PICHA: Rais Kikwete katika ziara rasmi Ottawa, Canada

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
attachment.php


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Oktoba 4, 2012

attachment.php

attachment.php

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

attachment.php

attachment.php

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

attachment.php

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Oktoba 4, 2012.

attachment.php
 

Attachments

  • 16.jpg
    16.jpg
    38.1 KB · Views: 4,014
  • ot1.jpg
    ot1.jpg
    72.7 KB · Views: 4,516
  • ot2.jpg
    ot2.jpg
    76.4 KB · Views: 4,100
  • ot3.jpg
    ot3.jpg
    76.3 KB · Views: 4,047
  • ot4.jpg
    ot4.jpg
    84 KB · Views: 4,270
  • ot18.jpg
    ot18.jpg
    93.8 KB · Views: 4,238
  • ot19.jpg
    ot19.jpg
    69.4 KB · Views: 3,977
Du! kweli urais ni mtamu. Kuishinda CCM 2015 kunahitaji nguvu za ziada
 
ahhhaaa hili TAIFA kweli Rais tunaye, hivi kagame huwa naenda kwenye anasa na tafrija namna hii? anapokelewa na waziri wa mambo ya Nje, duh heshima ya tanzania Nje kwisha.
 
Jamani hiyo ndiyo protocol ya ziara rasmi ya kikazi!!! Sasa ulitaka iweje mkuu?

Ndio na mimi naona mkuu wangu ana enjoy tu, ndio maana hawa magamba hawataki kutoka madarakani, anajuwa hapo hizo safari zitaisha, na wacha amalize muda wake atazilipa tu hizi safari zisizo na mpango......
 
Ndio na mimi naona mkuu wangu ana enjoy tu, ndio maana hawa magamba hawataki kutoka madarakani, anajuwa hapo hizo safari zitaisha, na wacha amalize muda wake atazilipa tu hizi safari zisizo na mpango......


Mwenzenu ameenda kuwahakikishia kuwa yale mabadiliko ya sheria ya madini yaliyoongera mrahaba, utekelezaji atahakikisha anaukwepa hadi atoke madarakani!!!

Ni mwendo wa kutembeza bakuli tu!!
 
''Mwanajeshi'' wetu mbona ''marching'' yake haiendani na hao wanajeshi wengine?.......left....right......left......... right

attachment.php

SnS picha inaongea zaidi ya maneno! Surely JK amechoka sana!!!!

Yupo tu, muda uende nina uhakika ile tamaa yake imekwisha kabisa!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom