Picha za kwanza za shimo jeusi angani zatolewa

Picha za kwanza za shimo jeusi angani zatolewa

Haya mashimo (au Black Holes) huwa yapo angani.Yapo kadhaa angani na kwa ukubwa mbalimbali hata kufikia ukubwa wa uwanja wa mpira.Wameandika kwenye hii makala kuwa,ipo kwenye sayari fulani.Hii ni makosa kabisa.Hakuna sayari inayoweza kuwa na kitu hichi kwani,kwanza,kwa hii iliyopigwa picha,ni kubwa sana ukilinganisha si tu na sayari (ambazo ni ndogo sana ukilinganisha na hili dubwana),hata na nyota yoyote(jua letu ni mojawapo ya nyota,ila ambayo ni ndogo sana tu licha ya kuwa na ukubwa wa almost 98% zaidi ya mkusanyiko wa sayari zetu 8 pamoja na ghasia zote kwenye eneo linaloitwa solar system).Pili,achilia mbali sayari,hata nyota ambazo ni kubwa sana ukilinganisha na kanyota ketu kanakoitwa Jua,yakikaribia eneo hatari la black hole,zinamezwa na kutokomea kwa kasi ya ajabu...
Black holes zipi unazungumzia ambazo zina ukubwa wa uwanja wa mpira!!!

Aliponichanganya namimi ni kwamba upana wake ni km 40bln halafu umbali wake umepimwa ni kama km 500ml.kiuhalisia hapa blackhole ni kubwa sana kuliko galaxy yetu kiasi kwamba ilitakiwa itufunike,tusiionee kwa mbali.

Fikiria kilimanjaro ingekuwa ndefu, kuliko umbali wa kutoka hapa mpaka mkoani moshi.
 
Kuna uwezekano siku moja dunia ikaingia kwenye kumi na nane za hilo dubwana so itavutwa na kupotelea humo na ndo ukawa mwisho wa dunia
So be prepared mda wote kwa muomba mungu wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Not only dunia, yani mfumo wetu wa jua ukijichanganya kukaribiana tu na hilo dubwana sayari zote pamoja na kajua ketu vinamezwa...
 
Black holes zipi unazungumzia ambazo zina ukubwa wa uwanja wa mpira!!!

Aliponichanganya namimi ni kwamba upana wake ni km 40bln halafu umbali wake umepimwa ni kama km 500ml.kiuhalisia hapa blackhole ni kubwa sana kuliko galaxy yetu kiasi kwamba ilitakiwa itufunike,tusiionee kwa mbali.

Fikiria kilimanjaro ingekuwa ndefu, kuliko umbali wa kutoka hapa mpaka mkoani moshi.
Huo umbali hata mie nimeshangaa labla alimaanisha 500 million km lightyears...
 
Aliponichanganya namimi ni kwamba upana wake ni km 40bln halafu umbali wake umepimwa ni kama km 500ml
Hapa umeongelea hii moja tu.Na haijasemwa popote kuwa black hole ni moja tu na yenye ukubwa huo huo tu au inayoendana na ukubwa huo huo tu.Tambua tu kuwa,black holes zingine zilijikuta zimekaribiana,kuvutana na kuishia kuungana na kuongeza ukubwa.

Ni kuwa,black holes zimezagaa sehemu tofauti angani (na kwenye galaxy tofauti),zenye ukubwa tofauti,na hata zilizo ndogo kama kiwanja cha mpira au ndogo zaidi ya hapo.Ila,udogo huo usikudanganye kwani,ukubwa wa madhara yake huwezi kuudhania na hauendani na ukubwa wake.

Hiyo Black hole inayoeelezwa hapa,ipo katikati ya galaxy yetu (roughly,ni kama bleda ya mpiara inavyokaa ndani ya mpira wa ngozi,gozi la nje ndilo liwakilishe utitiri wa hizi nyota na bleda ndio iwe hiyo black hole.Ila si kuwa ndio imekaribiana sana kama ilivyo bleda na gozi la mpira;nia ni jue tu ilivyokaa.Na pia,si kuwa katika mjumuiko huo zimekaa kwa umbo la mduara kamili kama mpira)).Hilo black hole limezungukwa na hizi vyota,vumbi zito na gesi kibao n.k. (ndio sababu si rahisi sana kuliona,licha ya umbali wake kuchangia pia).

Hivyo,hiyo black hole si kubwa zaidi ya galaxy kwani,imo ndani ya eneo la ujazo unaoitwa galaxy.Kusemwa kuwa ni kubwa,ni kweli ni kubwa mno,hata akili kuichanganua ni shughuli,ila kwa namba tu labda.lakini,sio kubwa zaidi ya galaxy.Galaxy ni kubwa zaidi.Labda (sina hakika) inaweza kumeza galaxy ndogo zaidi kwa ukubwa (kama zipo),
 
Back
Top Bottom