Vijana waandamana mkoani Iringa kumshukuru Kikwete kuwarudisha kazini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu watanzania,

Mkoani Iringa kuna vijana takribani 37 wameandamana mpaka ofisi za CCM kuishukuru serikali ya Rais samia kupitia Mh Ridhiwani Kikwete naibu waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora aliyefika mkoani hapo.

Vijana hao wamekuwa wakijitolea kwa miaka mingi katika nafasi za utendaji wa mitaa,mfano kuna wengine wamefanya kazi ya kujitolea na kufanya kazi na majukumu ya utendaji wa mitaa kwa miaka takribani tisa. Lakini ilipofika wakati wa kuomba ajira serikalini vijana hao wapatao 47 ambao walikuwa katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Iringa walijikuta vijana 37 wanaachwa kwa kigezo kuwa hawana sifa.japo wamefanya kazi ya kujitolea na kutimiza majukumu yao vyema kabisa.

Ridhiwani Kikwete akiongea kwa uchungu mkubwa na maumivu makubwa na huruma kubwa kwa vijana hao walioonyesha uzalendo kwa Taifa lao ,alihoji mamlaka mkoani Iringa kuwa iweje kwenye kuwafanyia usaili kuingia serikalini waseme vijana hao hawana sifa wakati wamefanya kazi hiyo kwa kujitolea na kukaimishwa nafasi za utendaji wa mitaa kwa muda mrefu? Akauliza unawezaje kumkaimisha mtu ofisi unayefahamu hana uwezo wala sifa?

Kikwete kwa uchungu mkubwa alisema muogopeni Mungu ndugu zanguu.na kusema kuwa kama wizara wamepitia na kuangalia wasifu wao na kila kitu na wamebaini na kujiridhisha kuwa vijana hao wana sifa na wamekidhi vigezo .hivyo kutoa maelekezo ya kuwarudisha vijana hao wote kazini.jambo lililo leta na kuamsha tabasamu,furaha na matumaini katika mioyo ya vijana hao wanaotoka familia maskini na wenye kutegemewa na familia zao zilizowasomesha kwa kujinyima na kujibana hadi kushindwa kupata milo mitatu ya chakula kwa siku ili mradi watoto wao wasome na kutimiza ndoto zao.

Hii ndio maana ya CCM kuwa Nuru,Tumaini na kimbilio la wanyonge. Ndio maana mtu akionewa au kunyimwa haki au kudhulumiwa haki yake anakuwa na matumaini kuwa akifika katika ofisi za CCM atapata majibu, tumaini na kufutwa machozi. Ndio maana vijana hawa walikimbilia ofisi za CCM tu na kuwaona viongozi wa CCM na kuwaeleza shida yao .ambapo viongozi wa CCM wakiongozwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia CCM mh Ritha kabati waliwapambania vijana hawa kwa nguvu zao zote mpaka hatimaye wamepata haki yao.

Hii ndio serikali ya Rais samia inayotoa haki kwa haki kwa watu wote.haitaki dhuluma wala uonezi wala unyanyasaji wala ukandamizaji kwa watu au mtu.ni serikali safi na yenye matendo safi.ni sauti ya watu na mtetezi wa wanyonge. Watanzania endeleeni kuiamini ccm na serikali yake kwa kuwa imedhamilia kuwainua na kumshika mkono kila mtu mwenye kuhitaji msaada au sauti ya kumtetea au kumsaidia au kumuwezesha kusonga mbele.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu watanzania,

Mkoani Iringa kuna vijana takribani 37 wameandamana mpaka ofisi za CCM kuishukuru serikali ya Rais samia kupitia Mh Ridhiwani Kikwete naibu waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora aliyefika mkoani hapo.

0742-676627.
WAZEE WANAOSUBIRI HAKI ZAO ZA NSSF MIAKA NENDA RUDI WAMWONE NANI MKUU?
 
Ni vizuri sana watu wamepewa haki yao, lakini tatizo bado halijapatiwa dawa kwa kuwa wahusika wa hili tatizo hawakuwajibishwa. Ukiwaacha hawa ni sawa na kucheka na ngedere utakula mabua
 
Ni vizuri sana watu wamepewa haki yao, lakini tatizo bado halijapatiwa dawa kwa kuwa wahusika wa hili tatizo hawakuwajibishwa. Ukiwaacha hawa ni sawa na kucheka na ngedere utakula mabua
Naamini serikali itawaonya na kuwapa kalipio kali na kwamba atakayerudia au kuendelea na Vitendo hivyo vya uonevu basi hatua kali zitachukuliwa zidi yake .
 
Kwani chama kilichowaondoa kwenye kazi ni chadema? Ccm chama cha kipuuzi sana.
Hawakuondolewa na chama bali na watumishi wachache wasiozingatia haki na maadili ya kazi.ndio maana CCM mtetezi na nuru ya wanyonge imewatetea na kuwarudisha kazini.
 
Sera ya ajira inakanyagwa, Sheria zinavunjwa vunjwa mnakenua. Sheria iko wazi, kwenye Ardhi ya Tanzania AJIRA INAPATIKANA KWA USHINDANI sio mapenzi na Matamko ya Mwanasiasa. Unawajua hao Watendaji? Walipatikanaje? Kama wataaalam wamepitia sifa zao wakajiridhisha hana sifa iweje umrudishe kwa Oya Oya kisa tu Uchaguzi unakuja. HAIKUBALIKI, VIONGOZI WAJIFUNZE KUFUATA SHERIA huu siyo Utawala Bora huyu kachemka vibaya sana.
 
Ngoja nitape supu kwanza kabla sijaunga mkono hojo
F2cz1YubEAAMwIp.jpeg
 
Sera ya ajira inakanyagwa, Sheria zinavunjwa vunjwa mnakenua. Sheria iko wazi, kwenye Ardhi ya Tanzania AJIRA INAPATIKANA KWA USHINDANI sio mapenzi na Matamko ya Mwanasiasa. Unawajua hao Watendaji? Walipatikanaje? Kama wataaalam wamepitia sifa zao wakajiridhisha hana sifa iweje umrudishe kwa Oya Oya kisa tu Uchaguzi unakuja. HAIKUBALIKI, VIONGOZI WAJIFUNZE KUFUATA SHERIA huu siyo Utawala Bora huyu kachemka vibaya sana.
Acha kukurupuka ndugu yangu.wizara imepita cv za hao vijana na imejiridhisha pasipo shaka kuwa vijana hao wana sifa na wamekidhi vigezo.lakini pia vijana hao wamefanya kazi hiyo na kukaimishwa majukumu ya utendaji wa mitaa kwa miaka tisa na muda wote wamefanya kazi na kutimiza majukumu yao kwa weledi na uaminifu mkubwa. Sasa iweje useme hawana sifa? Uliwapeje majukumu kwa miaka yote hiyo kama hawana sifa?
 
Wameshindanishwa na Vijana wa wapi kupata hizo ajira?? Ajira siyo hisani, ajira siyo zawadi, Ajira siyo Takrima tuache kabisa hizi giriba. Watu wapate kazi kwa jasho siyo kwa maneno ya majukwaani. Narudia huu siyo utawala bora, sheria imevunjwa kweupeee. Vijana mnaotafuta ajira huu ni wakati mdai haki zenu mpaka mahakamani kwa huu upuuzi wa kupokwa haki zenu. Sheria ziko wazi
 
Ndugu zangu watanzania,

Mkoani Iringa kuna vijana takribani 37 wameandamana mpaka ofisi za CCM kuishukuru serikali ya Rais samia kupitia Mh Ridhiwani Kikwete naibu waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora aliyefika mkoani hapo.

0742-676627.
Halafu, wanarudishwa kazini kwani walikuwa wamejiriwa? Au wamerudishwa kujitolea?
 
Lucas,

Ukitaka nikiamini Chama Cha mapinduzi,

Naomba wakuajiri kwanza wewe ,nitakiamini na nitachukua kadi kesho
Kwani hujaona serikali ya Rais samia ikitoa maelfu ya ajira kwa vijana waliokuwa wamekata tamaa na kuishiwa matumaini.hujaona namna mh Rais alivyojitahidi kutengezea fursa za ajira kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa hapa Nchini.
 
Halafu, wanarudishwa kazini kwani walikuwa wamejiriwa? Au wamerudishwa kujitolea?
Wataajiriwa serikalini maana walikuwa wametolewa katika ofisi walizokuwa wanafanya kazi kwa kujitolea lakini wakitekeleza majukumu yote ya mtendaji wa mtaa.
 
Kwani hujaona serikali ya Rais samia ikitoa maelfu ya ajira kwa vijana waliokuwa wamekata tamaa na kuishiwa matumaini.hujaona namna mh Rais alivyojitahidi kutengezea fursa za ajira kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa hapa Nchini.
Narudia
Lucas,

Ukitaka nikiamini Chama Cha mapinduzi,

Naomba wakuajiri kwanza wewe ,nitakiamini na nitachukua kadi kesho
 
Back
Top Bottom