GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Maeneo mengi ya Dar es Salaam sasa yametawaliwa na machine za kukanda chapati na majiko ya kukaanga mihogo pembezoni mwa barabara hasa mida ya jioni
Na kuna wengine wanakaanga mihogo chini ya nguzo za umeme hasa maeneo ya kariakoo na Posta
Zamani ilikuwa ukiona watu wamekaa mzunguko unajua ni wale wala pweza ,Lakini sasa watu wanakula chapati na mihogo ya kukaanga hasa mida ya jioni
Vituo hivi vimefumuka kwa kasi sana ambayo inaleta shaka juu ya pato na maisha ya watu
Lengo la huu uzi ni kuangalia kwanini wanatumia sponji kukaanga zile chapati,Unakuta kile kigodoro kinapungua siku hadi siku ,Je si kinaishia kwenye chapati
Pia wakaanga mihogo wanafunika mihogo kwa kutumia nailoni na maboksi wakati wa kupika,Hii si ni hatari kwa afya?
Mamlaka za Afya hazioni hili ni janga kubwa kutumia sponji kukaanga chapati au kutumia nailoni na maboksi wakati wa kupika mihogo? Au chapati na mihogo ndio maendeleo yenyewe ya kiuchumi ndani ya Dar es Salaam?