PICHA: Watoto halaiki waandamana kudai POSHO ZAO (Mwenge)

Huo mwenge hauna maana tena kwanza unawatumikisha watoto! wadai hadi kieleweke.
Ndio maana Nasari aliupiga marufuku jimboni kwake.
 
Hii nchi kwakweli tumeifikisha pabaya sana, tunadhulumu hata watoto wadogo? sasa hapo serikali inataka kutuambia fedha ya kuwalipa hao watoto imekwenda wapi?

Hali hii ikiendelea tutajenga kizazi cha hatari sana, ambacho hakitakuwa na njia nyingine ya kudai hki zao zaidi ya maandamano, na kitu kibaya sana ni hawa watoto kukua wakiwa na notion kwamba haki haipatikani bila maandamano.

Katika hali kama hii ni dhahiri serikali yetu inapanda mbegu mbaya kwa watoto wetu, wawalipe mara moja na wasiendelee na tabia hii ya kuwadhulumu watoto. Wamekuwa wakiwatenda hivi wafanyakazi wake hasa waalimu sasa imevuka mipaka.
 
This is alert news 4 ccm. waangalien sana hao watoto jaman tambueni wote wana vitambulisho vya kupigia kura!
 
hivi kikwete utaacha legacy gani kwenye nchi hii? hivi huoni aibu?
 
na hao wanaokubali kufanya kazi na ccm wanajitakia, sifa zote za ufisadi bado hawajifunzi tu. wamejitakia kuzikwa hizo posho zao.
 
hivi kikwete utaacha legacy gani kwenye nchi hii? hivi huoni aibu?

ataacha legacy ya kuwa kiongozi mwenye safari nyinngi sana, aliyejishirikisha na watu sana hata katika vitu visivyo na msingi, mvivu wa kutafakari na mgumu wa kutoa maamuzi. mpenda............................... na mengi tu yapo anayoyafanya na atayaacha. na tutamkumbuka kwa hayo
 
kweli ccm inafanya nchi isitawalike, yaani wanadhulumu hadi watoto?
 
Hivi serikali inaajiri watoto siku hizi? Nimesikia kuwa kila mtoto mmoja atalipwa tsh 20000/= je ni kweli?
 
Chenji gani???? Ya rada?
Cha muhimu ni sisi wazazi kuwakataza watoto wetu kushiriki huo utumbo wa CCM.
Watoto wanatolewa madarasani kwa zaidi ya wiki mbili wakifanya mazoezi na mafundisho ya halaiki,
wanapoteza muda wa masomo na nguvu zao, wanaumia kwa kupigwa na jua, na mwisho wa siku wananyimwa hata hela ya maji ya kunywa.
Kweli CCM ni baba la majambazi

Hamtaki watoto wenu watokelelezee kijani kibichi?
 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wotee...
Nchi yangu Tanzania.......
jina lako ni tamu sanaa...
 
kwani kazi hizo zinalipwa, nilidhani wanajitolea kwa uzalendo wao. Au zile suti walizoambia na mkubwa kuwa wabaki nazo ndo wamemalizana hapo
 
Back
Top Bottom