Picha: Ni kweli na shibuda hamtambui kikwete hii ilikua jana kwenye mnuso wa wabunge

Mbona kwenye Audio ya MKJJ Dr.Slaa alisema hawata hufdhuria sherehe?
Huyu shibuda vipi?na mbona ananyenyekea sana kusalimiana na mkwere?hebu mcheki mikono yake yote kamshika mkwere!mkwere nae hana hata tym nae basi tu lakini anajiuliza hii ni njaa au nini?
Shibuda simwamini kama ni mpinzani....chadema angalieni siri zisije kuvuja!
 
Mimi nina wasiwasi kwamba hiyo picha sio ya huo mnuso, wamechakachua tu, hebu chadema watuambie ukweli

Yaap umeshtukia, this is a wrong picture in a wrong time, Michuzi ni CCM hana jipya kai yake kuchengua watu, huu ni uongo no one from CDM MPs attended CCM party, no one, michuzi balaa, ignore this pict. please
 
Shibuda atofautiana na chama chake

MBUNGE wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda hakubaliani na msimamo wa chama chake kumsusia Rais Jakaya Kikwete, akisema matatizo humalizwa kwa mazungumzo.

“Suluhu ya matatizo huwa ni mazungumzo, na ndiyo sababu Palestina na Israeli wanafanya mazungumzo, ili kumaliza mgogoro wao,” alisema Shibuda jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu Chadema kususa hotuba ya Kikwete bungeni juzi Dodoma.

Source: HabariLeo Jumamosi Novemba 20, 2010

Frankly speaking, kama habari hii haiijachakachuliwa huyu jamaa anahitaji counseling ya nguvu, its tool early to sit witta CCMm for any discussion!!!
 
Shibuda atofautiana na chama chake

MBUNGE wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda hakubaliani na msimamo wa chama chake kumsusia Rais Jakaya Kikwete, akisema matatizo humalizwa kwa mazungumzo.

"Suluhu ya matatizo huwa ni mazungumzo, na ndiyo sababu Palestina na Israeli wanafanya mazungumzo, ili kumaliza mgogoro wao," alisema Shibuda jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu Chadema kususa hotuba ya Kikwete bungeni juzi Dodoma.

Source: HabariLeo Jumamosi Novemba 20, 2010

Frankly speaking, kama habari hii haiijachakachuliwa huyu jamaa anahitaji counseling ya nguvu, its tool early to sit witta CCMm for any discussion!!!

Huyu atatuvuruga sana, wasimpe hata cheo cha kufuta meza, nafisi ni mamluki sijui kwa nini
 
Shibuda atofautiana na chama chake

MBUNGE wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda hakubaliani na msimamo wa chama chake kumsusia Rais Jakaya Kikwete, akisema matatizo humalizwa kwa mazungumzo.

"Suluhu ya matatizo huwa ni mazungumzo, na ndiyo sababu Palestina na Israeli wanafanya mazungumzo, ili kumaliza mgogoro wao," alisema Shibuda jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu Chadema kususa hotuba ya Kikwete bungeni juzi Dodoma.

Source: HabariLeo Jumamosi Novemba 20, 2010

Frankly speaking, kama habari hii haiijachakachuliwa huyu jamaa anahitaji counseling ya nguvu, its tool early to sit witta CCMm for any discussion!!!

Shibuda ni mtu mmoja tatizo mno na ni 'very controversy' mno na yuko 'flip-flop' wakati wowote. Nachelea kutabiri mahusiano yake na Chadema katika siku fupi zijazo. Kwani ni kama mtu aliye CHADEMA kwa 'convinience' tu lakini moyo na hisia zake ziko CCM na unamhisi kuwa anatamani aendelee kuwa mbunge chini ya Chama tawala. Sita shangaa akirejea huko huko CCM hivi karibuni baada ya kwisha kuichafua CHADEMA.
 
Ila Chadema ilionywa kuhusu hawa 'mamluki' waliotoka ccm...
Nimeshtuka sana nilipoiona picha yake front page ya Mwananchi leo...
 
Shibuda bado mgeni kwenye kambi ya upinzani so bado ana itikadi za CCM, tumpe muda tu atabadilika, labda pia tumkumbushe kuwa CCM haimtaki kwa lolote
 
Nadhani ni kuwa makini sana na wabunge wote waliogombea kupitia CHADEMA baada ya kuangushwa kura za maoni CCM.Yawezekana Shibuda hajakosea kwa kusema hilo kwani ana haki hiyo lakini pia kumbukeni sherehe hiyo ilikuwa ni ya wabunge kupongezana so hakuna tatizo kwa Shibuda kuwepo.Kumpa mkono JK si dhambi ubinadadamu upo jamani.
 
Sherehe ilkuwa ni ya kupongeza wabunge , haihusiani na hotuba ya Raisi bungeni. Shibuda pia alikwenda kuwaringishia CCM kwamba pamoja na kunichakachua kwenye kura za maoni na kutaka kunimaliza kisiasa bado nipo mjengoni.
 
kimsingi kuna wakina 'Shubuda' wengi tuu na hasa kwenye nganzi ya udiwani cha msingi ni viongozi wa chama kuandaa semina ili kuwaweka sawa, sisi katika jimbo letu (kanda ya ziwa) ofisi ya wilaya imeisha liona hilo na tayari imeisha anza kuandaa semina kwa ajili ya madiwani wa CDM kwa sababu miongoni mwao wapo waliotoka CCMm, kwa kweli kwa hilo nawapongeza sana katibu na mwenyekiti wa CDM wilaya kwa kuliona hilo.
 
Je mnatambua kama Shibuda?
Huyu ni UWT ambaye alikaa sana Zanzibar kwa kazi hiyo, nasikia alitimuliwa kwa makosa ya Fedheha. Lakini amekuwa ganda la Muwa ambao CCM wamelikataa na Chadema kuliokota, kwa Mtazamo wanu hana madhara kwa mambo yake isipokuwa faida kwani amesaidia kutuongezea wingi wa viti. Anao mchezo mmoja wa MOMBASA ambao nadhani bado unampeleka CCM kwa washikaji wake.
 
pamoja na kwamba ilikuwa haijapangwa kwa yeye kwenda chadema lakini nadhan sasa ccm wamepata pa kuingilia kwa chama cha chadema.......akizidisha ujinga wamchinjie baharini kama kina kafulila wapo vijana wengi na tunaweza kuwakilisha jimbo la maswa.......hao wengine kumi waliotofautiana na kaka mkubwa ni akina nan?ebu nipeni majina ili tuanze kujua wasaliti:teeth:
 
- Demokrasia ya kweli inaruhusu viongozi wa siasa au vyama vya siasa kutoa maoni yao binafsi, besides ya msimamo wa chama chao, angalau huyu amesema wazi kuliko wale wanaojinafikisha, tuwaheshimu viongozi wote wanosema waazi misimamo yao bila kuogopa ndio tunaowahitaji katika kutafuta mabadiliko muhimu sana sasa ya kulisogeza taifa letu!

- Kuwatukana na kejeli za mashambulizi ya binafsi ni kuwakatisha tamaa na kuwataka wawe na sura mbili na za kinafiki, at least hapa as a chama unajua where yuo stand with this man on the ishu!

- Kuliko ndio mzee kumbe waongo wakubwa hayo ndio yamelifikisha taifa letu hapa lilipo!

William.
 
Ni mtazamo wake tuu tumvumilie ila ajue kuwa CDM ina msimamo.
Naona kale kadamu ka uccm bado anako tumhurumie
 
Huyu bwana sijamwamini bado kama si mwanasisiemu!

Vyama vya CCM na CHADEMA vimebeba ma mluki wengi sana. Humo CHADEMA wapo wabunge sawa au chini ya 10% ambao ni CHADEMA kweli, including Dr. Slaa, Tundu Lisu na Mnyika. Wengine ni.......

CCM ni Mzee Malechela, Pinda na Dr. Mwakyembe. Wengine ni...........
 
Ni mtazamo wake tuu tumvumilie ila ajue kuwa CDM ina msimamo.
Naona kale kadamu ka uccm bado anako tumhurumie

Hana dhambi, japo anaweza kuwa na kosa. Unajua Mzee wa mapesa aliadhibiwa na Spika Sitta baada ya kutofautiana na wapinzani wenzie......
 
Back
Top Bottom