PICHA: Ndege mpya za Fastjet hizi

PICHA: Ndege mpya za Fastjet hizi

Samahani mkuu nauliza tu kivivu hapa...ina maana tuki improve usafiri wa anga maisha ya mtanzania yatakuwa yamepaa automatically? Kwamba maisha ya Mtanzania yalikuwa yamezorota kwa kuwa usafiri wa anga ulikuwa na mushkeli?
La hasha, ni kumjengea Mtanzania huyohuyo mazingira rafiki ili aweze kufikia malengo yake. Mfano rahisi tu ukiweka uwezekano wa kuwa na usafiri wa anga kila mkoa wa Tanzania, unawajengea wananchi njia rahisi ya kuweza kusafiri wao wenyewe na hata mizigo yao. Kikawaida, wachumi wanafikiria kuwa uamuzi wa mteja hufikiwa baada ya kulinganisha mambo kadhaa na faida au hasara zake ndipo mtu ataamua ama afanye au asifanye. Chukulia jambo la kawaida tu kama sherehe ya harusi kwa mtu alnayeishi Songea na harusi iko Same. Most likely kwa mazingira ya sasa ni kuwa ama aombe likizo bila malipo ya wiki mbili ili aweze kuhudhuria, au asihudhurie kabisa. Kama kuna usafiri wa ndege inamchukua saa kadhaa kuwa Same na saa kadhaa kurudi kituo cha kazi.
 
Tatizo wabongo tuna makelele mengi sana....mara kwa nini tumenunua ndege...mara kwanini bombadier na sio jet?
Kama una uwezo wa kununua vitz utanunua vitz tu...Range rover utaishia kuitazama ikipita.

Lakini kununua vitz sio sawa na kununua baiskeli..tumenunua q400 mbili kwa uwezo wetu..wacheni zipige kazi
 
Tuna afford?
 
Ukisema uwezo ina maana jinsi miaka inavyozidi kusonga mbele uwezo wa tanzania unapungua.....mana ukiangalia ndege za zamani zilikuwa kubwa ukilinganisha na mabanga shaa.
 
Interesting.....

tuone 'mapanga shaa' na hizi nani zaidi
Nani zaidi kwa mlinganisho huu (Bombardier Q400 na Embraer 190), "The Boss":

1) BEI: Q400 ni rahisi kwa $19. 2m

2) GHARAMA YA MAFUTA: Q400 hutumia mafuta pungufu ya gharama kwa $6.25 kwa kila maili hewani

3) UMBALI WA KURUKA BILA KUTUA: E190 huruka mbali zaidi kwa maili 488 hewani

4) UMBALI WA JUU HEWANI: E190 hufika futi 16,000 usawa wa bahari juu zaidi

5) UWANJA: Q400 huitaji uwanja mfupi kwa futi 643 kupaa wakati E190 huhitaju pungufu ya futi 199 kutua.

6) ABIRIA: E190 huweza kubeba abiria 24 zaidi
 
Kupeana kazi kwa kujuana kunaanza na ukada. Wa juu wakishawekwa makada na chini kunafata. Ingelikua sio wanasiasa wanahusika wangeshakemea mapema sana
Kwa kiasi fulani ningekubaliana nawe kama ungesema kuwa kuingiliwa madaraka kwa viongozi waliokuwa ATC pia kulichangia kuliangusha shirika. Mfano mzuri ni ule wa Alliance. ushirika ule ulipingwa sana lakini haukufua dafu.
Jingine ni aina ya ushirika na SA nao vile vile ulipingwa na wataalam lakini nalo halikusikilizwa.
Kwenye shirika hili jipya mfano bora wa kuiga ni ule wa ET ambao katika kipindi chote cha misukosuko ya siasa ethiopia shirika hilo liliendelea vizuri mpaka ikafikia kuwa ni chanzo cha mapato ya kigeni kikubwa tu. Siri kubwa ilikuwa ni kuwaachia wataalam waliendeshe. Hivyo ushauri wangu kwenye shirika hili jipya serikali iwe 'eyes on hands off policy'
 
Back
Top Bottom