Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
Picha hizi sijazipenda kweye maombolezo ya hayati dada yetu Rigia Mtema
Najua wengi hapa watanifutulia macho, lakini watanzania tunatakiwa tuwe na upeo wa kutambua na kuchanganua nafasi za matukio. Hapa si masuala ya chama, ni msiba ambao unatuhusu watanzania wote. Alivyovaa Freeman Mbowe safi kabisa ni vazi la msiba. Picha ya kikwete unamwona kijana kwa mbali na pendera ya Chadema kajifungia huu ni mtazamo finyu, hapa ni msiba wetu sote.
Hali kadhalika Dr. Slaa anatakiwa awe na mabadiliko ya mivao kutofautisha nafasi kama hizi. Vazi hilo hilo ofisini, msibani, kanisani, hotelini nk. hapana, nitaendelea kutoa somo hadi tutakapokuwa mstari mmoja.
Haujapenda nini sasa mkuu?mbona hizo ni picha za kawaida sana?kumbuka Regia mpaka anaondoka alikua anasimamia na kutekeleza itikadi za chadema katika kuhakikisha watanzania wenzake wananeemeka na rasilimali zao,na ndio maana hata mh rais alipotuma salamu za maombelezo alimtumia MWENYEKITI WA CHADEMA na akaomba azifikishe kwa familia ya mpendwa wetu Regia,hizo picha hazina madhara yeyote na suala zima la msiba,na utamaduni huo si kua ndio chadema wa kwanza kuutumia duniani!sitashangaa na nitafarijika sana nikiona dada yetu anazikwa na bendera ya chama ambacho mpaka umauti wake aliamini kua kingewakomboa watanzania katika matatizo yao lukuki!watanzania ni wamoja,tunatofautiana kiitikadi tu jinsi ya ukombozi wetu kiuchumi!kapumzike kwa amani dada yetu,mwana Morogoro mwenzangu Regia E Mtema!tutaonana tena paradiso
Hojatete acha hizo. Kumbuka Hayati Regia alikuwa mbunge kupitia tiketi ya chadema hivyo nafikiri ni sahihi tu kuonekana kwa bendera ya chama. Sioni kama kuna tatizo sana hapo. Pia nashukuru sana kwa mdau aliyetuwekea picha tukaona kilichokuwa kinaendelea.
Picha hizi sijazipenda kweye maombolezo ya hayati dada yetu Rigia Mtema
Najua wengi hapa watanifutulia macho, lakini watanzania tunatakiwa tuwe na upeo wa kutambua na kuchanganua nafasi za matukio. Hapa si masuala ya chama, ni msiba ambao unatuhusu watanzania wote. Alivyovaa Freeman Mbowe safi kabisa ni vazi la msiba. Picha ya kikwete unamwona kijana kwa mbali na pendera ya Chadema kajifungia huu ni mtazamo finyu, hapa ni msiba wetu sote.
Hali kadhalika Dr. Slaa anatakiwa awe na mabadiliko ya mivao kutofautisha nafasi kama hizi. Vazi hilo hilo ofisini, msibani, kanisani, hotelini nk. hapana, nitaendelea kutoa somo hadi tutakapokuwa mstari mmoja.
Kwa mwendo huu Slaa hafai kuwa na nafasi kubwa kwenye serikali yetu.
Mtu asiyependa madiliko hafai. Inabidi ajifunze kubadilika na kuendana na mazingira.
Hii tafsiri si sahihi Rais anapewa mamlaka hata yaliyo nje ya katiba na yaliyo ya binafsi, huongozi maombolezo kama hujashiriki kujayaandaa na bila ridhaa ya wahusika! Naomba hiki kichwa cha habari kibadilishwe kiwa Rais JK ashiriki kwenye maombolezo au aongoza serikali yake kwenye maombolezo! Ni hayo tuu....Katika nafasi kama hizi tunatanguliza wakuu kwamba wanaongoza maombolezo, ni kitu cha kawaidfa kutafsirika vizuri tu. Asante Geza Ulole
Suala la mavazi sidhani kama ni tatizo wao Chadema kuweka mabango yao ni sawa kwa kuwa alikuwa mwakilishi kupitia chama chao, mavazi yao ni sehemu ya maombolezo kwao, hujawahi kuona wanachama wa nyama vingine pia wanazikwa wakati jeneza limefunikwa na bendera ya chama, na hiyo inatokea kokote kule duniani.
Picha hizi sijazipenda kweye maombolezo ya hayati dada yetu Rigia Mtema
Najua wengi hapa watanifutulia macho, lakini watanzania tunatakiwa tuwe na upeo wa kutambua na kuchanganua nafasi za matukio. Hapa si masuala ya chama, ni msiba ambao unatuhusu watanzania wote. Alivyovaa Freeman Mbowe safi kabisa ni vazi la msiba. Picha ya kikwete unamwona kijana kwa mbali na pendera ya Chadema kajifungia huu ni mtazamo finyu, hapa ni msiba wetu sote.
Hali kadhalika Dr. Slaa anatakiwa awe na mabadiliko ya mivao kutofautisha nafasi kama hizi. Vazi hilo hilo ofisini, msibani, kanisani, hotelini nk. hapana, nitaendelea kutoa somo hadi tutakapokuwa mstari mmoja.
Kwa kweli hii nimeipenda sana, tunatanguliza utaifa kwanza, katika matukio kama haya tofauti za kiitikadi tunaziweka kando na tunaungana kufanya maombolezo yanye kutukutanisha na kuwa taifa moja. Hizi ni nafasi adimu sana ambazo hutokea kutuunganisha watanzania wenye itikadi tofauti na kushirikiana kuwa kitu kimoja.
Sote pamoja na kutofautiana kiitikadi malengo ni kwa ajili ya kujenga taifa letu, kwani itikadi ni njia tofatuti tu tunazopitia tukiwa na malengo yale yale yakufikia kileleni. Na hizi tofauti zetu za kiitikadi tunapoziunganisha kwa kupishanisha kupeana awamu ni malengo ya kuchochea maendelea ya taifa si uadui.
Narudia matukio haya ni ujumbe mahsusi kwetu na njia ya kuzidi kutuunganisha na kutoa tofauti za kifikra za kuhasiniana bali kujenga mfumo wa kushindana kwa hoja ndio maendeleo tunayotaka.
Hongera viongozi wa serikali kuonyesha njia, kwani wengi wamejifunza na watazidi kujifunza mengi katika matukio kama haya licha ya simanzi nzito aliyotuachia dada yetu marehemu Regina Mtema.
Tunataka Maalim Seif awaongoze CUF na wazanzibar kushiririki msiba huu mzito wa kitaifa