Siku 21 za maombolezo ya kifo cha Rais Magufuli zafika ukingoni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa makamu wa Rais alitangaza kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli Machi 17, 2021 na kutangaza maombolezo ya siku 21 kwa mujibu wa sheria.

Hayati Rais Magufuli amefanyiwa maombolezo yakiwa ni pamoja na bendera kupepea nusu mlingoti na vyombo vya habari hasa televisheni na vituo vya redio vikipiga nyimbo za maombolezo.

Rais Magufuli alizikwa Machi 26, 2021 wilayani Chato, Mkoani Geita baada ya kuagwa na wananchi wa Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar na Mwanza.

Rais Magufuli aliingia madarakani Mwaka 2015 ambapo alichukua kiti cha urais kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
 
Back
Top Bottom