PICHA: Mapokezi ya Prof Lipumba; Afande sele atumbuiza

Hivi kwanini VINEGA ni wepesi kushutumu wenzao kuwa wadini, lakini hawana ujasiri wa kukiri ukristo ulioshamiri kwenye chama chao?
 
Nilishawahi kusoma Article zake mbili kuhusu uchumi wa Africa kweli huyu jamaa ni kichwa cha uchumi.Ila sijui kwa nini nchi zetu hizi za africa huwa hazitumii ipasavyo wataalam wetu.

vitu anavoandika huyu JK hawezi kuelewa hata paragraph moja ...
 
Aliwahi kupewa nafasi wakati wa mwinyi...akachemsha! Li pumba

Hapana hakuchemsha mkuu! Ila unajua hawa jamaa zetu wakishaingia ikulu washauri wao wanaowasikiliza ni akina Shekh Basaleh. Nina uhakika kama Prof angefanya kazi na serious president kama Mkapa, nchi hii ingekuwa mbali.
 
Mkuu kumbe na wewe una madongo.

Kiukweli Prof Lipumba ni mtu makini, Dunia ndio inajua umhuimu wake.

Hakuna ubishi kuwa jamaa ni kichwa, nadhani hata Uganda walimtumia. Lakini kwetu watu wanaingia ikulu na ajenda za mahakama ya kadhi na OIC (Badala ya kuwatumia akina Lipumba wao wanawatumia akina Shekh Yahya na akina Shekh Basalehe). JK anaulizwa kwa nini nchi yako ni masikini, yeye anajibu "hata mimi sijui"
 
mhh kweli inasikitisha kuona mtaalamu anasaidia kuimalisha uchumi wa nchi za wenzetu ili hali wa Tanzania tunadidimia kila kukicha mungu ibaliki Tanzania,kalibu nyumbani Proff Lipumba.:lock1:


Hamtaki kumtumia,mnaleta siasa hata ktk maswala ya utumiaji rasilimali watu
 
Kama sikumbuki enzi za mwinyi ndoo ulikuwa wakati wa Ruksa.Basi kumbe hakuchemsha bali alibadilisha mfumo wa uchumi kuutoa kwenye ujamaa wa nyerere wa raia kukatazwa kumiliki mali na kujizalishia kipato binafsi na kuupeleka ubepari ambapo ikawa rusksa raia kumiliki mali na kuzalisha uchumi kwa kilka mtu nanafsai yake.Ni wakati ambapo pesa ilianza kupatikana kwa wingi kwa wananchi.LIPUMBA LIWEZA baada kuona kupitia kwake mambo yanwezekana wakaamua kumuondoa ili watyu wasijewakamsifu na kumpa sifa yeye.

mkuu na hilo ndilo tatizo kubwa tulilonalo,kwani pindi mtu afanyavyo vyema basi hupenda kumwondoa haraka iwezekanavyo eti atapata sifa kwa kazi aliyofanya.

nadhani umefika wakati kuwatumia hawa wasomi wetu pasi kuangalia yupo chama kipi,nakumbuka pale UDSM na SUA wale wote walio kuwa kinyume na matakwa ya chama husika walinyimwa mkataba wa kuendelea kufundisha,sasa huwa najiuliza nani anae komolewa pale? ni chama,mhusika,chuo ama wanafunzi?
 
Karibu nyumbani Professor.Lakini hatutaki mapokezi yake yahusishwe na siasa.Nitakwenda nikikuta bendera ya chama chochote narudi nyumbani.

Mbona misiba yenu mnafunika bendera zenu na tunakuja? CCM na CDM mna tabu sana!
 
Mnatualika tukampokee hivi ndo anakuja na huo uchumi? wenzenu walipigwa risasi wakafa kwa ajili ya kumtetea sefu, leo sefu anawadhihaki maskini marehem, nanyi mnaleta ngonjera za lipumba kichwa lipumba kichwa! sera za cuf alimkabidhi kikwete siku akiapishwa, pangekuwa na sera za ukombozi wa kiuchumi mle kikwete angesha zitumia, mbona kaelekezwa na kichuguu slaa kuhusu ubovu wa sheria ya mabadiliko ya katiba fasta kapeleka mabadiliko bungeni kidhihiriza mibunge ya ccm ni mizoba na sasa angalau angalau. kuwa na mlima kilimanjaro lipumba ni hasara kwani akili zetu zinafikiria na kuushangaa unaodhaniwa ni bora wa mchumi bora kumbe inawezekana hamna kitu. mimi siendi kumpokea, kama uraia nifuteni!!!!!!
 
jamani nipo hapa uwanja wa ndege kumefurika wanachama wa cuf........waliosema cuf imekufa leo sijui mtajificha wapi watu wamejaa wakimsubili mkubwa na bigwa wa uchumi duniani
 
Back
Top Bottom