Picha za Green Guard, Red Brigade na Blue Guard

Picha za Green Guard, Red Brigade na Blue Guard

DSCN6076_thumb%25255B2%25255D.jpg
 
....HAYA YOTE NI MATOKEO YA udhaifu wa vyombo vyetu vya usalama,hususan polisi kuonyesha waziwazi kuwa wanafuata maagizo ya mwigulu. jwtz wanawabinya wanamtwara,ni wakati muafaka wa kutafakari na kuchukua hatua za kujilinda...
 
Mkuu Azimio Jipya naona umekasirika mpaka umesahau ku-edit ulichoandika.... Nimekuelewa. Hizi bluu nilizopaka ndio ulichokisema kwa uchungu nami nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa. Kimsingi Civil War ya Tanzania inatengenezwa na wanaofikiri watabaki salama kwa civil war hiyo. Kwa mfano, salamu za Red Guard na Blue Guard ilikuwa ni kujibu Green Guard. Hivyo, huhitaji kuumiza sana kichwa kuelewa ni kwa nini Green Guard haikemewi na watawala wakati inatumika kuumiza watu. Matokeo yake ndio haya, na reaction ya serikali imekuwa kama ulivyoandika.

Binafsi sifurahii hali ya uvunjifu wa amani, kinachotokea Tanzania ni watu kutumia fikra zao ili kuendelea kuhifadhi amani yao. Pengine ndio inabidi tujadili hii namna mpya ya kujilinda kuanzia sababu zilizotufikisha hapa, matokeo yake na namna gani tutarejea kwenye misingi yetu mizuri tuliyoipoteza kutokana na uongozi wa serikali kama ulivyoelezea.

Ingawa Mimi sio mwana historia!

Nafikiri kuna njia kuu mbili tu za kutufanya tuweze kurudi kwenye mstari inayoendena na hekima na sifa za kibinadamu. Njia moja imeegemea historia.

1. Kwa kuona kinachoendelea tunaweza kutumia akili na utashi wetu tukajielimisha ili tuelimke na kujirudi kwani tutapata maarifa ya kutosha kuona na kujua fika kuwa tukiendelea hivi tunavyoendea tutafikia mwisho mbaya usio na tija kwa wote.

2. Bahati mbaya tukishindwa kutumia uwezo wetu kama binadamu tuliokamilika na tunaotofautiana na tumbili wa manyara,.. tukashindwa kutumia maarifa na elimu kuepusha majanga ya kibinaadamu yanayoweza kufutaia kama hatutabadilika haraka, historia inaoyesha kuwa hapatakuwa na namna nyingine ila kudumbukia kwenye majanga kama vita vya wenyewe kwa wenyewe au majanga mengine ... hii ikiwa ni mbadala wa elimu tuliyoitupilia mbali na kugoma kubadilika mapema.

Nafikiri hapa tulipo si pabaya kama tukitaka kuepuka hatua hiyo ya pili!-
 
Hii watakanusha na kusema ni waasi wa Congo


mkuu hii si tanzania... naona wadau washadakia ni CCM , hebu angalia hizo kofia CCM ilitakiwa kuwe na lable hii
images

Wewe njiwa vipi? ... Sasa unataka kubisha nini? .. Kwani nembo zao huzijui? .... ... haya angalia na fananisha Nembo za Kofia hizi hapa chini.

chipukizi.JPG

KATIBU wa Siasa na Uenezi wa mkoa wa Morogoro (TANZANIA), Kulwa Milonge, akimpongeza Gabriel Amos baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi wa CCM Taifa katika uchaguzi uliofanyika juzi, Chuo cha Ualimu Morogoro. Gabriel ni mtoto wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Makalla. (Picha na Latifa Ganzel).
attachment.php


images


113.jpg
 
VURUGU+CCM.jpg




CCM+TABORA.3.jpg


Askari polisi Tabora akimwangalia kwa hasira baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa ni Green Guard ambao walikuwa wakimsulubu kijana huyo anayedaiwa kuwa ni wa Chadema katika vurugu zilizojitokeza baada ya zomeazomea wakati wa mkutano wa CCM Tabora.
 
Back
Top Bottom