Picha - Shonza/Mwampamba UVCCM - waliobaki wawafuate

Picha - Shonza/Mwampamba UVCCM - waliobaki wawafuate

Yuko kitengo cha "mawasiliano" ofisi ndogo. Hapandi tena daladala, siku hizi ana baloon.

Hivi anajua kuwasiliana huyu kweli , ama kitengo hicho ni cha mawasiliano ya aina gani? Maana najua hajui hata kutumia Kompyuta huyu sasa sijui hicho kitengo ni cha aina gani....
 
308012_334538663316880_538665124_n.jpg


Waliojivika ngozi ya kondoo ndani ya CHADEMA kama akina Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wangalipo? Hapana budi kuwaondoa warudi kwenye kundi lao kama wenzao hapa kwenye picha, Hatutaki ndumila kuniwi, wanachotafuta ni shibe si ukombozi wa Mtanzania.

CHADEMA wabaki wapiganaji wa kweli, kwani CCM wangali na oversize zisizotumiwa zinawasubiri.

Wenzano wameshtukia deal, mbona hawawafuati?
 
308012_334538663316880_538665124_n.jpg


Waliojivika ngozi ya kondoo ndani ya CHADEMA kama akina Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wangalipo? Hapana budi kuwaondoa warudi kwenye kundi lao kama wenzao hapa kwenye picha, Hatutaki ndumila kuniwi, wanachotafuta ni shibe si ukombozi wa Mtanzania.

CHADEMA wabaki wapiganaji wa kweli, kwani CCM wangali na oversize zisizotumiwa zinawasubiri.
Mbona sura zao zinaonyesha hawana Amani na Furaha ya ukweli ........
 
Bob Marley alishawahi kusema katika muziki wake wa "Time will Tell" akisema "You think you're in heaven, but you are living in Hell".Tuwasubirie hawa hata watatuambia tu kama wapo "Heaven" au "Hell"....
 
Sasa kama unajua haya kwanini unasema wamarekani wana genes tofauti na mimi? By the way, umejuaje kuwa mimi sio mmarekani?

Jisome mwenyewe hapo juu jinsi usivyo consistent. Wewe mwenyewe unasema mambo halafu wewe mwenyewe unayapinga na kujifanya kuwa ni maneno yangu!!! Lakini hii ni dalili kuwa umeelewa somo nililokupa. Haya sasa nenda na wewe ukafundishe wengine wanufaike.


Mimi nimejuwa kuwa wewe sio mmarekani kwa kumfananisha Shoza na Regan... regan kilichomwamisha ni sera shoza bila kupinga ni maslai... na kale ka maneno alikopewa kwa Bahasha ya khaki iliyoandikwa Goverment....
 
Ila tuache utani jezi za ccm ni nzuri kuliko chama chochote tanzania, hazitishi.
 
Njaa mbaya sana! Hawa lazima watauza chupa za maji!
 
Juliana Shonza

15 hours ago ·
Kumekuwepo na habari za uzushi na zilizojaa upotoshaji mkubwa juu ya kile tulichokizungumza mimi na Mtela Mwampamba katika kipindi cha mahojiano ya asubuhi katika redio moja ya passion fm ya jijini Dar es salaam.
* Nilipohojiwa juu ya msimamo wa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe wa kutaka kufanya maandamano ya kupinga matokeo ya form four..?
Niliyoyaeleza ni haya;
Kuwa kabla ya mbowe kufikiria maandamano ya kupinga na kuishinikiza serikali kubadili matokeo hayo ni muhimu kujiuliza maswali kadhaa ya msingi kabla ya kufikia hitimisho kuwa tatizo ni usahihishaji na grading ya matokeo.
Maswali hayo ya msingi ni kuwa;
1) Je Wanafunzi hawa walipata Elimu yao katika misingi stahiki..?
2) Je Wazazi walikuwa wakifuatilia matokeo na mienendo na maendeleo ya watoto wao mashuleni..?
3) Je Bodi za shule ambazo zinaundwa pamoja na kamati ambazo zina wajibu wa kufuatilia na kufanya tathmini ya kina juu ya Maendeleo ya shule husika hazikuona dalili za mazalia haya? Au hazikushauri shule na wazazi juu ya namna ya kuinua viwango vya ufaulu na mafanikio ya wanafunzi wao au zilikuwa bodi za vikao na posho..?
Hivyo unapotaka kuzungumzia juu ya kufeli na kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini kuna mlolongo wa sababu zinazozaa kasoro hizi tunazoziona leo, natoa hoja hizi kwa sababu si kila upele ni upele wa joto, upele mwingine unaweza kuwa ni upele wa surua ama tetekuanga.
Hivyo basi namtaka mbowe hatueleze sababu za yeye kufeli., je sababu zake za kufeli ni kama hizi zilizosababaisha matokeo ya sasa.?
Nilifafanua kuwa badala ya Mbowe kuendesha maandamano ambayo hayatokuwa na tija ni bora angeshirikiana kwa ukaribu na kamati iliyoundwa na Mhe. Waziri Mkuu ya kuchunguza kasoro zilizopelekea watoto kufeli na kufuatilia sababu halisi ya matokeo mabaya na kushuka kwa kiwango cha Elimu. Hili lingelikuwa na mantiki kubwa na hoja za msingi.
Naomba niongozwe na usemi usemao "nyani haoni kundule" kwa kuwa hata yeye Mbowe ni muhanga wa kufeli na kuitwa bwana zero kwa matokeo aliyopata form six., mbona yeye ama wazazi wake hawakuandamana pindi yeye alipopata zero..? kwanini yeye leo ashadidie watu kuandamana..?

Pia natoa wito kwa watanzania wasiwe tayari kushawishika kuandamana katika mambo ambayo hatujui chanzo chake ni nini. Lakini pia hukuna msingi wa kuandamana katika masuala ambayo suluhu yake haipatikani kwa maandamano.,umefika wakati sasa watanzania kuacha kuwa uhondo wa wanasiasa, wakawa wanacheza kila ngoma inayopigwa na wanasiasa hawa uchwara kama Mbowe.
Kuandamana katika suala hili ni sawa na kumlazimisha kumchoma sindano ya malaria mgonjwa kabla ya vipimo vya maabara havijatoka na kubainisha nini anachoumwa, ni vema kusubiri matokeo ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa.
Maandamano hayatoweza kutatua matatizo ya mfumo wa Elimu ambao unajumuisha na kuhitajia juhudi za pamoja kati ya wazazi, walimu na serikali. Suala hili linagusa mfumo wetu wa malezi na mabadiliko hasi ya nidhamu ndani ya jamii yetu. Si sahihi hata kidogo wazazi, walimu na jamii kujiweka pembeni na kuinyooshea kidole serikali pekee.
Lakini baya zaidi ni pale ambapo tunataka kuruhusu na kuliendesha suala hili kisiasa, kwa kulitazama tatizo hili la kitaifa kama fursa ya kujijengea ujiko wa kisiasa na kupotosha msingi wa tatizo na kupindisha uhalisia wa njia za kweli zinazoweza kutupa suluhisho la kudumu juu ya Elimu yetu.
Si kitendo cha kistaarabu hata kidogo, kujipa nafasi za kuwasemea watanzania katika mambo ambayo yanahitaji kauli na maamuzi ya pamoja. Mbowe hana legitimacy ya kuwasemea watanzania katika mambo yao ya msingi. Yeye sio msemaji wa serikali wala si mshirika wa serikali.
Mtangazaji alituuliza juu ya kauli ya mbunge wa kawe Mhe. Halima Mdee ya kutuita "sisimizi"
Majibu yetu yalikuwa ni;
Inahitaji subira na umakini pale ambapo unamjibu mtu ambae tayari anamatatizo ya kisaikolojia na anajihusisha na matumizi ya mihadarati hususani uvutaji wa bangi. Halima Mdee inaeleweka wazi kuwa ana matatizo makubwa ambayo yametokana na uvutaji wa bangi na hivyo huwa anaongea kulingana na zinavyomtuma kichwani mwake.
 

TAMKO LA MAKAMU MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA) TAIFA JULIANA SHONZA JUU YA MH SHIBUDA MBUNGE.

UTANGULIZI:-
Ndugu wanahabari,nimewaiteni hapa leo siku ya jumapili tarehe 20.05.2012 kwa ajili ya kuweka sawa baadhi ya mambo ambayo yameweza kulidhalilisha baraza letu la vijana,mambo hayo yanachafua taaswira nzima ya uongozi wa BAVICHA,chombo ambacho ndicho kinalea vijana wanaokwenda kuunda uongozi wa Serikali mwaka 2015.Chombo hiki ni nyeti sana,nichombo kilichoundwa kimakusudi kwa ajili ya kuwalea na kuwandaa vijana katika uongozi na utumishi wa Taifa hili kimaadili na kiutaalamu.Ndugu wanahabari,wote mnafahamu na mnalijua suala ambalo limejitokeza ndani ya wiki hii inayoisha juu ya Kauli ya Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Taifa, bwana John Heche.,

Tamko lake lilimhusu Mzee wetu Mh Shibuda[mb] juu ya kauli yake ya kugombea Urais mwaka 2015 alipo kuwa anatoa semina mjini Dodoma kama mjumbe wa APRM kwenye halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi[CCM].

Hili ndilo lililo nilazimisha Makamu Mwenyekiti wa baraza la Vijana kuona umuhimu wa kulitolea ufafanuzi wa kina,maana kwetu kama wanasiasa tunaokua tunaamini kwamba suala lolote lenye mashaka linapojitokeza kama hili ni vizuri kulijadili kwa kina na kulitolea ufafanuzi ili kuweza kuweka kumbu kumbu sawa.

KAULI YA MWENYEKITI JUU YA MZEE SHIBUDA[mb].
Ifahamike kwamba ni haki ya Kikatiba kwa mwanachama yoyote kuweza kuonesha nia ya kugombania nafasi yoyote inayojitokeza ndani ya chama na nje ya chama,nia hiyo inaweza ikaendana na mchakato wa kimaandalizi wa namna ya kufikia dhamira hiyo pasipo kuvunja vipengere vya kikatiba ya chama chetu,mwisho wa siku vikao halali vitaketi katika kuweza kuwachambua wagombea na kuwasilisha majina yao kwenye mkutano mkuu wa kichama Taifa unaohusisha wajumbe wa mkutanomkuu ambao ni viongozi wa chama katika ngazi za wilaya na mikoa,hao ndiyo kikatiba wanaosema ndiyo au hapana kwa wagombea.

Hivyo siyo vibaya kwa wanachama kuonesha dhamira zao za dhati juu ya Urais na nafasi nyingine yoyote kuwafahamu wagombea wao katika nafasi mbali mbali na ndiyo maana makamanda wetu wapo kujenga majimbo huko kwa ajili ya kufikia adhima zao za utumishi lakini hatima ya dhamira zao zitatimia kwa maamuzi ya vikao halali vya chama.Hivyo siyo sahihi kwa kiongozi wa chama kusema hapana kwa mgombea yoyote ndani ya chama,wenye mamlaka ya kusema hapana au ndiy ni wajumbe wa vikao halali na siyo mjumbe.

Nianze kwa kusema hakuna mfuko,uwe wa shati,sketi au Suruali unaweza kukaa na kaa la moto.Tamko la Mwenyekiti John Heche kuhusiana na Kauli aliyoitoa Mbunge wa Maswa Magharibi Mh John Shibuda kuhusu kutaka kugombea Urais.

Mimi kama Makam Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema[BAVICHA] Taifa,Siwezi kuvumilia kukaa na kaa la moto mfukoni,na hili naliongea kwa hisia kali kwasababu nataka niweke wazi kabisa kwamba tamko alilolitoa John Heche siyo tamko la Baraza kwa maana ya kuwa tamko la BAVICHA bali ni tamko lake kama Heche na siyo BAVICHA,namimi kama Kiongozi wa juu kabisa wa Baraza nina ujasiri na uhalali wa Kisiasa na KIsheria wa kutamka haya kwa sababu zifuatazo;

Kwanza John Heche alipotoa tamko hilo hakukuwa na kikao chochote cha baraza kiwe cha Viongozi wa kitaifa kwa maana ya Mwenyekiti,makamuMwenyekiti,ka tibu,Katibu mhamasishaji na Mweka hazina,wala Sekretarieti ya Baraza la Vijana la CHADEMA ili kulijadili kwa kina suala hili.

Hakukuwa na Kikao wala minitusi za kikao ambazo ndizo zilipaswa kutoa maazimio ambayo Mwenyekiti alipaswa kuyawasilisha kwa waandishi,kwa maana ya kuyatolea tamko ambalo sasa ndilo lingekuwa na hadhi ya tamko la BAVICHA.

Pia tamko hilo alilotoa John Heche dhidi ya John Shibuda[mb] liliandaliwa na kuandikwa na Afisa habari wa chama makao makuu.,kitu ambacho ni kinyume cha utaratibu na kanuni za BAVICHA,kwani BAVICHA tumejikamilisha kwa maana ya kwamba tuna uongozi wetu kamili wa Kitaifana tuna ofisi zetu ambazo ni nje ya ofisi za makao makuu.

Kwa maana hiyo basi,Shughuli zote zinazo husu baraza ikiwamo utayarishaji na uandikaji wa Matamko ya Baraza inapaswa ifanywe na Katibu wa Baraza au katibu mwenezi wa Baraza na na siyo afisa habari wa Chama.

Natambua wazi kuwa Mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa Baraza la Vijana kama taasisi,lakini siyo kila anachokisema ni cha Vijana,kama hili alilo lisema amesemea matamanio yake na siyo maamuzi ya Vijana.

Kama baraza la Vijana,kwa hili lililojitokeza dhidi ya Mzee Shibuda,ambaye ni mzee wetu,mbunge hivyo ni kiongozi mwenzetu,kama tungeliazimia kwamba ni kosa ilitakiwa tukishauri chama namna ya kuweza kulishughulikia kichama,lakini hata hivyo diwani ama mbunge anavyofanya vitu vitakavyotafsiriwa kwamba ni kosa,kuna Caucas ya wabunge,ambayo ndiyo inapawa kumjadili mbunge husika na kumchukulia hatua zinazo mstahili kikanuni,isipokuwa kama tamko lingekuwa limetolewa na mbunge Kijana,baraza lingeweza kumshughulikia kwenye vikao halali vya baraza pamoja na kwamba linajadiliwa na caucas ya chama,kwasababu ni kijana mwenzetu.

Kwani kunabaadhi ya wabunge vijana kama Mh Raya Ibrahim[mb] na Mh Sabrina Sungura[mb] ni wajumbe wa Baraza na huwa tunakutana nao kwenye vikao vya baraza.

Kama utaratibu huu alioutumia John Heche,angekuwa anautumia Katibu Mkuu wa Chama[Dr Slaa] au Mwenyekiti wa Chama[Mh Freeman Mbowe] kwamba wanafanya maamuzi wenyewe pasipo kuyajadili na Sekretarieti ya Chama makao makuu,nina uhakika matunda tunayoyaona leo ya chama yasingekuwapo.

Baraza la Vijana la Chama,hasa chama kikuu cha upinzani Chadema,chama kinachoangaliwa na watanzania kama tumaini lao,chama kinachokwenda kushika dola,ni lazima liweze kufanana na hadhi ya Serikali Mbadala,kwa hiyo ni lazima tuwe na viongozi vijana wanaojua maana ya taasisi na kutoa mfano wa kiuongozi kitaifa.

Ndugu Waandishi,hata kama Mwenyekiti wa Baraza,alimuona Mh Shibuda ana makosa,angeweza kushauriana na Baraza na kumfuata Mh Shibuda juu ya nia ya Kauli yake, Kwa maana hiyo Heche anamaanisha kwamba leo hii Mwenyekiti wa Chama Taifa Chadema au Katibu Mkuu Chama Taifa wakikosea tuweze kuwaropokea,kuwakejeli na kuwatukana hadharani,tena kwa vyombo vya habari.

Ndugu Waandishi,kuna matatizo makubwa sana yanawaandama vijana,kama vile suala la mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu,masuala ya ajira zao,masuala ya kinamama vijana kujifungulia sakafuni pasipo wakunga,masuala ya mamachinga nk,haya ndiyo baraza linapaswa kuonesha uongozi wake nahalali wa u uwepo wake.


 
Kutoka pipoooooooooooooo, pawaaaaaaaaaaaaaa, mpaka ccm oyee, oyeeee, du kweli wameshuka hamasa. mbona siwasikii siku hizi hawa jamaa, vipi zile kula elfu 35 za watu wa mbozi bado anazisema?
 
Back
Top Bottom