Picha: Ni kweli na shibuda hamtambui kikwete hii ilikua jana kwenye mnuso wa wabunge

attachment.php


I am speechless.....................to put it mildly.....................kweli this is the height of betrayal..............kula kwa nini....................is his body not more than food?

Dah jamaa nakumbuka amewahi sema adui yake mkubwa ni JK nashanga hapo kuzamia mnuso wa wakoloni weusi
 

Soma hapa alichosema Dr Slaa, nadhani utagundua kwa nini si vibaya kuhudhuria mnuso!

... "Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.
...
Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana."
 
hapa anaonyesha anampa pole kwa misukosuko ya hapa na pale, mara wabunge kususia, mara kuanguka wakati wa kampaini na anamwanyesha kuwa akae chonjo kwa misukosuko zaidi kwani karudi kwa kupitia mjia halali sio kuchakachua!!
 
Huyu anaonekana akimsalimia mwenzake kwa heshma ya ha hali ya juu. Huyu anaesalimiwa ni Kikwete au Rais wa JMT kwa mujibu wa picha hii.

Hakuna ajabu yoyote hapa. Shibuda na JK ni watani na kwa ukweli hasa siasa si uadui wa kusema basi kwa kuwa wewe ni mpinzani wa fulani ukimuona unakunja uso au kuangalia pembeni. Hebu tutenganishe siasa na personal connection. Nina uhakika hata leo hii JK akiitwa pae CCBRT atamkuta Dr Slaa kama mwenyekiti wa Board na kumlaki kwani CCBRT si chama cha siasa. Siasa si uadui na CHADEMA wanachokifanya kama chama cha siasa ni right ila wanachadema individual wana haki na uhuru wa kusalimiana kuongea na yeyote yule.
 
Mimi nina wasiwasi kwamba hiyo picha sio ya huo mnuso, wamechakachua tu, hebu chadema watuambie ukweli
 
Huyu anaonekana akimsalimia mwenzake kwa heshma ya ha hali ya juu. Huyu anaesalimiwa ni Kikwete au Rais wa JMT kwa mujibu wa picha hii.

Mbona akili zenu fupi, CHADEMA HAINA UGOMVI NA KIKWETE, WALA CCM, SISI WOTE NI WATANZANIA NA TANZANIA NI YEU SOTE. CHADEMA HAITAMBUI JK KAMA RAISI KWA SABABU YA TUME YA UCHAGUZI KUCHAKACHUA MATOKEO YA URAIS. JANA JIOINI ILIKUWA SHEREHE YA WABUNGE WOTE WALIOCHAGULIWA NA RAIS JK ALIKUWA KAMA MUALIKWA MWINGINE NA HAKUFANYA SHUGHULI YOYOTE YA KISERIKALI.
 
mbona akili zenu fupi, chadema haina ugomvi na kikwete, wala ccm, sisi wote ni watanzania na tanzania ni yeu sote. Chadema haitambui jk kama raisi kwa sababu ya tume ya uchaguzi kuchakachua matokeo ya urais. Jana jioini ilikuwa sherehe ya wabunge wote waliochaguliwa na rais jk alikuwa kama mualikwa mwingine na hakufanya shughuli yoyote ya kiserikali.

aanhaa kumbe!
 
Ukweli utabaki palepale ujumbe ulifika kwa mabalozi na wahisani, hivyo lengo la Chadema limetimia na CCM hawana la kufanya zaidi ya kutekeleza % kubwa ya matakwa ya Chadema.
 
Huyu anaonekana akimsalimia mwenzake kwa heshma ya ha hali ya juu. Huyu anaesalimiwa ni Kikwete au Rais wa JMT kwa mujibu wa picha hii.

Mwekiti Mbowe katoa tamko BBC kwamba hawana tatizo na Kikwete kama kikwete ila ni njia zilizotumika na tume kumpata rais, bungeni ilikuwa hotuba ya rais na nje ya hapo ni kitu kingine. Nadhani tunapaswa kuelewa ni CHADEMA inakilalamikia na Jana pale bungeni ilikuwa ni mahali pake haswa.
 
nafikiri hii party ilikuwa ya wabunge wote and we have to remember kikwete naye ni mbunge kwa mujibu wa katiba yetu yenye mapungufu ingalikuwa yake angaliifanyia chamwino na siasa sio uadui with reservation may i say shibuda hajafanya kosa labda kama kuna makubaliano ya chadema aliyoyavunja!


Kwani hotuba ya Rais ya ufunguzi wa bunge ilikuwa ya wabunge fulani tu?

Isitoshe, huyu Shibuda alitoa shillingi laki 2 kumchangia pesa za kumsaidia Kikwete kuchukua fomu ya Urais, kumtambua ataachaje?

Uhsbiki unawatokea puani, hakuna cha upiganaji, upiganiaji wala wazalendo. Wanasiasa wa sasa ni mafisadi , wa kuwafunga kengele anasoma elimu ya sekondari.
 
Mbona akili zenu fupi, CHADEMA HAINA UGOMVI NA KIKWETE, WALA CCM, SISI WOTE NI WATANZANIA NA TANZANIA NI YEU SOTE. CHADEMA HAITAMBUI JK KAMA RAISI KWA SABABU YA TUME YA UCHAGUZI KUCHAKACHUA MATOKEO YA URAIS. JANA JIOINI ILIKUWA SHEREHE YA WABUNGE WOTE WALIOCHAGULIWA NA RAIS JK ALIKUWA KAMA MUALIKWA MWINGINE NA HAKUFANYA SHUGHULI YOYOTE YA KISERIKALI.

Ndugu yangu, bora umeliona hili na kulisema !!
Kwani CDM imetangaza kwamba ina uadui na ccm na kikwete? Siasa iliisha baada ya bunge kuahirishwa, hapo walikuwa ktk sherehe ya wabunge wote. Jamani what the heck is wrong with your reasoning ability ?
 
HIYO ILIKUWA NI SHEREHE YA WABUNGE, NA SIO HOTUBA au WAZIRI MKUU KUAPISHWA, ni SHEREHE YA WABUNGE WALIOWEZA KUSHINDA.....Sio MBAYA CHADEMA KUWEPO, WALIKWENDA KUONYESHA USHUJAAA kuwa NAO NI WABUNGE MASHUJAA WALIOSHINDA. Na Kwenye picha ni DK.kikwete Anampongeza Shibuda kuwa Mbunge na SIO SHIBUDA Anampongeza Dk.kikwete....
 
Huyu anaonekana akimsalimia mwenzake kwa heshma ya ha hali ya juu. Huyu anaesalimiwa ni Kikwete au Rais wa JMT kwa mujibu wa picha hii.
Mkuu nadhani una-mislead watu

Haina maana kutomtambua kama rais, basi ni adui na hawapaswi kusalimiana

I believe hata leo slaa akikutana na KJ somewhere watapeana hug, ndivyo siasa zilivyo mkuu... MBONA UNAKUA ANFAAL SANA
 
Sina hakika kama watu wanajua mantiki ya CHADEMA na WATETEA HAKI WOTE dhidi ya demokrasia bakaji!!
MKUU... ni upeo mdogo wa akina afaal ndio unaochanganya wengine wachache... kisiasa watu wanweza kupingana na kutohudhuria hafla au dhifa lakini ile ni "position statement", na pale wanapokutana nje na institutions mambo yanakua kama kawaida

I was lucky ile kipindi karamagi amejiuzulu nikakutana naye na selelii airport tukienda mwanza (ile ndege ya saa kumi na mbili asubuhi), what i saw was stunning... karamagi made a coffee for selelii and selelii pulled a chair for karamagi. kwa mtu asiyejua siasa angeanza kurusha vyupa

KUNA NYAKATI ZA KILA TUKIO
 
mi sioni tatizo kuhudhuria mnuso kwani kulikuwa na hotuba ya Rais ? mana akihutubia tu kama rais sisi tunasepa ajiandae akija arusha,mwanza,kigoma,shinyanga,karatu kutopokelewa na mameya
 
Ni mpelelezi tu, ameenda kusikia wanawazungumziaje wanamapinduzi wa CHADEMA.
 
Tofauti za kisiasa siyo uadui. "Asante kwa kutupongeza, asante kwa chakula lakini bado tuna mawazo tofauti kisiasa, haturidhishwi na yaliyotokea", kuna ubaya gani kumwambia rais mambo hayo. Mimi naona Shibuda is right. Upinzani wa uadui kama ule wa CUF na CCM kule Pemba wa kususiana hadi misiba ni ulimbukeni wa kipumbavu.
 
Back
Top Bottom