Picha za Green Guard, Red Brigade na Blue Guard

Picha za Green Guard, Red Brigade na Blue Guard

Mkuu EMT, kwa picha hizi japo zipo kwa uchache...nina kila sababu ya kuamini Rais wetu na Mamlaka zake wamekurupuka kutoa hizo "Marufuku" walizozitoa.

Hivyo hilo linanifanya nitilie mashaka uwezo wa utendaji wa Rais wetu...

Nahisi CDM wamefanya makusudi kuropoka waliyoyasema ili wengine waingie kichwa kichwa. Na kwa hili wamefanikiwa.
 
lema.jpg
 
Huenda mkuu...

"Siasa ni mchezo mchafu" - Yusuph Makamba

Nahisi CDM wamefanya makusudi kuropoka waliyoyasema ili wengine waingie kichwa kichwa. Na kwa hili wamefanikiwa.
 
Kwa ufupi ni kwamba tamko la CHADEMA litakuwa ama chanzo cha kufungwa kwa biashara hii ya kuwatumia vijana na watoto ndivyo sivyo, au si ajabu ukawa ndio mwanzo wa 'kuviimarisha' kabisa vikosi hivi, maana vyama vitaanza kushindana nani ana jeshi kali zaidi.

Pengine pia tumepeta hoja ya nyongeza kwenye ibara ya katiba mpya inayohusu vyama vya siasa. Iwe "marufuku kwa vyama vya siasa kuonesha kusudio la kuanzisha, au kuazisha jeshi au kikundi chochote chenye kufanana kwa namna yoyote ile na jeshi"
 
Back
Top Bottom