Shimo Jeusi angani: Kundi la wanasayansi kuchunguza vitendo vyake

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,452
6,934
1572593150070.png

Filamu inayotarajiwa ya shimo jeusi itaanza kutazamwa hivi karibuni.

Kundi moja lililopiga picha za kwanza za shimo jeusi lililopo angani limetangaza mipango ya kuchukua video yenye uasili wa shimo hilo lililopo katikati ya anga

Setlaiti itazinduliwa kusaidia mfumo wa darubini nane zitakazotumika kuchukua filamu hiyo.

Watafiti wanasema kuwa uimarikaji wa mfumo huo utawezesha kuona jinsi shimo hilo linavyovuta na kuingiza ndani vilivyopo karibu yake.

Kundi hilo tayari limetuzwa tuzo ya ufanisi huo. Profesa Heino falcke , kutoka chuo kikuu cha Raboud nchini Uholanzi ambaye alipendekeza wazo hilo la darubini hizo aliambia BBC kwamba hatua ya pili ni kuona vitendo vya shimo hilo.

Kama vile sayari , shimo jeusi pia huzunguka . Na kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuharibu anga na wakati wake na kuona kitendo hiki cha kushangaza cha anga kuzungushwa ni miongoni mwa maajabu ya elimu ya angani.


1572593186639.png

Profesa Heino Falcke: Mradi wa shimo jeusi ni pendekezo lake

La kushangaza zaidi ni hatua ya kuchukua picha za rangi ya kitu ambacho uwezo wake ni mkubwa sana hali ya kwamba hata mwangaza hauwezi kuepuka.

Mapema mwaka huu kundi hilo lilichapisha picha za shimo kubwa jeusi lililokuwa katika sayari moja iliokuwepo umbali wa kilomita bilioni 40 - ikiwa ni mara tatu zaidi ya ukubwa wa dunia.

Picha hiyo inaonyesha gesi ya moto ikianguka katika shimo hilo katika rangi tofauti za machungwa.


1572593265198.png

Dkt Katie Bouman ni miongoni mwa wanasayansi waliohusika pakubwa katika mradi huo

Ukweli ni kwamba shimo jeusi halina rangi. Lakini kile ambacho wataalam wa angani wanaona ni vile vitu vinavyoingia ndani yake na kubadilika kua gesi ya moto.

Gesi hiyo inaonekana kubadilika rangi inapokaribia shimo hilo jeusi.

Kama jua linapokuwa nyuma ya mawingu jioni , mwanga kutoka kwa vitu hivyo vilivyobadilika na kuwa gesi moto unalazimika kusafiri kupitia gesi zaidi kuelekea duniani.

Hivyobasi athari yake itakuwa kubadili rangi na umbo la vitu hivyo karibu na shimo hilo.

Kundi hilo la wataalam linataraji kuongeza darubini katika eneo la Greenland, Ufaransa na maneo kadhaa ya bara Afrika na tayari limewasilisha ufadhili kutoka kwa wakfu wa wanasayansi wa kitaifa nchini Marekani NSF kutuma setlaiti tatu ndogo angani ili kusaidia uchunguzi huo utakaofanyika kutoka ardhini.

Kulingana na Profesa Falcke, hatua hiyo itasaidia kujenga darubini kubwa yenye ukubwa zaidi ya dunia , itakayoweza kuchukua picha asili ya shimo hilo lililopo katikati ya sayari.


1572593086321.png

Jinsi darubini hizo zitakavyochukua picha hiyo ya shimo jeusi

Profesa Falcke aliambia BBC News kuhusu mpango wa kundi hilo kwa jina EHT huku kundi hilo lenye wanasayansi 347 likipokea $3m (£2.48m) kama tuzo kufuatia ufanisi wao.

Ijapokuwa ni yeye aliyependekeza wazo hilo na kupigania kupata ufadhili amesema kwamba tuzo hiyo inatambua juhudi zilizofanywa na kundi lote la wanasayansi hao.

Kundi hilo linashirikisha wanasayansi kutoka Ulaya, Chiina, Afrika Kusini, Japan na Taiwan.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom