Picha: Yaliyojiri Dar na kwingineko Oktoba 19, 2012

DSC_3231.JPG


Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo mchana.
 
hawakupewa juicy?

Halafu watanzania wa ajabu sana.....

Miguuni umevaa ndala, badala ya kwenda kutafuta uondokane na ndala, unajiunga kufanya upuuzi.....kumnufaisha mwengine
 
..halafu wamebeba chupa za maji tayari kwa kujikinga na mabomu ya machozi.

..but this is very SAD. hivi kweli watu wazima wameshindwa kukaa chini na kutumia BUSARA kumaliza matatizo haya.
 
Muulize Kova na askari wake bettles la Msimbazi na Kidogo Chekundu Polisi wote walikimbia na kwenda kuomba msaada kutoka JWTZ unadhani maandamano ya Chadema hayo FFU wawili wanasambaza uwanja mzima, watu wamefika mpaka Ikulu kama wangekuwa na nia ya kulipua saizi tungeongea mengine
mmesikia presdaa anarudi leo ndo maana mnang'ang'ania kwenda ikulu mkagaiwe tende na pilau za oman ahahahaaaaaaaa
 



Ona sasa hawa jamaa wamevaa mavazi meupe mazuri, mavazi kama haya yangewakilisha amani na upendo.

Cha ajabu wako chini ya ulinzi nini maana yake? utasikia wanasema wameonewa na kunyanyaswa wanafata nini ikulu???

IKULU NI MAHALA PATAKATIFU - JK Nyerere (huendi kufanya fujo kule, nikutafuta matatizo na wameyapata!)​
 
Tuandamane kukusanya michango ya kujenga shule ili watoto wenu tukasome na kuondoa ujinga badala ya kuandamana kwa upuuuuuuuuuuuuuzzzzzzzzzzzi, tumekosa elimu tuuuuuuuuuuuuuuuuu na mengineyo ni kisingizio.
Huyo jamaa ingawa ni jamaa yangu, shule hana ndiyo yupo hivo............ Hivyooooooooooooo.
 
Ndugu yangu usiwe Tomaso
Mi nipo kariakoo kwa ndugu yangu. Umejifungia ndani vurugu zimekolea ni risasi na mabomu ya machozi. Soko lilifungwa tangu saa 7 na watu wote wanalazimishwa kutawanyika kurudi makwao.
Kumetokea fujo kubwa mitaa ya Msimbazi,Congo,Mkunguni,Mafia na Nyamwezi ndio maeneo nilipo japo sijaweza kuchungulia muda mrefu kwa ajili ya mabomu.
Hofu mnazozidi kutupa hazionekani kwenye picha.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Pix-8.JPG


Askari wa jiji nao wakishiriki katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo
 
Dah kweli wakati vijana wa kikristo wanakazia maarifa darasani, wale wa kiislam wako maandamanoni!! Mtihani wa taifa ukifika matokeo yakitoka mnasema mnaonewa!! Wakishafeli basi maisha hawana ni kuvaa ndala za chooni!!! Siku hizi hata ndala haziingii chooni!!! Uchafu mtupu!! Leo Taifa litahutubiwa au ni kapa? Tusubiri!!
 
Asante kwa picha

lakini naona ni askari tu, hao waandamanaji wachache, Humu jamvini tunavyoaminishwa kwamba kuna fujo sana, lakini sioni kwenye picha hizi.

A picture speaks louder than words.
 
"Tumefika hapa kutokana na UDHAIFU wa Rais Jakaya Kikwete.." J.J. Mnyika, Bungeni,June,2012.

Najikuta nikitafakari hii kauli japo siku za nyuma sikuwa nimeitilia maanani.
 
Ya Mbagala Na Bedui Aliyekojoa
Msikitini... Ndugu zangu, Moja ya hadithi za Mtume Muhammad
S.A. W ni pale Mtume Muhammad
alipokuwa msikitini na maswahaba
wake. Mara akaingia msikitini mtu wa
kabila la Mabedui na kuanza kukojoa.
Maswahaba wa Mtume wakasimama kwa hamaki kutaka kumwadhibu Bedui
yule. Mtume akawasihi maswahaba wake
wasifanye jambo lolote litakalomdhuru
Bedui yule. Hapo ikavutwa subira. Bedui
yule akakojoa na akamaliza. Mtume
Muhammad alipomuhoji Bedui yule
ikabainika kuwa alikuwa ni mtu wa hovyo na wala hakujua kuwa
alimokuwa ni msikitini. Bedui yule
akaelimishwa, akaelewa. Akarudi
kwenye ustaarabu. Ndio mkojo ule ulifutwa kwa maji na
amani ikawepo. Wahenga walinena;
Subira yavuta heri. Siku zote, hamaki si
jambo jema. Kwa kutanguliza subira na
kutumia hekima Mtume Muhammad
aliivuta heri na kuepusha shari. Maana, kama Mtume alisingewaasa
maswahaba wake kuvuta subira, basi,
makubwa matatu yangetokea ndani ya
msikiti ule; Mosi, zingezuka vurugu na
watu kuumizana na hata kutoana roho.
Pili, mkojo wa Bedui yule ungesambaa msikitini kwa vile alishaanza kukojoa na
isingekuwa rahisi kwake kukatisha
mkojo wake. Tatu, Mkojo una madhara
ya kiafya pia. Naam, kwa mwanadamu, ni muhimu
kuwa na subra na kutafakari kabla ya
kufanya maamuzi. Kwa ndugu zangu
Waislamu, tunaona Mtume Muhammad
ameweza kuonyesha hilo. Na kwa ndugu
zangu Wakristo, kuna mifano pia ya Yesu Kristo kuonyesha subra. Ndio, Uislamu, kama ilivyo kwa Ukristo
na dini nyingi za humu duniani, msingi
wake ni amani na upendo. Kitendo cha
mtoto yule wa Mbagala kukojolea korani
kitazamwe kwa sura ya kitendo
kilichofanywa na mtoto . Na kama ilivyokuwa kwa Bedui yule,
kama pale Mbagala subira na hekima
vingetangulizwa, basi, yumkini
tungebaini kuwa mtoto yule hakujua
madhara ya kitendo chake. Naye
angekanywa kama tuwakanyavyo watoto wetu. Na hata kitendo hicho
kingefanywa na mtu mzima, bado
tulikuwa na haja ya kutanguliza subira
na hekima kumhoji aliyetenda, yaweza
akawa kama Bedui yule kwenye msikiti
alimosali Mtume na maswahaba wake. Na kwa kuangalia picha zile za Mbagala
naiona hatari iliyopo sasa, kuwa tuna
vijana wengi wasio na kazi; Wakristo
kwa Waislamu. Vijana wasio na dogo. Ni
kama moto uliofifia. Akipatikana kwa
kuchochea kuni wanalipuka. Ni vijana wanaopatikana wakati
wowote na mahali popote. Hata jambo
likianza saa tatu asubuhi wao wapo.
Hawana ofisi wala bosi wa kumwomba
ruhusa ya kwenda kuandamana na
kurusha mawe. Ndio hawa wanaonekana wamevaa ' Kata kiuno' na
wengi wao hawajahi hata kuingia
misikitini au makanisani. Inakuawaje kijana wa kweli wa Kiislamu
achome kanisa na kuiba kompyuta.
Inakuawaje kijana na muumini wa kweli
wa Kiislamu aonekane saa mchana wa
jua kali akivamia baa na kukimbia na
kreti za bia? Ni maswali yanayotutaka tutafakari kwa makini. Maana, ninavyoamini mimi, uchumi na
elimu duni ndio hasa vinavyochochea
vurugu za kijamii, iwe za kidini au
kisiasa, na hususan inapohusisha vijana.
Vijana wetu hawana misingi mizuri ya
elimu, na wengi hawana ajira pia. Haya ni sawa na makombora yasiyo na
gharama kubwa kuweza kutumiwa na
wanasiasa wasio waadilifu na hata
viongozi wa kidini wenye mitazamo
mikali. Ni makombora yaliyoanza
kutulipukia. Tuliziona ishara, tukazipuuzia. Leo Kuna vijana watakaotumiwa au
kutumia fursa hiyo kutenda maovu kwa
kisingizio cha dini. Ni hawa wataoshiriki
kuchafua taswira za dini husika pia.
Tujiadhari, kabla ya hatari kubwa
inayotujia. Hatujachelewa. Na hilo ni Neno La Leo. Maggid Mjengwa, Iringa. 0788 111 765
 
Asante kwa picha

lakini naona ni askari tu, hao waandamanaji wachache, Humu jamvini tunavyoaminishwa kwamba kuna fujo sana, lakini sioni kwenye picha hizi.

Kuwe na fujo kusiwe na fujo ni afadhali leo hao wanajeshi angalau wameruhusiwa kwenda kuvuta oxygen uraiani kwa kushirikiana na polisi... siku zote falsafa yangu ni kuwafanya wanajeshi wawe productive kuliko kuwaweka makambini huku wakila na kunywa fedha za walipa kodi... nimefurahi sana kuziona picha zao maana kaka zangu polisi wanaoneka kuelemewa na zege la machafuko kila kona ndo maana wao ni kufyatua fyatua tu mabomu ya machozi bila mpangilio na kuwauwa wasio na hatia...

Natumaini zoezi hili la wanajeshi litakuwa endelevu na sio zima moto ...Inafaa pia tuweke sheria kwamba wanaopatikana na makosa ya kuandamana wapewe pia adhabu ya kuwaomba msamaha directly kwa wale wote waliovunjiwa au kuhalibiwa mali zao na pia waamrishwe kulipwa fidia either collectively au individually ili dhana ya maandano ya amani iweze kutawala bila kuathiri shughuli nyimgine za watu kujipatia ridhiki zao na katika kusukuma kurudumu la ujemzi wa taifa kiujumla...

kila siku wakiitisha maandano au kutishoa maandamano ni hofu kila kona.. mambo gani haya bwana.. kila mtu ana uhuri wake wa kufanya mambo kwa kuzingatia na bila kuvunja sheria za nchi na uhuru wa watu wengine.. hii ndio basic human right ya kila mtu...
 
Back
Top Bottom