Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 18,549
- 21,675
"Mwaka 1995 siku moja asubuhi nikapokea ugeni mtoto akaja chumbani kuniambia baba kuna ugeni nikawakuta marafiki zangu watatu, Samwel Sitta, Edward Lowassa na Rostam Aziz, wakaja kuniambia kwamba tunataka muende na Edward Dodoma mkachukue fomu ya kugombea urais mimi nikasema jambo hilo halipo kwenye mawazo yangu, kama yeye lipo kwenye mawazo basi aende, naye akasema siendi bila ya wewe,"- @jmkikweteukiona mtu anatabasamu kwenye kuzika ujue ni psychopath au kwa tafsiri nyingine anafurahia, angalia picha ...
"Basi tukabishana mpaka tukakubaliana kwamba wacha twende, tukaenda kuchukua fomu zile tukazijaza zikarudishwa, michakato ndani ya chama mwenzangu hakubahatika mimi nikabahatika kuwemo kati ya wale watano na baadaye tukapiga kura kwenye NEC nikawemo katika wale watatu, tukaenda mkutano mkuu nikawemo katika wawili, lakini kura zangu hazikutosha akapata Mzee Mkapa nikaja kuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje na mwenzangu akaja kuwa Waziri," - Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu
#RIPLowassa