PICHA: Ndege mpya za Fastjet hizi

PICHA: Ndege mpya za Fastjet hizi

Sidhani hata kama hata anajua hizo ndege. Atakuwa amesikia watu wanaponda na yeye amejiunga nao as long ni wa chama kimoja. Watanzania sijui lini tutaanza kuthamini vitu vyetu.

Kiukweli mkuu....mambo ya siasa vijana wengi wameyajua kuanzia 2005-10,ila nashangaa upinzani sasa umekua uadui wala sio democracia.....kushabikia vya wenzetu ni ushamba....
 
Tumepata rais mwanamiundombinu, kule bandari, kule reli, kule ndege, barabara ndio usiseme..
 
Tunasahau kuwa Fastjet wameamua kuleta ndege ndogo baada ya "kulost".
Huu ni ushahidi kuwa ndege kubwa hazifai kwa safari fupi za ndani.
Na huu ni ushahidi dhidi ya wale waliokuwa wanalilia "tungenunua airbus kama za fastjet".
Ni lazima sasa kundi hilo likiri kua walipotoka. Na kuwa ndege ndogo na za kati ndo mpango mzima kwa safaei za ndani na sio zile kubwa.
Hata precission walichemsha na ile jet yao mapema sana.

Na vile vile kuna mashirika mengi sana ya ndege yanarusha hayo "mapanga shaa" na wabongo wanapanda...lakini kwa kuwa ni cha serikali ishakuwa nongwa...watu hao hao wanapanda panga shaa la ethiopiana kwa tabasam na raha tele na wanashuka JKNIA kwa swagger....lakini ya serikali matusi..
Na precission kila walivyokuwa wanaongeza "mapanga" mapya tuliwasifu sana.....na nyuzi ziko hapa jukwaani. Watu hao hao leo matusi yake hayasemeki kama vile kununua "mapanga" ni dhambi kubwa.
Tuache unafiki na tubadilike.

Maswala yangu yanayonipa wasiwasi ni ishu za menejiment ya ile kampuni...kampuni iliyooza, je kampuni ile itaweza?

The Boss nakupa changamoto, Emirates ni kampuni ya ndege maarufu sana....je unajua ilianza na ndege ngapi miaka ya 80?
Menejiment na weledi wa biashara. Hili jambo sisikii likiongelewa. Tunatukana ndege weeee...hata ukipewa airbus mpya 100 kama huna menejiment nzuri utachemsha ndani ya miaka 5.

Tunavyoanza kujenga nchi, kujenga uchumi tujielekeze kwenye viopaumbele halisi..na sio chuki kwa serikali pekee.
Issue si kuwa na Airbus kama za fastjet, bali ndege ndogo za :-

1.Jet engine
2. Bei nafuu na gharama ndogo za uendeshaji.
3. Kubeba abiria 100 - 180.
4. Kutua kwenye viwanja vingi nchini.
5. Kusafiri umbali wa masafa mafupi na kati.

ndege za kampuni ya Embraer ya Brazil inatikidhi vigezo hivi, na ndio maana fastjet wanaoleta kupambana na tudege twenu twa pangaboi.
 
Wee ni mganda?
 
Ambacho hamuelewi wengi ni kwamba kwa sababu ya engine za jet embraer ina limit ya kutua viwanja wenye lami tu.hata pale mwanza pakitokea ile midege inayoruka ruka imedata na kusambaa airport basi emmbraer haitaweza kutua wala kupaa.ATCL wameanza na nadhani juzi waliingia makubaliano ya kununua Bombardier CS300 mbili ambazoni jet.Kumbukeni ATCL wamekodi CRJ 200 ambazo ni jet mnazozipenda nyinyi
 
Hizi ndo ndege unazinunua unaweza kujisifia siyo yale mapangaboi.
 
Sio kwamba Jast jet akija na hizo ndege,ndio Atcl itashindwa kufanya vyema,Itafanya vyema sana tu km uongozi utakuwa mzur katika kusimamia mapato.
 
Interesting.....

tuone 'mapanga shaa' na hizi nani zaidi
Nasikia mapanga inaconsume sana mafuta ila ni safe kwa kuwa haihitaji mazingira rafiki sana kwenye landing na kupaa...najaribu kuwaza kivivu tu kwamba uendeshaji wake utakuwaje kwenye soko hili lenye ushindani mkubwa?
 
Kwa msaada tu mkuu, siyo kweli kwamba consumption kubwa ni mapanga shaa. Pili, mtumiaji yoyote anachukua kitu kwa matumizi yake na si ya mwingine. Ukiwa na mtoto mchanga utahitaji nepi ama diapers kwa hiyo siyo vema ama busara mtu akakukuta dukani ukinunua nepi akuambie kwa nini usinunue suruali bana!! Viwanja vyetu vingi haviwezi kuhudumia ndege kubwa kwa hiyo tukiwa na dhamira ya kuwahudumia wa TZ wengi kwa usafiri wa anga mapanga shaa ndiyo yanayofaa kwa sasa.
 
Samahani mkuu nauliza tu kivivu hapa...ina maana tuki improve usafiri wa anga maisha ya mtanzania yatakuwa yamepaa automatically? Kwamba maisha ya Mtanzania yalikuwa yamezorota kwa kuwa usafiri wa anga ulikuwa na mushkeli?
 
Mi sipandi ndege ambayo imenunuliwa kwa kuacha kununua dawa hospitali au kutengeneza madawati.

Kila kitu kina mchango wake kwenye Taifa. Matatizo hayawezi kuisha, you can say the same na ujenzi wa Daraja, Barabara, Reli etc
 
Binafsi naona Irkut MC-21 au Sukhoi SuperJet SJJ-100 ni bora zaidi kuliko Embraer, Serikali yetu ingie kwenye mazungumzo na moja ya makampuni hayo ili at least ifikapo mwaka kesho tuweze kununua ndege aina ya jet hata moja ya kisasa kwa kuanzia.
 
Back
Top Bottom