PICHA: Rais Kikwete katika ziara rasmi Ottawa, Canada

Unaacha mipaka yetu ina porwa na malawi wewe unaenda kuvutwa na mikokoteni ya wanyama? Si Arusha ipo inayo beba maji kutoka visimani? kweli watanzania mzigo mnao. Ole wako utoke madarakani ukituonyesha nchi yetu imebaki nusu.
 
Tuliyataka wenyewe kwa kutosikia ya wakuu aliposema mwalimu kwamba J.K hafai kuwa rais kwa kuwa ni mtoto. Tungepaswa kutafakari kauli ya 'utoto wa Kikwete'. Katiba inamruhusu mgombea urais awe na umri kuanzia miaka 40. Alipoambiwa ni mtoto alikuwa na umri wa miaka 45. Ni wazi kwamba mwalimu alikuwa anamaanisha utoto wa akili. Mwaka 2005 wengi walimchagua, si kwa sababu ya rekodi yake kiutendaji, bali kiushabiki tu. Sasa haya ndio matokeo yake! Utoto mtupu...'Chronological age' yake ni miaka 60+ lakini 'mental age' yake ni ya teenager wa miaka 19 hivi maana ana tamaa sana, hasa ya kusafiri safiri...!
 
''Mwanajeshi'' wetu mbona ''marching'' yake haiendani na hao wanajeshi wengine?.......left....right......left......... right

attachment.php

Gwaride ameshasahau !
 
Huyu ni rais wetu tuliomuweka Ikulu sisi wenyewe kwa kura zetu , kama mnampenda hamumpendi anamaliza 2015 tutachagua rais mwengine. Kwa sasa shime wananchi tumpe support rais wetu amalize muda wake. Maana kuna wengine hata wakiona picha rais anakunywa maji wanakasirika eti kwanini rais anywe maji kwikwikwikwi .
 
Kwa hiyo tulimchagua atimize muda au wajibu na majukumu yake? HATUWEZI KUACHA KUMSEMA kama hatofanya yale yanayopaswa kufanywa na RAIS katika hali ya kawaida ikiwemo kutimiza wajibu na majukumu yake ipasavyo. Na tunafanya haya ili huyo ajaye asije kuwa kama yeye na wala si chuki na yeye.
 
Amenifurahisha hapo alipopanda kwenye mkokoteni....ha ha ha ha ha ha ha ha, kama anachungulia pembeni vile. Kweli kazi tunayo watanzania.
 
JF acheni upuuzi wa kijinga. Naona sasa watu wameishiwa point wanaropoka tu. Hii ni ziara ya kiserikali. Mimi ninashangaa sana kuna humu JF wanajiita wanamheshimu Mungu kumbe ujinga dini zinasema "HESHIMUNI MAMLAKA ILIYOWEKA". Sasa kutoa mananeno ya kejeri, vijembe ambavyo havina mantiki kwangu binafsi naona ni ujinga.

afadhari tumpe tafu Raisi wetu. Ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kwa hiyo tulimchagua atimize muda au wajibu na majukumu yake? HATUWEZI KUACHA KUMSEMA kama hatofanya yale yanayopaswa kufanywa na RAIS katika hali ya kawaida ikiwemo kutimiza wajibu na majukumu yake ipasavyo. Na tunafanya haya ili huyo ajaye asije kuwa kama yeye na wala si chuki na yeye.

Sasa kuna makosa gani rais kufanya Ziara nchi za nje kwenda kuzungumza na mataifa mengine.

Huoni kama hizo ni learning opportunities kwa Mr Presient na delegation yake?
 
Kwa hiyo tulimchagua atimize muda au wajibu na majukumu yake? HATUWEZI KUACHA KUMSEMA kama hatofanya yale yanayopaswa kufanywa na RAIS katika hali ya kawaida ikiwemo kutimiza wajibu na majukumu yake ipasavyo. Na tunafanya haya ili huyo ajaye asije kuwa kama yeye na wala si chuki na yeye.

Subirini rais wenu kivuli Slaa ambaye atakuwa anafanya Ziara za Arusha-DSM tu! teh teh teh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom