Picha za kwanza za shimo jeusi angani zatolewa

Picha za kwanza za shimo jeusi angani zatolewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,609
Shimo jeusi
Haki miliki ya pichaEHT COLLABORATIONImage caption

Picha ya kwanza ya shimo jeusi . limezungukwa na gesi inayovutwa ndani na shimo hilo
Wanaanga wamefanikiwa kuchukua picha za kwanza kuhusu shimo jeusi ambalo linapatikana katika sayari ilio mbali.

Shimo hilo lina ukubwa wa kilomita bilioni 40 kwa upana ikiwa ni mara milioni 3 zaidi ya dunia na limetajwa na wanasayansi kuwa 'dubwana'.

Shimo hilo jeusi lipo umbali wa kilomita milioni 500 na lilipigwa picha na jumla ya darubini nane kote duniani

Maelezo yamechapishwa katika jarida la wananaga la Astrophysical .
Picha za shimo jeusi
Haki miliki ya pichaDR JEAN LORRE/SCIENCE PHOTO LIBRARY

Profesa heino Falcke wa chuo kikuu cha radboud nchini Uholanzi , ambaye alipenedekeza jaribio hilo, alimbia BBC kwamba shimo hilo lilipatikana katika sayari kwa jina M87.

Kile tunachokiuna ni kikubwa zaidi ya mfumo wote wa jua, alisema.
Jinsi picha hizo zilivyopigwa

Shimo hilpo lina uzito mara bilioni 6.5 zaidi ya Jua. na ni mojwawapo ya mashimo meusi ambayo tunadhani yapo. Ni dubwana kwa kweli, likiwa ndio shimo lenye uzito mkubwa zaidi ya yote ulimwenguni.
 
Albert Eistein alikuwa na akili sana, alishazungumzia hii kitu miaka mingi iliyopita.
Kwel nimeamin kizaz kilichopita kilikuwa kizaz cha Magenius waliopitiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo alisema hilo shimo liko kwenye nini,hewani,kwenye sayari nyingine au....?
 
Kwahiyo alisema hilo shimo liko kwenye nini,hewani,kwenye sayari nyingine au....?
Haya mashimo (au Black Holes) huwa yapo angani.Yapo kadhaa angani na kwa ukubwa mbalimbali hata kufikia ukubwa wa uwanja wa mpira.Wameandika kwenye hii makala kuwa,ipo kwenye sayari fulani.Hii ni makosa kabisa.Hakuna sayari inayoweza kuwa na kitu hichi kwani,kwanza,kwa hii iliyopigwa picha,ni kubwa sana ukilinganisha si tu na sayari (ambazo ni ndogo sana ukilinganisha na hili dubwana),hata na nyota yoyote(jua letu ni mojawapo ya nyota,ila ambayo ni ndogo sana tu licha ya kuwa na ukubwa wa almost 98% zaidi ya mkusanyiko wa sayari zetu 8 pamoja na ghasia zote kwenye eneo linaloitwa solar system).Pili,achilia mbali sayari,hata nyota ambazo ni kubwa sana ukilinganisha na kanyota ketu kanakoitwa Jua,yakikaribia eneo hatari la black hole,zinamezwa na kutokomea kwa kasi ya ajabu...
 
Back
Top Bottom