya magamba kutoa bure kofia,tisheti na kanga.Hivi hii tabia mtaacha lini?

Tatizo liko kwa wanaopokea hizo khanga na kofia, hao ndio wanatakiwa kulinda utu na heshima zao lakini cha kushangaza ndio wanatangulia kuupuuza utu wao na kujidharau wenyewe! hawa ndio tuwaulize, tabia hii ya kupokea khanga na kofia mtaiacha lini?
 
Mimi nafikiri wapewe muda kwani naona Safu yao ni makini sana kwani Mwenyekiti ni Lt Col (Rtd) Kikwete na Katibu wake ni Col (Rtd) Abdul rahman Kinana. sasa tungojeee kwata lake.


Kila la kheir

Bwanyenye wewe kwa kupenda vitu vinavyoua nchi yetu..hujambo.We si ukae huko kwenu tuu, sisi hatuna tena wala tende wenye maana nchi hii.Wote wamechoka wamebaki kuwa uamsho tuu.
 
Back
Top Bottom