Picha: Yaliyojiri Dar na kwingineko Oktoba 19, 2012

Published on 19 Oct 2012 by ITV TANZANIAJeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam kutawanya makundi ya Waislam

 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
  • Msafara wa Rais Jakaya Kikwete washuhudia live jamaa wakila kichapo mbele ya Ikulu wakati Rais akiwasili toka ziarani Oman
  • mifuko ya nailoni yatumika kuficha kanzu ili kufika Ikulu
TAZAMA VIDEO HII

 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Kitendo cha serikali kuleta JWTZ kwenye hili kinaonyesha ni jinsi gani watawala wanaaza kuzidiwa na nguvu za matukio, hizi ni dalili tosha kwamba tunaelekea kwenye vita kamili. Nina wasiwasi na nia, uwezo na ujasiri wa serikali kuwathibiti hawa wanaojiita waislamu. Tatizo ni kwamba hii ni hali ambayo watawala waliiruhusu na kuilea ikakua na sasa imekomaa, ina maana serikali haikujua matokea ya kulea hayo? Busara zisipotumika tutaenda mbali zaidi ya kutuliza vurugu.
 
.... several international news sources are reporting heavy fighting in dar es salaam between muslims and army. can someone update us in dar please

Licha ya polisi kuweka ulinzi mkali katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam kuwadhibiti watu wanaodhaniwa ni Waumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa na nia ya kufanya maandamano kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza kuachiliwa huru wenzao wanaoshikiliwa na polisi baadhi yao wamefanikiwa kupenya hadi katika maeneo ya Ikulu japo wameishia mikononi mwa polisi waliokuwa wamezunguka kona zote za makazi hayo ya raisi


Source: ITV TANZANIA youtube
 
Last edited by a moderator:

What are saying?

attachment.php

Jeshi lilokosa kazi ilo!! Kalindeni mipaka na malawi sio mnatumia vibaya kodi zetu. Wanadhani nguvu ya umma ikiamua watasaidia kitu hao? Check nchi mfano wa Egypt,tunisia etc. Wapuuzi sna hao
 
Asante kwa picha

lakini naona ni askari tu, hao waandamanaji wachache, Humu jamvini tunavyoaminishwa kwamba kuna fujo sana, lakini sioni kwenye picha hizi.

Inawezekana wapiga picha wanaogopa kukaribia kwenye vishindo. Usisahau FFU wanapiga mabomu kwenye matumbo ya watu.
 
Rais dhaifu, viongozi dhaifu, polisi dhaifu, wanachi dhaifu, yaani kila kitu ni dhaifu.
Nchi inaelekea kubaya nawaomba wenye dini na wasio na dini kila mtu kwa imani yake tuiombee hii nchi yetu dhaifu. Binafsi nimezoea kuona haya mambo kwenye tv ktk nchi za wenzetu sasa yanatokea kwetu, Eee Mungu tunusuru na hali hii
 
Back
Top Bottom